top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

13 Aprili 2020 14:40:28

Natalizumab

Natalizumab

Ni dawa iliyo kwenye kundi la dawa la monoklono antibodi, hufanya kazi kwa kuzuia chembe za damu za lyukosaiti kuingia kwenye mfumo wa fahamu wa kati na hivyo kupunguza inflamesheni na kuondolewa kwa mayelini za mishipa ya fahamu.


Natalizumab hupatikana kwenye mfumo wa maji na hutolewa kwa njia ya sindano inayochomwa kweney misuri.


Matumizi nachakula


Haina madhara yeyote inapotumika na chakula au pasipo na chakula.


Dozi ya dawa


Dozi yake hutumika kila baada ya siku 28


Uwezo wa dawa kupenya kwenye tishu


Dawa huwa na uwezo wa kuingia kwenye mfumo wa fahamu wa kati.


Kazi za Natalizumab


Hutumika kutibu ugonjwa wa Matipo sklerosisi

Hutumika kutibu ugonjwa wa Crohn’s


Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Natalizumab


 • Baricitinib

 • Beclomethasone, ya kunusa

 • Certolizumab pegol

 • Ifosfamide

 • Chanjo ya kirusi cha influenza

 • Lomustine

 • Mechlorethamine

 • Melphalan

 • Ocrelizumab

 • Procarbazine

 • Vedolizumab


Tahadhari ya Natalizumab


 • Huongeza hatari ya kupata ugonjwa endelevu wa Matifoko lyukoensephalopathi (PML)

 • Usitumie pamoja na dawa zingine za kushusha kinga ya mwili

 • Huweza kupelekea mzio

 • Huweza kupelekea kuvimba kwa ubongo

 • Huweza kupelekea kujeruhiwa kwa ini


Haipaswi kutumika kwa mtu mwenye mzio na dawa hii au mwenye historia ya kupata ugonjwa endelevu wa Matifoko lyukoensephalopathi (PML)


Matumizi ya Natalizumab kwa mama mjamzito


Hutumika kwa mama mjamzito pale tu faida zinapokuwa muhimu kuliko hasara.


Matumizi ya Natalizumab kwa anayenyonyesha


Kwa mama anayenyonyesha hapaswi kutumia sababu huweza kuleta athari kwa mtoto.


Maudhi ya Natalizumab


 • Kuchoka

 • Kuhara

 • Kukojoa mara kwa mara

 • Sinusaitiz

 • Maambukizi kwenye uke

 • Maumivu kwenye jointi

 • Kukohoa

 • Maambukizi ya virusi

 • Kuvimba ngozi

 • Maumivu ya koo

 • Kuvimba miguu

 • Kutokwa vipele

 • Maumivu kwenye hedhi

 • Masikio kupiga kelele

 • Kubeua gesi

 • Kuharibika kwa kazi za figo

 • Mzunguko wa hedhi kutokuwa katika mpangilio

 • Kujikojolea

 • Maumivu ya jino

 • Muwasho

 • Maumivu ya tumbo chini ya kitovu

 • Kutokuona choo au choo kigumu

 • Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo

 • Tumbo kujaa gesi

 • Kutokuona hedhi


Je endapo umesahau dozi ya Natalizumab ufanyeje?


Endapo mgonjwa atasahau dozi anapaswa kuwasiliana na daktari aliyemuandikia dawa hii kwa maelekezo zaidi.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

28 Januari 2022 19:15:23

Rejea za mada hii:-

1.BNF September 2018 march 2019. Ukurasa wa 837-837. bnf.org

2.Medscape. Drug Interaction of Natalizumab. https://reference.medscape.com/drug/tysabri-natalizumab-343085. Imechukuliwa 11/4/2020

3.Web Md. Natalizumab. https://www.webmd.com/drugs/2/drug-92174/natalizumab-intravenous/details. Imechukuliwa 11/4/2020

4.Drug bank. Natalizumab. https://www.drugbank.ca/drugs/DB00108. Imechukuliwa 11/4/2020

5.Med line plus. Natalizumab. https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a605006.html. Imechukuliwa 11/4/2020
bottom of page