top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

15 Aprili 2020 05:31:42

Mefenamic acid

Mefenamic acid

Ni dawa jamii ya NSAIDs inayozuia inflamesheni kwenye seli hivyo kuleta madhara chanya ya kuzuia uvimbe, kutuliza maumivu na homa.


Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia uzalishwaji wa prostaglandini kwenye tishu mwilini, prostanglandini ni kemikali inayozalishwa na mwili kuitikia uharibifu uliotokea kwenye seli. Kemikali hii inapotolewa huambatana na homa Pamoja na uvimbe sehemu yenye shida.


Fomu ya Mefenamic Acid


Inapatikana mfumo wa kidonge milligramu 500 na 250


Umetaboli wa Dawa hufanywa kwa Ini, sumu huondolewa nje ya mwili kwa kuchunjwa na figo kwenye mkojo

Dawa hii ni nzuri ikitumiwa pamoja na chakula au dawa za antiasidi


Dawa ya Mefenamic acid hutibu


• Maumivu wakati wa hedhi

• Homa

• Kutibu ugonjwa wa arthraitizi

Maudhi ya Mefenamic acid

• Maumivu ya tumbo

• Kichefuchefu na kutapika

• Kupata kiungulia

• Kuharisha

• Kuvimbiwa

• Kizunguzungu

• Maumivu ya kichwa

• Kupumua kwa shida

• Upele

• Kuvimba kwa Uso, mikono, miguu

• Ugonjwa wa usingizi na hali ya kukasirika


Tahadhari ya Mefenamic acid kwa wagonjwa wafuatao;


• Wenye shida ya Ini

• Wenye matatizo ya Moyo

• Wenye shida ya Figo

• Wenye Aleji au mzio wa Mefenamic acid

• Wenye vidonda vya tumbo.

• Wenye pumu (asthma)

• Mama anayetarajia kupata mimba( huweza kuzuia kutungishwa kwa mimba)


Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Mefenamic acid


• Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa zingine jamii ya NSAIDS mfano aspirin, ibuprofen, naproxen hii hupelekea hatari ya kupata vidonda vya tumbo

• Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa zinazozuia damu kuganda mfano warfarin

• Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa za kuzuia gesi tumboni (antasidi)

• Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa digoxin

• Quinapril

• Ramipril

• Siponimod

• Tacrolimus

• Trandolapril

• Aminolevulinic ya kunywa

• Aminolevulinic ya kupaka

• Apixaban

• Baricitinib

• Benazepril

• Captopril

• Enalapril

• Erdafitinib

• Fosinopril

• Ketorolac

• Lisinopril

• Methotrexate

• Methyl aminolevulinate

• Moexipril

• Pemetrexed

• Perindopril


Matumizi ya Mefenamic acid Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha


Kwa Wajawazito


Tahadhari wakati wa ujauzito. Dawa hii hupelekea kufunga kwa haraka mishipa wa daktasi arteriosasi, mshipa huu husaidia kupelekea virutubishi na oksijeni kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Dawa hii haipaswi kutumika miezi mitatu ya mwisho katika ujauzito wa mama.


Kwa Wanaonyonyesha


Dawa hii isitumike kwa mama anaenyonyesha.


Je endapo umesahau dozi ya Mefenamic acid ufanyeje?


Kama umesaau kunywa dose yako Unaweza kunywa Mara tu unapokumbuka Isipokua endapo muda wa dozi nyingine umefika Unatakiwa kuruka hiyo dozi uliyosahau na kuendelea na dozi yako kwa muda uliopangiwa. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

28 Januari 2022 19:43:43

Rejea za mada hii:-

1.Mefenamic acid Uses, side effects and Warnings at https://www.drugs.com/mtm/mefenamic-acid.html. Imechukuliwa 14.4.2020

2.Mefenamic acid dosing, indications, interactions at https://reference.medscape.com/drug/mefenamic-acid-343294. Imechukuliwa 14.4.2020

3.Mefenamic acid Uses, side effects, Interactions at https://www.webmd.com/drugs/2/drug-11586/mefenamic-acid-oral/details. Imechukuliwa 14.4.2020

4.Mefenamic acid side effects ,Uses, dosage at https://www.healthline.com/health/mefenamic-acid-oral-capsule. Imechukuliwa 14.4.2020

5.MHRA. Medicines and Health Regulatory Agency "MHRA Drug Safety Update. Available from: URL: http://www.mhra.gov.uk/Safetyinformation/DrugSafetyUpdate."

6."Product Information. Ponstel (mefenamic acid)." Pfizer U.S. Pharmaceuticals Group, New York, NY.

7.D A Stinson.EFFECT OF EARLY CLOSURE OF DUCTUS ARTERIOSUS (DA) ON RESPIRATORY DISTRESS (RD) IN LAMBS.Pediatric research. https://www.nature.com/articles/pr19841622. Imechukuliwa 14.4.2020
bottom of page