top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

31 Machi 2020 16:31:44

Loperamide

Loperamide

Ni dawa iliyo kwenye kundi la dawa zinazozuia kuhara. Dawa hii inaweza kupatikana kwa majina tofauti kulingana na kiwanda kilichotengeneza lakini kiini cha dawa ni kimoja ambacho ni loperamide. Jina jingine la dawa hii ni Imodium.


Loperamide inafanya kazi kwa kupunguza mijongeo ya utumbo hivyo kupunguza kwenda choo na kufanya kinyesi kisiwe na majimaji mengi., kuzuia kupitishwa kwa kinyesi na huzuia kubana kwa misuli ya tumbo.


Fomu na Rangi ya Loperamide


Dawa hii hupatikana katika mfumo wa majimaji/uji, kidonge au tembe na tembe ya kutafuna.


Dawa hii haipaswi kutumiwa pamoja na chakula kwa muda huo huo pia haipaswi kutumika pamoja na pombe maana huongeza mauzi ya dawa hiyo.


Baadhi ya magonjwa ambayo hutibiwa na dawa ya Loperamide


• Kuhara kwa kawaida

• Kuhara kwa muda mrefu

• Kuhara kwa wasafiri

• Kolaitizi ya limfatiki

• Kwa wagonjwa waliofanyiwa iliostomi

• Kutibu ugonjwa wa inflamatori boweli

• Matibabu ya baweli koliki baada ya upasuaji

• Matibabu ya kushindwa kuzuia kinyesi kutoka


Loperamide haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:


• Lasmiditan

• Elagolix

• Istradefylline

• Methotrexate

• Furosemide

• Omeprazole

• Metformin


Dawa ya Loperamide haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao :


• Muharo uliosababishwa na Bakteria

• Mgonjwa wa figo

• Mgonjwa wa ini

• Mgonjwa mwenye upungufu wa Elekrolaiti

• Megakolonya sumu

• Anayehara damu

• Mwenye homa kali

• Konstipesheni

• Anayeumwa tumbo bila kuhara


Tahadhari ya Loperamide kwa watoto


Dawa ya Loperamide haipaswi kutumika kwa mtoto chini ya miaka 2


Dawa hii inapaswa kusimamishwa kama itaonyesha dalili zifuatazo


• Kushindwa kutuliza kuharisha kwa kawaida ndani ya masaa 48

• Kama itapelekea kukosa choo kabisa

• Kama itapelekea damu kwenye choo


Kwa mama mjamzito na mama anayenyonyesha:


• Mama mjamzito: Inaweza kutumika maana tafiti zinaonyesha kuwa haina shida kwa mtoto japo tafiti

zingine zinaonyesha ina madhara madogo sana kwa mtoto

• Mama anayenyonyesha:Haijulikani kama ina madhara Bali inapaswa kutumika kwa tahadhari


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ya Loperamide


• Kizunguzungu

• Kuchoka

• Tumbo kuuma

• Kutokuona choo (constipation);

• Kichefuchefu

• Mdomo kuwa mkavu

• Kutokwa vipele

• Tumbo kujaa Gesi


Endapo dawa hii itatumika kwa dozi kubwa tofauti na inavyoagizwa huweza kupelekea shida katika moyo pamoja na kuishiwa kwa maji (dehydration) kwa watoto chini ya umri wa miaka 6


Je endapo utasahau dozi ya Loperamide ufanyaje ?


Endapo ukisahau kunywa dozi yako, unaweza kunywa mara pale utakapokumbuka, Isipokuwa endapo muda wa dozi nyingine umeshafika unatakiwa kuruka hiyo dozi uliyosahau na kuendelea na dozi yako kama muda uliopangiwa.


Jambo muhimu la kukumbuka. Dawa hii haitibu kuhara bali huzuia kuhara. Kisababishi cha kuhara lazima kifahamike na kitibiwe wakati unatumia dawa hii.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

28 Januari 2022 19:40:01

Rejea za mada hii:-

BNF 76 september 2018- march 2019. Loperamide page 66,67

Mediscape. Loperamide https://reference.medscape.com/drug/imodium-k-pek-ii-loperamide-342041 imechukuliwa 30.03.2020

Goodman and Gilman’s The pharmacological Basis of therapeutic ISBN 978-0-07-1624428
3)Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel Ukurasa wa 473

Clinical pharmacology and Therapeutics Written by James M Ritter ISBN 978-0-340-90046-8
bottom of page