Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
23 Juni 2021, 17:21:49
Misoprostol
Misoprostol dawa aina ya prostaglandin, dawa hii huwekwa kwenye makundi mbalimbali ya dawa kutokana na uwezo wake wa kutibu hali na magonjwa mbalimbali. Misoprostol hutumika kupunguza hatari ya kupata vidonda vya tumbo kutokana na matumizi ya dawa jamii ya NSAID, huzuia kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua. Kazi nyingine muhimu ya misoprostol ni kutoa mimba katika kipindi cha kwanza cha ujauzito.
Majina mengine ya misoprostol
Dawa Misoprostol hufahamika kwa majina mengine kama
Miso
Cytotec
Cytotec 200 Mcg
Dozi fomu na rangi ya misoprostol
Dawa hii hupatikana katika fomu ya kidonge cheupe chenye uzito wa maikogramu 100 na 200 kinachoweza kutumia kwa kuweka ukeni, chini ya ulimi, kumeza au kuweka njia ya haja kubwa.
Ikumbukwe pia, licha ya kuwa na rangi nyeupe, rangi pia hutegemea rangi pendekezwa na kiwanda kinachzalisha dawa.
Dawa zinazofanya kazi kama misoprostol
Dawa zingine zilizo kundi la dawa za kuongeza mijongeo ya misuli ya kizazi na kufungua njia shingo ya kizazi kama misoprostol ni;
Oxytocin
Ergometrine
Syntometrine
Prostaglandins
Carbetocin
Namna misoprostal inavyofanya kazi yake
Misoprostol husisimua milango ya prostaglandin kwenye tumbo, kusisimuliwa kwa milango hii husababisha kupungua kwa uzalishaji wa tindikali tumboni na kusisimua milango ya misuli ya kizazi na shingo ya kizazi ambayo huongeza kishindo cha mjongeo wa kuta ya uzazi na kufunguka kwa mlango wa kizazi.
Kazi za awali za misoprostol
Misoprostol hutumika katika matibabu ya;
Kupunguza hatari ya kupata vidonda vya tumbo kwa wanaotumia dawa jamii ya NSAID kama aspirin, diclofenac n.k
Hutumika kwenye matibabu ya osteoathraitiz ikiwa imeunganika pamoja na dawa jamii ya NSAID kwa wagonjwa wenye hatari kubwa ya kupata vidonda vya tumbo
Kazi zisizo za awali za misoprostol
Kazi zisizo za awali za misiprostol ni;
Kuanzisha uchungu kwa mimba iliyofia ndani ya kizazi
Kufungua shingo ya kizazi kuanzisha uchungu
Kutoa mabaki ya uchafu yaiyobaki kwenye kizazi baada ya mimba kutoka
Kuzuia kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua
Kutoa mimba katika kipindi cha kwanza cha ujauzito au ikiwa pamoja na dawa ya mifepristone
Dawa ambazo hazipaswi kutumika na misoprostol
Misoprostol haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Aluminum hydroxide/magnesium carbonate
Aluminum hydroxide/magnesium trisilicate
Citric acid/glucono-delta-lactone/magnesium carbonate
Magnesium gluconate
Oxytocin
Wagonjwa wasiopaswa kutumia misoprostol
Misoprostol haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye mzio na dawa hii
Wagonjwa wenye hatari ya kupata vidonda vya tumbo lakini wana ujauzito
Tahadhali ya matumizi ya misoprostol
Isitumike kwa wagonjwa wenye ujauzito ambao wanapenda uendelee
Isitumike kwa wanawake walio kwenye umri wa kubeba mimba isipokuwa hawana mimba
Ina hatari ya kuchana kizazi endapo itatumika kwa mjamzito
Matumizi ya misoprostol na chakula
Dawa hii inaweza kutumika pamoja na chakula, na endapo itatumika pamoja na chakula hupunguza kupata hali ya kuharisha.
Matumizi ya misoprostol wakati wa ujauzito
Haipaswi kutumika wakati wa ujauzito, inaongeza hatari ya mimba kutoka na madhaifu ya kuzaliwa kwa mtoto.
Matumizi ya misoprostol wakati wa kunyonyesha
Soma zaidi kuhusu matumizi wakati wa kunyonyesha kwenye Makala ya ‘dawa salama kipindi cha ujauzito na kunyonyesha’
Maudhi ya misoprostol
Maudhi yanayotokesa sana
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Maumivu ya kichwa
Maudhi yanayotokea kwa kiasi
Anafailaksia
Upunfugu wa damu
Disrithimia ya moyo
Maumivu ya kifua
Kujamba
Kuvia kwa damu tumboni
Kupoteza usikifu
Kuchanika kwa kizazi
Kichefuchefu
Madhaifu ya damu kuganda
Endapo umeshau dozi ya misoprostol ufanyaje?
Endapo umesahau kutumia dozi yako ya misoprostol, kunywa mara utakapokumbuka, na endapo muda wa dozi nyingineumekaribia sana, acha dozi uliyosahau kisha endelea na dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023, 16:54:56
Rejea za mada hii:-