Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
30 Machi 2020, 12:06:10

Penicillin V
Ni antibayotiki asili jamii ya Penicillin inayotokana kwenye fangasi wenye jina la mold.
Majina ya kibiashara
Penicillin V hufahamika kwa jina lingine kama Phenoxymethylpenicillin.
Fomu na uzito wa Penicillin V
Dawa hii hupatikana katika mfumo wa kidonge au mfumo wa majimaji ya kunywa katika miligramu 250 na 500 au kimiminika cha mililita 125 au 250.
Penicillin V na chakula
Penicillin V inapaswa kutumika kabla ya kula chakula ili iweze kufyozwa vizuri. Ni vema ukasubiria angalau masaa 2 baada ya kula au saa moja kabla ya kula ili unywe dawa hii.
Dawa zilizo kundi moja na Penicillin V
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na penicillin V ni kama zifuatazo:
Penicillin G
Procaine penicillin
Benzathine
Bakteria wanaouliwa na Penicillin V
Baadhi ya Bakteria ambao hutibiwa na hii antibayotiki ni bakteria jamii ya :
Streptococcus pharyngitis :Maambukizi kwenye koo ambao hupelekea koo kuwa kavu
Actinomyocosis:Ni maambukizi ambayo husababisha majipu kwenye sehemu tofauti za mwili
Erysipelas :Ni maambukizi kwenye ngozi ambayo husababisha ngozi kuwa nyekundu
Magonjwa ya fizi
Hutumika kuzuia homa ya Rheumatic ambayo huathiri kwa wingi jointi za mwili
Laryngeal diphtheria :Maambukizi ya bakteria chini ya koromeo ambao muda mwingine hupelekea shingo kuvimba
Streptococcal farinjaitizi
Aktinomyaikosisi
Kinga zidi ya maambukizi ya bakteria baada ya upasuaji
Matibabu ya ugonjwa wa elipsera
Magonjwa ya fizi
kinga ya Homa ya kujirudia ya ryumatiki
Mwingiliano wa Penicillin V na dawa zingine
Dawa zisizopaswa kutumika na Penicillin V
Penicillin V haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Chanjo ya BCG kwa watoto
Chanjo ya kipindupindu
Chanjo hai ya taifodi
Doxycycline
Tetracycline
Demeclocycline
Minocycline
Omadacycline
Serecycline
Mgonjwa anapaswa kuwa kwenye uangalizi endapo atatumia Penicillin V pamoja na;
Amifampridine
Choline magnesium trisalicylate
Dienogest/estradiol valerate
Ethinylestradiol
Ibuprofen iv
Levonorgestrel oral/ethinylestradiol/ferrous bisglycinate
Methyclothiazide
Neomycin po
Rose hips
Salicylates (non-asa)
Salsalate
Sodium phenylacetate
Sodium picosulfate/magnesium oxide/anhydrous citric acid
Dawa zenye maudhi madogo ya Penicillin V
Maudhi madogo yanaweza kutokea endapo itatumika pamoja na dawa hizi;
Aspirin
Aspirin/citric acid/sodium bicarbonate
Azithromycin
Chloramphenicol
Chlorothiazide
Clarithromycin
Erythromycin base
Erythromycin ethylsuccinate
Erythromycin lactobionate
Erythromycin stearate
Furosemide
Hydrochlorothiazide
Probenecid
Wagonjwa wasiopaswa kutumia Penicillin V
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao:
Wagonjwa wenye aleji (mzio) na dawa jamii ya Penicillin
Wagonjwa wenye aleji na dawa jamii ya Cephalosporins
Angalizo
Dawa hii inapaswa kutumiwa kwa ungalifu kwa makundi yafuatayo :
Matatizo ya figo
Wagonjwa wa pumu
Kwa watoto chini ya siku 28
Penicillin V na ujauzito
Penicillin V haina shida endapo itatumika kwa mama mjamzito maana haina hatari yeyote kwa mtoto.
Pen V na mama anayenyonyesha
Tafiti zinaonekana kuwa kuna kiwango cha penicillin V hupita na kuingia kwenye maziwa ya mama, lakini hakuna tafiti zinazoonyesha madhara kwa mtoto kutokana na kunyonya maziwa ya mama au madhara dhidi ya uzalishaji wa maziwa.
Maudhi ya Penicillin V
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na :
Kuharisha
Kizunguzungu
Kiungulia
Kukosa usingizi
Kichefuchefu
Kuwashwa mwili
Kutapika
Maumivu ya tumbo
Mzio
Kuishiwa damu
Neflaitizi ya intastisho
Mzio wa anafailaksisi
Kipimo chanya cha kumbu
Maambukizi ya candida mdomoni
Je kama umesahau dozi ya Penicillin V ufanyaje ?
Kama umesahau dozi yako ya Penicillin V , tumia mara pale utakapokumbuka, lakini ikiwa muda umekaribia sana, subiria muda wa dozi nyingine ufike kisha unywe dozi moja tu na kuendelea kama ulivyopangiwa na daktari wako
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:26:09
Rejea za mada hii:-