top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

10 Aprili 2020 14:52:23

Lopinavir(LPV)/Ritonavir

Lopinavir(LPV)/Ritonavir

Lopinavir(LPV)/ritonavir ni dawa mojawapo ya kudhoofisha makali ya Virusi vya UKIMWI(ART) na Hepataitizi C, dawa hii ipo kwenye kundi la dawa zinazoitwa Proteaazi inhibita.


Dawa hizi hazitumiki zenyewe bali huunganishwa pamoja na dawa zingine za kuthibiti makali ya kirusi cha UKIMWI-ART ili kufanya kazi kwa ufanisi kuzuia kuzaliana kwa virusi na kuongeza kwa kinga za mwili.


Dawa inapoingia mwilini, huenda kuzuia kimeng’enya muhimu cha kirusi kinachoitwa proteazi ili kisifanye kazi yake. Kimeng’enya hiki hufanya kazi muhimu ya kukomaza kirusi, dawa inapozuia utendai kazi wa kirusi, virusi huwa huacha kukomaa na kukosa uwezo wa kuambukiza seli zingine za ulizinzi wa mwili (CD4).


Huweza kutumika pamoja au bila chakula


Dawa zilizo kundi moja na Lopinavir(LPV)/Ritonavir


Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na Lopinavir/Ritonavir ni:


• Amprenavir

• Atazanavir

• Darunavir

• Fosamprenavir

• Indinavir

• Lopinavir

• Nelfinavir

• Ritonavir

• Saquinavir

• Tipranavir


Baadhi ya dozi zilizotengenezwa na Lopinavir/Ritonavir


Lamivudine (3TC)+Lopinavir/Ritonavir(LPV/r)


Mgonjwa anapaswa kutumia dawa hii kama ambavyo atakavyoelekezwa na Daktari


Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Lopinavir/Ritonavir


Lopinavir/Ritonavir haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:


• Alfozosin

• Cabergoline

• Amiodarone

• Cobimetinib

• Ergotamine

• Erythromycin

• Rifampin

• Pimozide

• Quinidine

• Midozalam

• Nolaxegol

• Conivaptan

• Elagolix

• Eliglustat

• Irinotecan

• Ivabradine

• Midazolam


Tahadhari ya Lopinavir/Ritonavir


• Inapaswa kukatishwa endapo utapata mzio au vipele

• Mgonjwa anayetumia dawa hii huweza kuvimba kongosho

• Mgonjwa anapaswa kupimwa ini kabla na baada ya kutumia dawa maana hupelekea sumu kwenye ini

• Huongeza kolestrol mwilini

• Huongeza kiwango cha glukozi kwenye damu


Dawa ya Lopinavir/Ritonavir haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:


• Mgonjwa mwenye mzio na dawa


Matumizi ya Lopinavir/Ritonavir Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Tafiti zinaonyesha kuwa dawa hii haina madhara kwa mama mjamzito na mtoto lakini huwa na maudhi madogo madogo


Mama mwenye Maambukizi ya HIV hapaswi kunyonyesha wakati wa miezi 6 yote japo dawa hii haina madhara kwake mtoto licha ya kuwa huwa inapita kwenye maziwa.


Maudhi ya Lopinavir/Ritonavir


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na:


• Kuharisha

• Kichwa kuuma

• Vipele

• Kichefuchefu

• Kutapika

• Kuharisha

• Tumbo kuuma

• Likamu mwilini kuongezeka

• Kuwa mdhaifu

• Kuwa na seli nyeupe chache


Je endapo umesahau dozi ya Lopinavir/Ritonavir ufanyeje?


Endapo utasahau kunywa dozi yako, unapaswa kunywa mara moja na Kuendelea muda huo siku inayofuata.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

28 Januari 2022 19:40:48

Rejea za mada hii:-

1.National Guidelines for the management of HIV&AIDS 7thEdition April 2019 ukurasa wa 72 na 207

2.AIDSINFO.LOPINAVIR.https://aidsinfo.nih.gov/guidelines/html/2/pediatric-arv/132/lopinavir-ritonavir . Imechukuliwa 09.04.2020

3.WebMd.Lopinavir.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-19938-542/lopinavir-ritonavir-oral/lopinavir-ritonavir-oral/details . Imechukuliwa 09.04.2020

4.MEDSCAPE.LOPINAVIR.https://reference.medscape.com/drug/kaletra-lopinavir-ritonavir-342629. Imechukuliwa 09.04.2020

5.Lopinavir.DrugBank.https://www.drugbank.ca/drugs/DB01601. Imechukuliwa 09.04.2020
bottom of page