Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
23 Aprili 2020 08:37:43
Glicazide
Glicazide ni dawa mojawapo iliyo kwenye kundi la sulfonylurea inayotumika kushusha kiwango cha sukari ya damu kwa wagonjwa wa sukari.
Majina mya kibiashara ya Glicazide
Diabrezide
Diaglyk
Diaikron
Diamicron
Gen Gliclazide
Gen-Gliclazide
Gliclazide
Gliklazid
Glyade
Glyclazide
Fomula ya kikemikali ya Glicazide
C15H21N3O3S
Jina la kikemikali la Glicazide
1-(3,3a,4,5,6,6a-hexahydro-1H-cyclopenta[c]pyrrol-2-yl)-3-(4-methylphenyl) sulfonylurea
Muonekano wa Glicazide
Ni dawa ya kidonge inaweza kuwa na umbo na rangi mbalimbali kulingana na kiwanda kinachozalisha.
Namna ya kutumia Glicazide
Tumia kama utakavyo elekezwa na daktari wako. Unashauriwa kumeza baada ya kula ili kuepuka hatari ya sukari kushuka kupita kiasi.
Ufanyaji kazi wa Glicazide
Inachochea seli beta za kongosho kuzalisha insulin ambayo ndiyo hushusha sukari ya damu.
Inapunguza kasi ya ini kutengeneza sukari
Inaongeza uwezo wa ufanisi wa vipokezi vya homoni ya insulin kwenye seli za mwili hivyo insulin kufanya kazi vizuri.
Utoaji wa Glicazide mwilini
Takamwili za mabaki yake hutolewa kwa njia ya mkojo na kwenye kinyesi.
Muingiliano wa Glicazide na dawa nyingine
Dawa hizi huweza kuongeza ufanisi wa dawa ya gliclazide:-
Maudhi ya Glicazide
Kutapika
Kichefuchefu
Kutapika
Maumivu ya tumbo
Madhara ya Glicazide
Kushusha sukari kupita kiasi. Unashauriwa unapotumia dawa hii kutembea na vyakula kama pipi, juisi au biskuti na ule pale unapoona dalili za sukari kushuka kupita kiasi. Dalili hizi ni kama mwili kuchoka na kuishiwa nguvu,kizunguzungu kichwa kuuma.
Tahadhari ya Glicazide
Atari ya sukari kushuka kupita kiasi nirahisi kuwapata wagonjwa wafuatao;
Wazee
Wagonjwa wenye upungufu wa virutubisho mbalimbali (utapia mlo)
Wagonjwa wenye matatizo ya figo
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Glicazide
Marufuku kutumiwa na wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wa sukari inayotibika kwa insulini pekee (sukari aina ya kwanza)
Wagonjwa ambao ini linashindwa kufanya kazi
Wagojwa ambao figo zinashindwa kufanya kazi.
Matumizi wakati wa ujauzito na kunyonyesha
Glicazide haitumiki kwa mama mjamzito kwani inaweza kumuathiri mtoto aliyeko tumbomboni huswa wakati wa kuzaliwa. Pia haitumiwi na mama anaenyonyesha kwani inaweza kushusha sukari ya mtoto anae nyonya.
Mama mjamzito atabadilishiwa dawa kama vile kutumia insulini kwa namna atakavyo ona daktari wake.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:33:31
Rejea za mada hii:-