top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

15 Aprili 2020, 09:31:03

Fluoride

Fluoride

Floraidi (fluoride) ni madini yanayohifadhiwa kwa wingi kwenye meno na mifupa. Madini haya hutumiwa na wataalamu wa meno kuimarisha ukuta wa meno uitwao enemo ili usishambuliwe na vimelea wa meno.


Floraidi huweza kupatikana kwenye vyanzo asilia mfano ni;


  • Maji

  • Udongo

  • Mimea

  • Miamba

  • Hewa


Madini haya hutumiwa na wataalamu wa meno kuimarisha ukuta wa meno uitwao enemo ili usishambuliwe na vimelea wa meno.


Madini ya floraidi huwekwa kwenye dawa nyingi za meno,vimiminika vya vkusukutulia kinywa n.k


Faida za madini ya Floridi kwenye afya ya meno


  • Huweza kuimarisha ukuta wa meno wa Enemo kama ni dhaifu

  • Hupunguza kiasi cha upungufu wa madini kwenye enemo

  • Huzuia meno kuoza

  • Huzuia ukuaji wa bakteria kwenye meno

  • Fluoraidi inapotumika kupita kiasi huweza kusabababisha madhara yafuatayo;

  • Rangi ya meno kuwa na madoa na kupoteza rangi ya weupe, huweza kuwapata watoto ambao meno yao ya utu uzima yanaanza kuota, hivyo unapaswa kumsimamia mwanao wakati wa kuswaki ili asitumie maji yenye madini haya kwa wing.

  • Mifupa ya Skeletoni kuwa na rangi ya madoa kutokana na wingi wa Fluoride, hii huweza kupelekea maumivu kwenye jointi na kukaza kwa jointi.

  • Maumivu ya mifupa yanayoweza kuwa sehemu moja ya mwili au mwili mzima.

  • Watoto kuzaliwa na madhaifu ya mifupa


Kuepuka athari za fluoride



Kupunguza athari hizi za Fluoride tumia maji ambayo hayana madini haya kwa wingi au kuchemsha maji ya kunywa na kupikia.

Pia kuepuka kutumia kwa wingi dawa za meno zenye Fluoride kwa wingi

Mfano mtu anaweza tumia maji yenye Fluoride kwa wingi na bado akatumia dawa ya meno yenye Fluoride kwa wingi

Hii huweza kuleta athari zilizotajwa hapo juu

Kama upo kwenye vyanzo vya maji ambavyo havina Fluoride unapaswa kununua dawa za meno zenye madini hayo ili usipitwe na madhara ya upungufu wa madini haya

Lakini kama upo kwenye maji yenye madini ya Fluoride unapaswa kutumia dawa ya meno yenye Fluoride kidogo au ambayo hayana madini haya kabisa.


Baadhi ya vinywaji na vyakula vyenye madini ya Floraidi


  • Chai ya rangi iliyopikwa kwa maji ya bomba

  • Juisi ya zabibu

  • Soda za machungwa

  • Samaki aina ya shrimp

  • Divai

  • Kahawa

  • Spinach zilizopikwa

  • Viazi vilivyochemshwa

  • Karoti zilizopikwa

  • Wali mweupe


Maeneo gani Tanzania yana madini ya floraidi kwa wingi?


Kutokana na tafiti mbalimbali inaonyesha kuwa mkoa wa Arusha katika wilaya ya meru, Longido, na wilaya ya Arusha ina madini ya floraidi kwa wingi sana. Kiwango cha kawaida cha madini haya kwenye maji kilichopendekezwa kutumika kwa binadamu na shirika la afya duniani- WHO ni miligramu 1.5 kwa kila lita ya maji. Cha kushangaza kiwango cha maji asili katika wilaya za Longido na Meru ni miligramu 20 kwa kila lita moja ya maji. Wananchi katika eneo hili wanabidi kuwa makini ili kuzuia madhara yanayotokana na kutumia madini ya floraidi kwa wingi.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021, 11:33:03

Rejea za mada hii:-

1.MyFoodData.Fluoride.https://www.myfooddata.com/articles/high-fluoride-foods-and-drinks.php. Imechukuliwa 14/4/2020

2.HealthLine.Fluoride.https://www.healthline.com/health/what-is-fluoride. Imechukuliwa 14/4/2020

3.MedicalNewToday.Fluoride.https://www.medicalnewstoday.com/articles/154164. Imechukuliwa 14/4/2020

4.MedicalNewToday.Fluoride.https://www.webmd.com/vitamins/ai/ingredientmono-1068/fluoride. Imechukuliwa 14/2020
bottom of page