Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
12 Aprili 2020, 12:44:18
Methotrexate
Ni dawa ambayo ilikuwa inafahamia kwa jina la amethopterin na huuzwa katika jina la Trexal, hufanya kazi kama dawa ya kushusha kinga za mwili na kuondoa uvimbe wa saratani.
Kinga za mwili vinapofanya mwitikio kwenye maambukizi au majeraha husababisha mwonekano wa uvimbe. Hivyo kwa kushusha kinga za mwili, uvimbe, maumivu na mwitikio dhidi ya maradhi hupungua.
Majina mengine ya Methotrexate ni;
Methotrexate hufahamika kwa majina mengine kama;
• Trexall
• Otrexup
• Rasuve
• Xatmep
• Reditrex
Fomu na uzito wa Methotrexate
Dawa hii hupatikana katika fomu ya unga, maji na vidonge endapo mtu atakuwa na mzio na kidonge atapewa dawa ya kuchoma( unga)
Kidonge huwa na uzito wa;
• 2.5mg
• 5mg
• 7.5mg
• 10mg
• 15mg
Unga huwa na uzito wa gramu 1 kwa kichupa komoja
Maji huwa na uzito wa miligramu 25 kwa kila mililita moja ya maji
Rangi yake hutegemea aina ya kiwanda kilichotengeneza na dawa haina madhara yeyote yale ikitumika Pamoja na chakula
Jinsi Methotrexate inavyofanya kazi
Methotrexate huzuia ufanyajikazi wa kimeng’enya daihaidrofoleti redaktezi hydrfolate, kimengenya hiki hufanya kazi muhimu katika utengenezaji wa DNA ya seli na uzalishwaji wa seli.
Madhara ya dawa ambayo hutumika kama tiba ni kuzuia kuzwalishwa kwa DNA, kuzuia kujiponya kwa DNA na kuzuia kuzalishwa kwa seli.
Dawa hii hutumika mara moja kwa wiki siku ile ile.
• Kidonge chake kina gram 2.5 hadi 10
Methotrexate hutibu nini?
Dawa hii hutolewa kwa wagonjwa wa arthritis na magonjwa yanayoendana na hii hali
• Hutumika kutibu aina mbalimbali za saratani ,mfano saratani ya damu, saratani ya matiti, shingo na saratani ndani ya ubongo.
• Hutumika kutibu Saratani ya meninjo
• Hutumika kutibu osteosarcoma- ni aina ya saratani ambayo hushambulia seli zinazounda mifupa
• Hutumika kutibu wagonjwa wa Ryeumatoid arthraitizi ambao ni ugonjwa unaoshambulia jointi na mtu hupata maumivu makali ya jointi.
• Hutumika kutibu arthraitizi
• Hutumika kutibu vazikulitizi
• Hutumika kwa wagonjwa wa psoriatiki arthraitizi ,Ni aina ya arthraitizi inayoathiri watu wenye ugonjwa wa Ngozi wa soriasisi
• Hutumika kwa wagonjwa wa juvenaili arthraitizi isiyojulikana- hii ni aina ya arthraitisi ambayo hupelekea kuvimba kwa jointi zaidi ya moja hasa hasa huathiri wadada katika umri wa shuleni
• Hutumika kutibu plagi ya soriasisi
• Hutumika kutibu ugonjwa wa yuveitizi- ni uvimbe kwenye yuvea ya macho
• Hutumika kutoa mimba iliyotungwa nje ya mfuko wa kizazi endapo haijapasuka bado(mfano kwenye mirija, kwenye shingo ya kziazi n.k)
Tahadhari ya Methotrexate kwa wagonjwa wafuatao;
• Hutumika tu kwa jinsi ulivyoelezewa na daktari mbobezi katika kutoa dawa hii
• Inapaswa kutumika kwa uangalifu kwa wazee huku upimwaji wa kazi za ini ukizingatiwa
• Hutumika pamoja na foliki asidi miligramu 1 kwa siku ili kupunguza athari kwenye figo
• Huweza kuwa sumu katika mfumo wa umeng’enyaji wa chakula na kupelekea kuhara
• Huweza kuongeza hatari ya kupata Maambukizi zaidi sababu hupunguza kinga za mwili
Mwingiliano wa Dapsone na chakula
Dawa hii huweza kutumika kukiwa na chakula ama bila chakula.
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Methotrexate
• Wagonjwa wenye mzio na Methotrexate
• Wagonjwa wenye ujauzito
Utoaji taka wa Methotrexate mwilini
Kiwango kikubwa cha dawa hii hutolewa kwa njia ya mkojo na kiwango kidogo kwa njia ya haja kubwa.
Dawa zenye muingiliano na Methotrexate
Dawa zenye mwingiliano mkali na hivyo kutofaa kutumika pamoja na Methotrexate;
• Aspirin
• Chanjo hai ya BCG
• Diclofenac
• Ibuprofen
• Mefenamic acid
• Meloxicam
• Piroxicam
• Sulfamethoxazole
• Sulfasalazine
• Sulfisoxazole
• Sulindac
• Tepotinib
Dawa zinazoweza kutumika na Methotrexate chini ya uangalizi;
• Allopurinol
• Amoxicillin
• Ampicillin
• Chanjo ya Hepatitis B
• Chanjo ya Influenza a (H5N1)
• Ciprofloxacilin
• Dapsone
• Dicloxacillin
• Digoxin
• Doxycycline
• Hepatitis a vaccine inactivated
• Ibuprofen iv
• Lansoprazole
• Omeprazole
• Phenytoin
• Procarbazine
• Safinamide
• Tetanus toxoid adsorbed or fluid
• Tetracycline
• Zidovudine
Dawa zenye mwingiliano mdogo na Methotrexate;
• Adalimumab
• Colestipol
• Folic acid
• Golimumab
• Hydrochlorothiazide
• L-methylfolate
• Maitake
• Methyclothiazide
• Rituximab-hyaluronidase
• Voclosporin
Matumizi ya Methotrexate kwa mama mjamzito
Tafiti zinaonesha kuwa dawa hii inaweza kuleta madhara kwa mtoto hivyo haishauriwi kutumia dawa hii wakati wa ujauzito.
Matumizi ya Methotrexate mama anayenyonyesha
Dawa hii inaingia kwenye maziwa ya mama anayenyosha hivyo inashauriwa kwa mama aache kunyonyesha wakati anatumia dawa.
Maudhi ya methotrexate
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na :
• Ngozi kuwa nyekundu
• Kuwepo kwa uric asidi kwa wingi kwenye damu
• Asaretivu stomataitizi
• Kuvimba kwa ulimi
• Kuvimba kwa fizi
• Kichefuchefu na kutapika
• Kuharisha
• Kukosa hamu ya kula
• Kutoboka kwa tumbo
• Myukozaitizi
• Kushuka kwa kinga ya mwili
• Thrombosaitopenia- kushuka kwa chembe sahani za damu
• Kuferi kwa figo
• Azotemia
• Nephropathi
• farinjaitizi
• Alopesia
• Kuongezeka hisia ya macho kwenye mwanga
• Kupata vipele na harara
• Mwili kuchoka
• Homa
• Kushuka kwa uwezo wa kupambana na magonjwa
Je endapo umesahau dozi ya Methotrexate ufanyeje?
Kama ukisahau kutumia dozi yako, wasiliana na daktari aliyekuandikia dawa kwa maelekezo zaidi.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
28 Januari 2022, 19:45:41
Rejea za mada hii:-