Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
22 Juni 2021, 05:57:23

Levonorgestrel
Levonorgestrel ni dawa mojawapo iliyo kwenye kundi la dawa za progestin, hutumika kama dawa za uzazi wa mpango wa dharura. Dawa hii huzuia kutungishwa kwa mimba kwa kuzia ovari kutoa yai.
Majina ya kibiashara
Dawa hii hufahamika kwa majina mengine ya kibiashara kama;
Emerginor
Dawa ya Plan B,
My Way,
Aftera,
Econtra EZ,
Fallback Solo,
Opcicon One-Step,
React,
Take Action,
Preventeza n.k
Dawa ya P2
Tembe ya uzazi wa dharura P2
Fomu na rangi ya Levonorgestrel
Dawa hii hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa miligramu 0.75 na 1.5
Rangi ya dawa
Rangi ya levonorgestrel mara nyingi huwa nyeupe, hata hivyo inategemea kiwanda kilichotengeneza dawa hii
Namna Levonorgestrel inavyofanya kazi
Dawa hii ya progestin, huzuia utolewaji wa yai kwenye ovari kwa kutoa mrejesho hasi kwenye tezi ya hypothalamus kwamba isiruhusu kutolewa kwa homoni muhimu za ujauzito yaani FSH na LH.
Muda wa kufanya kazi
Mara mtu anavyokunywa dawa hii, huweza hupotea kwenye damu baada ya muda wa masaa 48.8 hadi 52 , nusu maisha yake imeonekana kwenye tafiti nyingi kuwa masaa 24.4 hadi 26.
Dawa zingine zilizo kundi moja na Levonorgestrel
Norethindrone
Progesterone
Megestrol
Medroxyprogesterone
Drospirenone
Etonogestrel
Kazi ya Levonorgestrel
Hutumika kama njia ya uzazi wa mpango ya dharura endapo umeshiriki ngono siku za hatari bila kondomu au wakati kondomu imepasuka
Hutumika kuzuia mimba kwa waliobakwa
Wakati gani wa kunywa Levonorgestrel
Dawa hii hutumika ndani ya masaa 72 baada ya kushiriki ngono ziku za hatari tu.
Tahadhari kwa watumiaji wa Levonorgestrel
Endapo una aleji(mzio) na dawa zingine kama norethindrone, mwambie daktari au mfamasia kwa kuwa Levonorgestrel inaweza kukuletea mzio pia. Pia endapo una mzio nayo toa taarifa kuepuka mdhila ya dawa.
Wagonjwa wa ini lililoferi, ujauzito, na wanaotumia dawa ambazo hazipaswi kutumika na dawa hii, hawapaswi kutumia dawa p2
Endapo Levonorgestrel inatumika na dawa zifuatazo, inapaswa kuongezwa dozi kwa kuwa dawa hizo hupunguza kiasi chake kwenye damu na kuongeza hatari ya kupata mimba.
Rifampicin
Carbamazepin
Phenorbarbital
Dawa asili ya St. john's
Tafiti zinaonyesha pia kuwa, watu wenye uzito mkubwa kupita kiasi ( obeziti), asilimia 50 ya dawa huwa inaisha kabla ya kufanya kazi hivyo inashauriwa kutumia dozi mara mbili ya mtu mwenye BMI ya kawaida kwa ufanisi
Dawa ambazo zinazopunguza ufanisi wa Levonorgestrel
Dawa zifuatazo hazipaswi kutumika pamoja na levonorgestrel kwani hupunguza ufanisi wake na kuongeza hatari ya kupata mimba.
Carbamazepine
Felbamate
Griseofulvin
Mizizi ya St. John's
Modafinil
Nelfinavir
Nevirapine
Phenytoin
Primidone
Rifabutin
Rifampin
Topiramate
Dawa ambazo hazipaswi kutumika pamoja na Levonorgetrel
Abametapir
Antithrombin alfa
Antithrombin iii
Apalutamide
Argatroban
Bemiparin
Bivalirudin
Brigatinib
Calaspargase pegol
Dalteparin
Darunavir
Elagolix
Enoxaparin
Eslicarbazepine acetate
Fondaparinux
Heparin
Idelalisib
Lesinurad
Lopinavir
Lorlatinib
Mifepristone
Nefazodone
Nelfinavir
Perampanel
Pexidartinib
Phenindione
Pretomanid
Protamine
Ritonavir
Sugammadex sodium
Tucatinib
Voxelotor
• Warfarin
Matumizi ya Levonorgestrel na pombe na chakula
Pombe inafanya uwe na kizunguzungu, matumizi ya Levonorgestrel na pombe husababisha kizunguzungu kiwe kikubwa zaidi. Hata hivyo pombe haipunguzi ufanisi wa wa Levonorgestrel.
Unaweza kunywa dawa hii pamoja au bila chakula
Maudhi ya Levonorgestrel
Kichefuchefu na kutapika
Maumivu ya tumbo
Uchovu
Kizunguzungu
Kutokwa na damu ukeni
Maumivu ya titi
Maumivu ya kichwa
Matumizi ya Levonorgestrel kabla na wakati wa ujauzito
Levonorgestrel haipaswi kutumika wakati wa ujauzito au endapo unafikiria kuwa mjamzito. Soma maelezo zaidi kuhusu Levonorgestrel kwenye mada za‘ushauri wa dawa wakati wa ujauzito na kunyonyesha’ ndani ya tovuti hii.
Matumizi ya Levonorgestrel wakati wa kunyoyesha
Dawa hii huwa inaingia kwenye maziwa ya mama lakini haina madhara kwa mtoto. Soma maelezo zaidi kuhusu Levonorgestrel kwenye mada za‘ushauri wa dawa wakati wa ujauzito na kunyonyesha’ ndani ya tovuti hii.
Endapo umesahau kunywa dozi ufanyaje?
Endapo umesahau kunywa dozi moja, kunywa pale utakapokumbuka, lakini endapo zimeshapita siku tatu. Tumia njia zingine za uzazi wa mpango.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-