Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
31 Machi 2020 15:40:00
Penicillin G
Ni antibayotiki jamii ya Penicillin iliyotengenezwa kutoka kwa fangasi wanaofahamika kama Penisillium.
Majina ya kibiashara
Penicillin G kwa jina jingine hufahamika kam Benzylpenicillin
Uwezo wa Penicillin G
Penicillin G huwa na uwanja mdogo wa kutibu magonjwa yanayosababishwa na bakiteria wanaodhuriwa na dawa.
Bakteria wanaodhurika sana na Penicillin G
Dawa ya Penicillin G ni nzuri kwa bakteria wafuatao;
Streptococcus pneumoniae
Streptococci kundi A, B, C na G
Bakiteria wasio jamii ya enterococcal
Streptococci kundi D
Kundi la streptococci viridans
Bakiteria staphylococcus wasiozalisha penicillinase Aminoglycosides
Bacillus anthracis
Corynebacterium diphtheria
Erysipelothrix rhusiopathiae
Bakteria wengine wanaodhuriwa na Penicillin G
Bakteria wanaodhuriwa na Penicillin G ni;
Treponema Pallidum
Group A-hemolitiki streptococci
Pasteurella multocida
Fomu ya Penicillin G
Penicillin G hupatikana katika fomu ya unga na huingia mwilini kwa kuchoma sindano.
Penicillin G na chakula
Penicillin G inapaswa kutumika lisaa 1 au 2 baada ya kula au kabla ya kula
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na penicillin V ni zifuatazo;
Penicillin V
Procaine penicillin
Benzathine
Penicillin G hutibu nini?
Baadhi ya magonjwa ambayo hutibiwa na hii antibayotiki ni :
Group A Streptococci Infection: Maambukizi yote ambayo husababishwa na huyu bakteria hutibiwa na hii dawa
Kaswende : Ni ugonjwa wa zinaa ambayo huenezwa kwa ngono zembe
Kaswende kwa watoto chini ya siku 28
Maambukizi kwenye misuli ya ndani ya moyo (Infective endocarditis)
Pharyngitis : Maambukizi chini ya koo ambayo hupelekea kuwasha
Homa ya Rheumatic :Ni Maambukizi ambayo hushambulia kwa wingi jointi za mwili
Baadhi ya shida ya figo (Renal Impairment) Katika dosi ndogo hutibiwa na hii dawa
Angalizo kuhusu Penicillin G
Haipaswi kuchanganywa na dawa zingine na kutolewa pamoja;
Haipaswi kutolewa kwa mtu mwenye aleji (Hypersensitivity)
Haipaswi kuchomwa karibu na nevu au ateri
Penicillin G na ujauzito
Penicillin G haina shida endapo itatumika kwa mama mjamzito maana haina hatari yeyote kwa mtoto.
Penicillin G wakati wa kunyonyesha
Tafiti zinaonekana kuwa kuna kiwango cha penicillin G hupita na kuingia kwenye maziwa ya mama, lakini hakuna tafiti zinazoonyesha madhara kwa mtoto kutokana na kunyonya maziwa ya mama au madhara dhidi ya uzalishaji wa maziwa.
Maudhi ya Penicillin G
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa ya Penicillin G ni pamoja;
Kuharisha
Kizunguzungu
Kiungulia
Kukosa usingizi
Kichefuchefu
Kuwashwa mwili
Kutapika
Maumivu ya tumbo
Mzio
Je, kama dozi yako ya Penicillin G itasahaulika utafanyaje ?
Kama umesahau dozi yako ya Penicillin G, tumia mara pale utakapokumbuka. Kama muda wa dozi inayofuata umekaribia sana, subiria muda wa dozi hiyo kisha kunywa dozi moja tu na kuendelea kama ulivyoshauriwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:26:02
Rejea za mada hii:-