Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
10 Julai 2020, 09:24:16

Dawa ya Voriconazole
Voriconazole ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyoko katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi. Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Vfend.
Rangi ya dawa
Voriconazole huwa mara inatofautiana na mara nyingi utegemea aina ya kiwanda kinachotenegeneza.
Fomu na uzito wa dawa
Voriconazole hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu,
50
200
Voriconazole hupatikana katika fomuya maji wenye ujazo wa;
Miligramu 200 kwa mililita 5 za maji (200mg/5ml)
Voriconazole hupatikana katika fomu ya maji ya sindano kwa ujazo wa 200mg/ml
Ufanyaji kazi wa Voriconazole
Dawa jamii ya Antifangasi ikiwa pamoja na Voriconazole hufanya kazi zifuatazo ili kutibu fangasi.Dawa ya Voriconazole ni aina ya dawa kutoka kundi la antifangasi, Dawa hii hufanya kazi zake kwa kuingilia kimeng;enya muhimu kwenye ini kinachoitwa saitokromu P-450.kimeng’enya hichi hubadili kiunda cha lanosteroli kwenda ergosteroli. Ergosteroli ni homoni muhimu sana inayotengeneza vijenzi vya ukuta wan je wa seli ya fangasi. Kukosekana kwa homoni hii hupelekeakuta za seli ya fangasi kuwa dhaifu na hivyo kupoteza maisha na kutozaliwa kwa seli mpya.
Dawa zinazofanana
Voriconazole ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:
Amphotericin B
Butoconazole
Capsofungin
Ciclopiro
Econazole
Flucytosine
Griseofulvin
Itraconazole
Miconazole
Naftifine hydrochloride
Nystatin
Oxiconazole nitrate
Sulconazole nitrate
Terbinifine
Terconazole
Tioconazole
Tolnaftate
Voriconazolehutibu nini?
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi.
Hutumika kwenye matibabu ya fangasi kwenye mfumo wa umeng'enyaji wa chakula uliyosababisha na Kandidiasi.
Dawa mwiko kutumika na Voriconazole
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Carbamazepine
Chloroquine
Cobimetinib
Conivaptan
Dihydroergotamine
Dihydroergotamine intranasal
Efavirenz
Eliglustat
Ergotamine
Flibanserin
Ivabradine
Lefamulin
Lomitapide
Lovastatin
Lurasidone
Naloxegol
Phenobarbital
Pimozide
Quinidine
Regorafenib
Rifabutin
Rifampin
Ritonavir
Sirolimus
Venetoclax
Wagonjwa mwiko kutumia Voriconazole
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Wagonjwa wenye Magonjwa ya figo
Upekee wa Voriconazole
Dawa hii hutolewa mwili kwa njia ya Ini kwa asilimia kubwa na kwa njia ya mkojo.
Matumizi kwa mama mjamzito
Dawa hii hushauriwa kutumika kwa hali ya hatari ambapo hamna dawa nyingne mbadala wakati wa kipindi cha ujauzito.Takwimu zinaonyesha kuwa dawa hii husababisha ujauzito kutoka.
Matumizi kwa mama anayenyonyesha
Takwimu hazijaonyesha kuwa kuna uwezekano wa hii dawa kuingia au hapana kwenye maziwa ya mama ila itumike kwa wamama wajawazito kwa uangalifu.
Maudhi ya Voriconazole
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;
Kichefuchefu
Kutapika
Maumivu ya tumbo na kichwa
Kizunguzungu
Kuharisha
Shinikizo la juu la damu
Shinikizo la chini la damu
Kupata homa
Mapigo ya moyo kwenda haraka
Kupata maruerue
Kuogopa mwanga
Kuwashwa mwili
Je kama utasahau dozi yako ufanyaje?
Kama ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:55:27
Rejea za mada hii:-