top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

2 Aprili 2020 09:16:28

Paracetamol

Paracetamol

Parasetamo kwa jina lingine hujulikana kama acetaminofeni ni dawa inayotumika kutuliza homa pamoja na maumivu.


Majina ya kibiashara


Parasetamu hufahamika kwa majina mengine kama;


 • Panadol

 • Acetaminophen

 • Acephen

 • Acetadryl

 • Allzital

 • Apadaz

 • Bupap

 • Butapap

 • Cetafen

 • Contac Cold

 • Flu Non Drowsy

 • Coricidin Hbp Cold & Flu

 • Darvocet-N

 • Dayquil Sinex

 • Dolofin

 • Dologen

 • Dologesic

 • Duralgina

 • Dvorah

 • Endocet

 • Esgic

 • Exaprin

 • Excedrin

 • Excedrin PM Triple Action

 • Excedrin Tension Headache

 • Feverall

 • Fioricet

 • Fioricet With Codeine

 • Goody's Back & Body Pain Relief

 • Goody's Body Pain

 • Goody's Extra Strength

 • Goody's Headache Relief Shot

 • Goody's PM

 • Hycet

 • Legatrin PM

 • Little Fevers

 • Lorcet

 • Lortab

 • Mapap

 • Mapap Sinus Congestion and Pain

 • Mersyndol

 • Midol Complete

 • Midol Cramps & Bodyaches

 • Nalocet

 • Norco

 • Ofirmev

 • Orbivan

 • Pamprin Max Formula

 • Pamprin Multi-symptom

 • Panadol

 • Pediacare Children's Fever Reducer Pain Reliever

 • Percocet

 • Percogesic Reformulated Jan 2011

 • Pharbetol

 • Premsyn Pms

 • Prolate

 • Rivacocet

 • Robaxacet

 • Robaxacet-8

 • Roxicet

 • Spasmhalt-8

 • Sudafed PE Sinus Headache

 • Tactinal

 • Tencon

 • Trezix

 • Triatec

 • Triatec-30

 • Triatec-8

 • Tylenol

 • Tylenol PM

 • Tylenol With Codeine

 • Ultracet

 • Vanatol

 • Vanatol S

 • Vanquish

 • Vtol

 • Xodol

 • Xolox

 • Zamicet

 • Zebutal

 • Zflex

 • Zydone


Parasetamu na chakula


Inapaswa kutumika pamoja na chakula ili kuepusha maudhi kwenye mfumo wa chakula


Dawa zilizo kundi moja na parasetamu


Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja pamoja na Parasetamo ni:


 • Aspirini

 • Diclofenac

 • Ibuprofen

 • Naproxen


Namna parasetamu inavyofanya kazi


Parasetamu hufanya kazi kwa kuzuia utengenezwaji wa kemikali ya prostaglandini ambayo hhuuletea mwili maumivu,homa na kuvimba.


Parasetamo hutibu nini?


 • Hupunguza maumivu ya wastani

 • Hutuliza homa

 • Huondoa maumivu kwa wagonjwa wa arthraitisi


Dawa zenye mwingiliano na parasetamu


Paracetamol haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;


 • Pexidartinib

 • Pretomanid

 • Apalutumide

 • Avapritinid

 • Dapsone topical

 • Isoniazid

 • Lomitapide

 • Tinidazole

 • Warfarin

 • Tetracaine

 • Lemborexant


Wagonjwa wasiopaswa kutumia parasetamu


Parasetamu hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;


 • Magonjwa makali ya ini

 • Mwenye aleji na acetaminophen


Angalizo la parasetamu


Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao:


 • Magonjwa ya Ini

 • Wagonjwa wa figo iliyoferi kwa muda mrefu

 • Mgonjwa anayetumia waliokubuhu matumizi ya pombe

 • Wagonjwa wenye utapiamlo


Parasetamu na ujauzito


Dawa huingia kwa mtoto akiwa tumboni, dawa ikitumiwa kwa kiasi kikubwa na mama huweza kuambatana na shida kwa mtoto aliye tumboni.


Parasetamu wakati wa kunyonyesha


Dawa hii huingia kwenye maziwa pia,hakuna madhara yeyote yanayoletwa na dawa hii kwa mtoto endapo atanyonya maziwa ya mama.


Maudhi ya parasetamu


Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ya parasetamu ni pamoja na;


 • Kizunguzungu

 • Vipele na harara

 • Sumu kwenye ini

 • Ini kushindwa kufanya kazi

 • Upungufu wa Sodiamu

 • Sindromu ya Steven Johnson

 • Kupungua kwa chembechembe nyeupe za damu

 • Kichefuchefu

 • Kukosa hamu ya kula

 • Kuwashwa


Je endapo utasahau dozi yako ya parasetamu ufanyaje?


Kama umesahau kutumia dozi ya parasetamu, tumia mara pale utakapokumbuka kisha endelea kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:25:47

Rejea za mada hii:-

1.Goodman and Gilman’s The pharmacological Basis of therapeutic ISBN 978-0-07-1624428 ukurasa wa 960

2.Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel Ukurasa wa 314

3.Clinical pharmacology and Therapeutics Written by James M Ritter ISBN 978-0-340-90046-8 ukurasa wa 156

4.Tylenol(Acetaminophen)Dosage, Indications https://reference.medscape.com/drug/tylenol-acetaminophen-343346 1/4/2020

5.Acetaminophen, Use and Side Effects https://www.medicinenet.com/acetaminophen/article.htm 2/4/2020
bottom of page