Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
4 Mei 2020 23:22:15
Famotidine
Famotidine ni dawa ambayo huzia tindikali isizalishwe kutoka kwenye seli za ukuta wa tumbo zinazoitwa gastrini. Dawa hii iliyopo kwenye kundi la dawa zinazozuia H2 risepta antagonisti, huzuia kemikali ya histamine ambayo huchochea kutengenezwa kwa tindikali tumboni isishiriki katika kazi hiyo.
Hivyo dawa hii hutumika kutibu matatizo mbalimbali yanayotokana na tindikali ya tumboni.
Majina ya kibishara ya Famotidine
Pepcid
Famotidinum
Brolin
Gastro
Apogastine
Gastrodomina
Gastrosidin
Fomula ya kikemikali
Famotidine hufahamika kikemikali kama C8H15N7O2S3
Jina la kisayansi (IUPAC) la Famotidine
3-[[2-(diaminomethylideneamino)-1,3-thiazol-4-yl]methylsulfanyl]-N'-sulfamoylpropanimidamide
Famotidine hutibu nini?
Matibabu ya vidonda vya tumbo
Matibabu ya Kiungulia
Matibabu ya Kucheua tindikali
Kutibu michubuko kwenye koo la chakula vilivyo sababishwa na michubuko ya tindikali (kiungulia).
Husaidia kuzuia damu kuvuja kwenye njia ya juu ya mfumo wa chakula
Hutumiwa wakati mgonjwa akipewa dawa ya usingii kwa dharura ili kuzuia mgonjwa asipaliwe na tindikali kutoka tumboni
Kutibu sindromu ya Zollinger-Ellison
Dozi za Famotidine
Vidonge
Miligramu 10
Miligramu 20
Miligramu 40
Dawa ya kimiminika
Miligramu 40 kwa mililita 5
Dawa ya kuchoma kwa sindano
Miligramu 10 kwa mililita
Miligramu 0.4 kwa mililita
Namna ya kutumia Famotidine
Tumia kama utakavyo elekezwa na daktari.
Matumizi yanategemea ni hali gani inatibiwa na hali ya mgonjwa.
Dawa hii inaweza kutumiwa pamoja na au bila chakula.
Namna Famotidine inavyofanya kazi mwilini
Dawa hii huzuia risepta za H2 kupokea homon ya histamine ambayo huchochea kutengenezwa kwa tindikali tumboni
Kwa kufanya hivyo dawa hii huzuia utengenezaji wa tindikali tumboni na hivyo kusaidia kutibu magonjwa na hali mbalimbali kutokana na uzalishaji wa tindikali ya tumboni.
Mwili unachofanya kwa Famotidine
Asilimi 45 tu ya dawa hufyonzwa na kuingia kwenye damu baada ya kumeza dawa.
Huanza kufanya kazi kati ya saa 1 hadi 4 baada ya kumezwa.
Hufanya kazi mwilini kwa saa10 hadi 12.
Huchakatwa na mwili kwenye ini ili iweze kufanya kazi na kuondolewa sumu.
Sehemu kubwa ya taka mwili ya dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo.
Maudhi madogo madogo ya famotidine
Maumivu ya kichwa
Kizunguzungu
Kutopata choo
Homa
Mwili kufa ganzi
Kuchoka
Kuwashwa
Mdomo kukauka
Kichefuchefu
Tumbo kuuma
Kuchanganyikiwa hususani kwa wazee.
Mara chache inaweza kupunguza uwezo wa kufanya tendo kwa wanaume.
Famotidine marufuku kutumika kwa
Wagonjwa wenye aleji na dawa ya fomatidine.
Tahadhari wakati wakutumia fomatidine
Matumizi ya fomatidine kwa wazee na wenye shida ya figo dawa hii inaweza kusababisha yafuatayo;
Kuchanganyikiwa
Kuona maruweruwe
Kupata degedge
Mwili kukosa nguvu
Kwa wagonjwa wenye saratani ya tumbo, kupata nafuu wakati antumia dawah ii haimaanishi kua saratani imetibka.
Muingiliano na dawa nyingine
Famotidine isitumike pamoja na dawa zifuatazo kwani huzuia ufyonzwaji wa dawa hizo;
Dasatinib
Delavirdine mesylate
Cefditoren
Fosamprenavir
Ikitumika pamoja na tizanidine ina weza kusababisha shinikizo la la damu kushuka, mapigo ya moyo kuwa taratibu na mwili kukosa nguvu
Dawa zifuatozo hupunguza ufyonzwaji wa famotidine:
Sodium bicarbonate
Calcium carbonate
Magnesium dihydroxide
Magnesium carbonate
Magnesium trisilicate
Aluminium hydroxide
Metoclopramide
Matumizi ya Famotidine wakati wa ujauzito
Ni vyema kuepuka matumizi ya Famotidine wakati wa ujauzito kwa hakuna taarifa/tafiti za kutosha juu ya madhara yake kwa mtoto aliyeko tumboni wakati wa ujauzito. Ikibidi kutumia dawa hii basi uzito wa faida kwa mama na madhara kwa mtoto unabidi uzingatiwe.
Matumizi ya Famotidine wakati wa kunyonyesha
Pia ni vyema kuepuka matumizi ya dawa hii wakati wa kunyonyesha kwani hufika kwenye maziwa ya mama na inaweza kusababisha madhara kwa mtoto anaenyonya. Daktari anaweza kutumia dawa nyingine zenye manufaa zaidi na ikilazimu kutumia famotidine basi uzito wa faida kwa mama na madhara kwa mtoto unabidi uzingatiwe. Moja ya njia ya kutatua utata kama huu ni mtoto kuachishwa kunyonya kama mama atatumia dawa ya kumdhuru mtoto anaye nyonya.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:55
Rejea za mada hii:-