top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

28 Juni 2020 20:05:29

Guanfacine

Guanfacine

Guanfacine


Guanfacine ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu Iliyopo kwenye kundi la dawa linaloitwa Alpha 2 Adrenergic Agonisti. Dawa hii huwa maarufu kwa majina ya Intuniv na Tenex


Rangi ya dawa ni nyeupe lakini mara nyingi hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza.


Guanfacine haipaswi kutumiwa pamoja na chakula cha mafuta, hutumika mara moja kwa siku au kama utakavyoelekezwa na kushauriwa na daktari wako.


Dawa hii hupatikana katika mfumo wa kidonge katika uzito wa;


• 1 Mg

• 2 Mg


Namna dawa inavyofanya kazi ;


Dawa jamii ya Apha 2 Adrenergic Agonisti ikiwa pamoja na Guanfacine hufanya kazi zifuatazo;


• Hufanya kazi kwa kupunguza shughuli za Kisimpathetic ambazo hupelekea kupunguza mapigo ya moyo


Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja (Alpha 2 Adrenergic Agonisti ) na dawa hii ni;


• Clonidine

• Detomidine

• Exmedetomidine.

• Medetomidine

• Romifidine

• Tizanidine

• Xylazine


Kazi ya dawa :


• Hutumika kwa ajili ya kushusha shinikizo la juu la damu na kuwa sawa


Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (Alpha 2 Adrenergic Agonisti)


• Dawa hii huchochea presynaptic alpha adrenoceptors mara kumi zaidi ya dawa zingine kwenye kundi hili


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;


• Amitriptyline

• Amoxapine

• Apalutamide

• Clomipramine

• Desipramine

• Doxepin

• Imipramine

• Iivosidenib

• Lofepramine

• Lofexidine

• Maprotiline

• Mirtazapine

• Nortriptyline

• Protriptyline

• Trazodone

• Trimipramine

• Tucatinib

• Voxelotor


Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao ;

Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au dawa zingine jamii ya Alpha 2 Adrenergic Agonisti


Tahadhari ya dawa hii


• Haipaswi kusitishwa ghafla sababu huweza kupelekea hali ya woga na wasiwasi

• Huweza kupelekea Haipotension

• Huweza kupelekea kulala hivyo si vyema kuendesha chombo cha moto unapotumia dawa hii


Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Dawa hii ipo kwenye kundi B la usalama wa dawa kipindi cha ujauzito


Dawa hii inaweza kutumika kwa kwa mama mjamzito sababu tafiti za wanyama zinaonyesha hakuna hatari yeyote kwa wanyama ilipotumiwa

Kwa mama anayenyonyesha dawa hii haipatikani kwenye maziwa ya mama ,Tafiti za wanyama zinaonyesha dawa hii ilipotumiwa kwenye panya ilipatikana kwenye maziwa hivyo huenda ikaweza kupatikana na kwenye maziwa ya binadamu ,Hivyo inaweza kutumika kwa tahadhari kwa mama anayenyonyesha


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni;


• Midomo kuwa mikavu

• Maumivu ya kichwa

• Kizunguzungu

• Choo kuwa kigumu

• Kuchoka

• Maumivu ya tumbo


Mengine yanayofanyika Mwilini


Kiwango cha juu cha dawa kwenye damu hufikiwa ndani masaa 3 hadi 6 na nusu maisha ya dawa mwilini ni masaa 16 mpaka 18

Mabaki yake hutolewa kwa njia ya Mkojo kwa asilimia 80


Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje?


Endapo ukisahau dozi yako ya dawa unapaswa kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:55:27

Rejea za mada hii:-

1.DrugBank.Guanfacine.https://www.drugbank.ca/drugs/DB01018 . Imechukuliwa 28/6/2020.

2.Drugs.Guanfacine.https://www.drugs.com/mtm/guanfacine.html. Imechukuliwa 28/6/2020

3.Medscape.Guanfacine. https://reference.medscape.com/drug/intuniv-tenex-guanfacine-342384. Imechukuliwa 28/6/2020.

4.WebMd.Guanfacine.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-5481-1255/guanfacine-oral/guanfacine-extended-release-oral/details . Imechukuliwa 28/6/2020
bottom of page