Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
13 Aprili 2020, 15:25:46
Oxaprozin
Ni dawa jamii ya NSAIDs inayotumika kutuliza au kuzuia uvimbe kutokana na michomo kinga, kutuliza maumivu na homa.
Fomu na uzito wa Oxaprozen
Dawa ya Oxaprozen hupatikana katika fomu ya tembe
Oxaprozen na chakula
Oxaprozen haina shida ikitumika Pamoja au bila chakula
Dawa zilizo kundi moja na Oxaprozen
Aspirin
Celecoxib (celebrex)
Diclofenac
Diflunisal
Etodolac
Ibuprofen
Indomethacin (indocin)
Ketoprofen
Ketorolac
Nabumetone
Naproxen
Piroxicam
Salsalate
Sulindac
Tolmetin
Oxaprozen hutibu nini?
Hutumika kutibu maumivu ya ugonjwa wa Reumatoid arthraitizi
Hutumika kutibu maumivu ya ugonjwa wa osteoarthraitizi
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Oxaprozen
Aminolevulinic ya kunywa
Apixaban
Baricitinib
Benazepril
Captopril
Enalapril
Fosinopril
Ibuprofen
Ketorolac
Lisinopril
Methotrexate
Methyl aminolevulinate
Moexipril
Pemetrexed
Perindopril
Quinapril
Ramipril
Tacrolimus
Trandolapril
Angalizo la Oxaprozen
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mgonjwa wa pumu
Huweza kupelekea hatari ya magonjwa ya kiharusi na magonjwa ya moyo
Hatari yake huongezeka kadri inavyotumika kwa muda mrefu
Huongeza maudhi kwenye mfumo wa umeng’enyaji wa chakula kama kutokwa damu na vidonda vya tumbo
Huweza kupelekea kuanza kwa shinikizo la juula damu
Huweza kupelekea maudhi makali kwenye Ngozi
Haipaswi kutumika kwa mgonjwa mwenye mzio na dawa hii na wagonjwa wenye vidonda vya tumbo,
Oxaprozen kwa mjamzito
Inapaswa kutumika kwa tahadhari hasa kwenye miezi mitatu ya mwisho wakati wa ujauzito sababu huweza kupelekea shida kwa mtoto (Kucehelewa kufunga kwa mshipa wa daktas arteriosus)
Oxaprozen wakati wa kunyonyesha
Hakuna madhara yeyote kwa mtoto.
Maudhi madogo ya Oxaprozen
Maudhi madogo ya Oxaprozen ni;
Vipele
Tumbo kuuma
Kukosa hamu ya kula
Kukosa choo
Kuhara
Chakuka kutokumeng'enywa
Kichefuchefu
Kutapika
Vidonda kwenye mfumo wa umeng’enyaji
Kiungulia
Kupungukiwa damu
Kusikia mlio kwenye sikio
Kukojoa mara kwa mara
Je endapo dozi yako ya Oxaprozen ufanyaje ?
Endapo mgonjwa atasahau dozi yake, anapaswa kuitumia pale atakapokumbuka."
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:28:04
Rejea za mada hii:-