top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

22 Aprili 2020 05:10:02

Fosinopril

Fosinopril

Fosinopril ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la dawa linaloitwa angiotensini konventing enzaimu inhibita- ACEIs.


Fomu na uzito wa Fosinopril


Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Monopril na inapatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu,


 • 10mg

 • 20mg na

 • 40mgUfanyaji kazi wa Fosinopril


Namna dawa inavyofanya kazi kupunguza shinikizo la damu.


Dawa jamii ya ACEIs ikiwa pamoja na fosinopril hufanya kazi zifuatazo ili kupunguza shinikizo la damu

Kutanua kipenyo cha mishipa ya damu ya vena na ateri kwa kupinga utengenezaji wa homoni ya angiotensin II na uvunjwaji wa bradykinin. Kutanuka kwa mishipa husababisha mishipa kuwa na kipenyo kikubwa hivyo kushuka kwa shinikizo ndani ya mishipa na matokeo yake ni kupunguza mzigo wa damu unaoingia na kutoka kwenye moyo na kupunguza utendaji kazi wa moyo kupita kiasi.


Dawa zilizo kundi moja na Fosinopril


Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:


 • Benazepril

 • Captopril

 • Enalaprili

 • Lisinopril

 • Moexipril

 • Perindopril

 • Quinapril


Fosinopril hutibu nini?


Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu

Hutumika kwenye matibabu ya moyo ulioferi


Usitumie Fosinopril na daw again?


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo


 • Valsartan

 • Tolmetin

 • Telmisartan

 • Sulindac

 • Salsalate

 • Sacubitril/valsartan

 • Sacubitril/valsartan

 • Pregabalin

 • Piroxicam

 • Oxaprozin

 • Olmesartan

 • Naproxen

 • Nabumetone

 • Meloxicam

 • Mefenamic acid

 • Meclofenamate

 • Losartan

 • Lofexidine

 • Ketorolac

 • ketoprofen

 • Irbesartan

 • Indomethacin

 • Ibuprofen

 • Flurbiprofen

 • Fenoprofen

 • Etodolac

 • Eprosartan

 • Diflunisal

 • Diclofenac

 • Celecoxib

 • Candesartan

 • Azilsartan

 • Aspirin

 • Aliskiren


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Fosinopril


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:


Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au dawa jamii ya ACEIs


Tahadhari ya Fosinopril


Dawa hii inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;


 • Wagonjwa wenye shida ya ini

 • Wagonjwa wenye shida ya figo

 • Wagonjwa wenye hatari ya kupata haipakalemia


Matumizi ya Fosinopril kwa mama mjamzito


•Haipaswi kutumika kwa mama mjamzito kwa sababu husababisha athari kwa mtoto tumboni. Madhara hayo kwa mtoto ni haipotension, haipoplezia ya fuvu, anyuria, kuferi wa figo na kifo.


Matumizi ya Fosinopril kwa mama anayenyonyesha


Haishauriwi kutumika kwa mama anayenyonyesha kwa sababu huingia kwenye maziwa ya mama.


Maudhi ya Fosinopril


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na;


 • Maumivu ya kichwa

 • Kutapika

 • Kizunguzungu

 • Haipakalemia

 • Othorstatik haipatesheni

 • Maumivu ya kifua

 • Kikohozi kikavu

 • Vipele kwenye ngozi

 • Kuharisha

 • Mwili kuishiwa damu

 • Mwili kuchoka


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau kutumia Fosinopril, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:33:23

Rejea za mada hii:-

1.Drugs.fosinopril.https://www.drugs.com/mtm/fosinopril.html. Imechukuliwa 21/4/2020

2.Medscape.fosinopril.https://reference.medscape.com/drug/monopril-ranfosinopril-fosinopril-342328. Imechukuliwa 21/4/2020

3.WebMd.fosinopril.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-6036/fosinopril-oral/details. Imechukuliwa 21/4/2020

4.MedicinePlus.fosinopril.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a692020.html. Imechukuliwa 21/4/2020

5. Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasa wa 210-213

6.RxWiki.https://www.rxwiki.com/fosinopril. Imechukuliwa 21.02.2020
bottom of page