top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

13 Aprili 2020 13:57:23

Meclofenamate

Meclofenamate

Ni dawa jamii ya NSAIDs inayozuia inflamesheni kwenye seli hivyo kuleta madhara chanya ya kuzuia uvimbe, kutuliza maumivu na homa.


Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia uzalishwaji wa prostaglandini kwenye tishu mwilini, prostanglandini ni kemikali inayozalishwa na mwili kuitikia uharibifu uliotokea kwenye seli. Kemikali hii inapotolewa huambatana na homa Pamoja na uvimbe sehemu yenye shida.


Fomu na Rangi ya Meclofenamate


Dawa hii hupatikana katika mfumo wa tembe yenye uzito wa 50mg na 100mg


Haina madhara ikitumika Pamoja na chakula


Dawa zilizo kundi moja na Meclofenamate


Dawa hii ipo katika kundi moja na dawa zifuatazo;


• Aspirin

• Celecoxib (celebrex)

• Diclofenac

• Diflunisal

• Etodolac

• Ibuprofen

• Indomethacin (indocin)

• Ketoprofen

• Ketorolac

• Nabumetone

• Naproxen

• Oxaprozin

• Piroxicam

• Salsalate

• Sulindac

• Tolmetin


Jinsi Meclofenamate inavyofanya kazi


Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia homoni ya prostaglandin ambayo husababisha uvimbe na maumivu


Kazi za meclofenamate;


• Hutumika kutibu maumivu ya ugonjwa reumatoid arthraitizi

• Hutumika kutibu maumivu ya ugonjwa osteoartharitizi

• Hutumika kutibu maumivu ya ugonjwa wa ankalozing spondilaitizi

• Hutumika kutibu maumivu ya bazaitizi

• Hutumika kwa mgonjwa mwenye athraitizi ya gauti

• Hutumika kutibu maumivu ya hedhi(dismenolea)

• Hutumika katika maumivu ya kiasi na wastani

• Hutumika kutibu homa


Dawa usizopaswa kutumia pamoja na meclofenamate


Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;


• Aminolevulinic acid oral

• Aminolevulinic acid topical

• Apixaban

• Baricitinib

• Benazepril

• Captopril

• Enalapril

• Fosinopril

• Ibuprofen IV

• Ketorolac

• Ketorolac intranasal

• Llisinopril

• Methotrexate

• Methyl aminolevulinate

• Moexipril

• Pemetrexed

• Perindopril

• Quinapril

• Ramipril

• Tacrolimus

• Trandolapril


Tahadhari ya meclofenamate kwa wagonjwa wafuatao;

• Huweza kupelekea hatari ya kupata magonjwa ya kiharusi na magonjwa ya moyo na kutokwa na damu

• Hatari yake huongezeka kadri inavyotumika kwa muda mrefu

• Huongeza maudhi kwenye mfumo wa umeng’enyaji wa chakula kama kutokwa damu na vidonda vya tumbo

• Huweza Kupelekea kuanza kwa shinikizo la juu la damu

• Huweza kupelekea maudhi makali kwenye Ngozi

• Haipaswi kutumika kwa mgonjwa mwenye mzio na dawa hii


Matumizi ya meclofenamate Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Inapaswa kutumika kwa tahadhari au pale inapohitajika kwa ulazima kwa mama mjamzito .


Hivyo hivyo kwa mama anayenyonyesha huweza kutumika kwa tahadhari


Maudhi ya meclofenamate


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na :


• Kuhara

• Kichefuchefu

• Kutapika

• Tumbo kujaa gesi

• Vipele

• Kichwa kuuma

• Kizunguzungu

• Kukosa hamu ya kula

• Kutokuona choo

• Mdomo kuvimba

• Vidonda vya tumbo

• Kusikia mlio kwenye sikio


Je endapo umesahau dozi ya meclofenamate ufanyeje?


Endapo utasahau kutumia hii dozi. kunywa mara utakapokumbuka, kisha endelea na masaa yale yale uliyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

28 Januari 2022 19:43:05

Rejea za mada hii:-

1.Web Md.Meclofenamate. https://www.webmd.com/drugs/2/drug-8673/meclofenamate-oral/details. Imechukuliwa 13/4/2020

2.Medscape.meclofenamate. https://reference.medscape.com/drug/meclofenamate-1000133 . Imechukuliwa 13/4/2020

3.Drug bank.meclofenamate sodium. https://www.drugbank.ca/salts/DBSALT001241. Imechukuliwa 13/4/2020

4.Medline Plus.meclofenamate. https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a682287.html. Imechukuliwa 13/4/2020
bottom of page