top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

23 Aprili 2020, 08:56:09

Glimepiride

Glimepiride

Glimepiride ni dawa inayotumika kwenye matibabu ya wagonjwa wa kisukari aina ya pili. Dawa hii inanguvu zaidi ya kushusha kiwango cha sukari kwenye damu na kufanya kazi kwa muda mefu zaid na ipo katika kundi la kizazi cha tatu cha dawa jamii ya sulfonylurea.


Majina mya kibiashara ya Glimepiride


  • Amarel

  • Amaryl

  • glimepiride

  • glymepiride


Fomula ya kikemikali ya Glimepiride


  • C24H34N4O5S


Jina la kisayansi la Glimepiride


4-ethyl-3-Methyl-N-[2-[4-[(4-methylcyclohexyl) carbamoylsulfamoyl] phenyl] ethyl]-5-oxo-2H-pyrrole-1-carboxamide


Fomu na uzito wa Glimepiride


Dawa hii hupatikana katika vidonge vya milligram;


  • 1mg

  • 2mg

  • 4mg


Wagonjwa wanaopaswa kutumia Glimepiride


Wagojwa wa sukari ambao mazoezi na mlo havitotoshi kurekebisha kiwango cha sukari cha damu.

Wagonjwa ambao dawa moja kama metformin na insulin haitoshi kusha kiwango cha sukari kwenye damu.


Matumizi ya Glimepiride


  • Meza kama ulivyo elekezwa na daktari wako.

  • Unashauriwa kutumia dawa hii mara baada ya kupata kifuangua kinywa au mlo wako wa kwanza wa siku.


Ufanyaji kazi wa Glimepiride


  • Inachochea seli beta za kongosho kuzalisha insulini ambayo ndiyo hushusha sukari ya damu.

  • Inapunguza kasi ya ini kutengeneza sukari

  • Inaongeza uwezo wa ufanisi wa vipokezi vya insulini kwenye seli za mwili hivyo insulini kufanya kazi vizuri.

  • Hufika kwenye damu baada ya kufyonzwa kutoka kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.

  • Hufika kilele cha uwezo wa kufanya kazi kati ya saa 2-baada ya kumezwa.

  • Huweza kufanya kazi mwilini kwa saa 24 baada ya kumezwa

  • Huanza kufanya kazi saa 1 baada ya kumezwa.

  • Huchakatwa na mwili kwenye ini ili iweze kufanya kazi na kuondoa sumu.

  • Takamwili za mabaki yake hutolewa kwa njia ya mkojo (asilimia 60) na kwenye kinyesi (asilimia 40).


Glimepiride marufuku kwa wagonjwa wafuatao


  • Wagonjwa wenye mzio na kemikali ya salfa

  • Wagonjwa wa sukari inayotibika kwa insulini pekee (sukari aina ya kwanza)


Matumizi ya Glimepiride wakati wa ujauzito


Kama ikitumiwa wakati wa ujauzito, wakati wa kuzaliwa mtoto kuna hatari ya mtoto kuzaliwa na sukari ya chini kupita kiasi, kushindwa kupumua na mama kuchelewa kujifungua. Kama ililazimu mama kutumia dawa hii basi mama anapaswa kuacha kuitumua wiki 2 kabla ya siku ya matarajio ya kujifungua.

Matumizi ya Glimepiride wakati wa kunyonyesha


Pia ni vizuri kuacha kutumia wakati wa kunyonyesha, na ikibidi kutumia basi mtoto anaenyonya atawekwa kwenye uangalizi wa karibu kwa kuangalilia dalili kama vile kuwa wa blue mdomoni viganja na miguu, kulala kupita kiasi, kushindwa au kunyonya kwa udhahifu na degedege.


Maudhi ya Glimepiride


  • Kizunguzungu

  • Maumivu ya kichwa

  • Kichefuchefu

  • Kuwashwa ngozi

  • Kuharisha

  • Maumivu ya tumbo


Madhara makubwa ya Glimepiride


  • Sukari kushuka kupita kiasi

  • Kupoteza fahamu

  • Upungufu wa damu

  • Aleji ya ngozi (ugonjwa wa Steven Johnson syndrome)

  • Ini kushindwa kufanya kazi

  • Kunyonyoka nywele

  • Degedege


Kiwango cha madhara haya makubwa ni chini ya asilimia 1 ya waliotumia glimepiride.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021, 11:33:38

Rejea za mada hii:-

1.Drugbank. https://www.drugbank.ca/drugs/DB00222 . Imechukuliwa 22/04/2020.

2.Pubchem. https://pubchem.ncbi.nlm.nih.gov/compound/Glimepiride-d5. Imechukuliwa 22/04/2020.

3.Madescape. https://reference.medscape.com/drug/amaryl-glimepiride-342707. Imechukuliwa 22/04/2020.

4.Drugs.com Glimepiride .https://www.drugs.com/pregnancy/glimepiride.html. Imechukuliwa 22/04/2020.
bottom of page