Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
4 Mei 2020 08:23:42
Oxprenolol
Oxprenolol dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo kwenye kundi la beta bloka.
Majina ya kibiashara ya Oxprenolol
Dawa hii huwa maarufu pia kwa jina la Trasicor
Fomu na uzito wa oxprenolol
Oxprenolol hupatikana kwenye fomu ya kidonge chenye uzito wa;
20mg
40mg na
80mg
Namna oxprenolol inavyofanya kazi
Dawa jamii ya beta bloka ikiwa pamoja na Oxprenolol hufanya kazi zifuatvyo ili kupunguza shinikizo la damu.
Oxprenolol hufanya kazi kwa kufunga milango ya seli yenye jina la beta-adrenorisepta na hivyo kuzuia ufanyaji kazi wa homoni ya epinephrine na norepinephrine kwenye risepta hizo. Kuzuiwa kufanya kazi kwa homoni hizi husababisha kupungua kwa matendo ya ki simpathetiki katika moyo na mishipa ya damu. Matendo ya kisimpathetiki hujumuisha ongezeko la ufanyaji kazi wa misuli ya moyo na shinikizo la damu. Matokeo ya ufanyaji kazi wa dawa hii ni kupunguza uwezo wa moyo kusukuma damu na hivyo kupunguza shinikizo la damu.
Hata hivyo dawa jamii ya beta bloka haziwezi kutumika kushusha shinikizo la damu kwa haraka, dawa hii inapaswa kutumika Pamoja na dawa zingine mfano diuretics ili kupunguza shinikizo la damu kwa haraka.
Dawa zilizo kundi moja na Oxprenolol
Oxprenolol ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;
Acebutolol (Sectral)
Betaxolol (Kerlone)
Bisoprolol (Zebeta, Ziac)
Carteolol (Cartrol)
Carvedilol (Coreg)
Labetalol (Normodyne, Trandate)
Metoprolol (Lopressor)
Nadolol (Cornard)
Pindolol (Visken)
Propanolol (Inderal)
Sotalol (Betapace)
Timolol (Blocadren)
Oxprenolol hutibu nini?
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu
Hutumika kwenye matibabu ya anjaina
Hutumika kwa wagonjwa wenye shida ya Moyo
Dawa zisizopaswakutumika na Oxprenolol
Oxprenolol haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Acebutolol
Betaxolol
Bisoprolol
Carvedilol
Celiprolol
Clonidine
Digoxin
Diltiazem
Esmolol
Labetalol
Lofexidine
Metoprolol
Nadolol
Penbutolol
Pindolol
Propranolol
Rivastigmine
Saquinavir
Sotalol
Timolol
Verapamil
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Oxprenolol
Oxprenolol haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au dawa jamii ya ya Beta bloka
Wagonjwa wenye historia ya kuwa na asthma
Wagonjwa wenye moyo ulioferi
Wagonjwa wenye kiwango kikubwa cha asidi kwenye damu
Wagonjwa wenye saratani ya tezi ya adreno
Angalizo la Oxprenolol
Oxprenolol itumike kwa tahadhali kwa;
Wagonjwa wenye kisukari
Wagonjwa wenye shida ya Moyo kuferi
Wagonjwa wenye umri mkubwa
Wagonjwa wenye haipathairodisim
Wagonjwa wenye shida ya figo
Wagonjwa wenye shida ya Ini
Oxprenolol na ujauzito
Dawa hii itumike wakati wa tahadhari ambapo hamna dawa nyingine ya mbadala ya kummpa mama mjamzito.
Oxprenolol kwa anayenyonyesha
Dawa hii haijulikani kama inawezekana kuwepo kwenye maziwa au hapana.Hivyo inashauriwa isitumike kwa wamama wanaonyonyesha
Maudhi ya Oxprenolol
Baadhi ya maudhi madogo ya Oxprenolol ni;
Kizunguzungu
Uchovu
kizunguzungu
Maumivu ya kichwa
Msongo wa mawazo
Moyo kuferi
Shinikizo la chini la damu
Mikononi na miguu kuwa baridi
Kupatashida ya kupumua
Je, kama umesahau dozi ya Oxprenolol ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi yako ya Oxprenolol, tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi nyingine umekaribia sana, subiria ufike kisha endelea na dozi uliyosahau kama ulivyoelekezwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:55
Rejea za mada hii:-