top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

26 Aprili 2020 12:41:54

Pindolol

Pindolol

Pindolol ni dawa mojawapo ya kutibu shinikizo la juu la damu iliyo katika kundi la beta bloka.


Majina ya kibiashara


Pindolol huwa na jina kingine la kibiashara kama Visken.


Uzito na fomu ya Pindolol


Pindolol hupatikana katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa miligramu,

5mg na

10mg


Dawa kundi moja na Pindolol


Pindolol ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo;

Acebutolol (Sectral)

Betaxolol (Kerlone)

Bisoprolol (Zebeta, Ziac)

Carteolol (Cartrol)

Carvedilol (Coreg)

Labetalol (Normodyne, Trandate)

Metoprolol (Lopressor)

Nebivolol (Bystolic)

Propanolol (Inderal)

Sotalol (Betapace)

Timolol (Blocadren)


Ufyonzwaji wa Pindolol


Pindolol hufyonzwa vyema kwenye mfumo wa chakula(zaidi ya asilimia 90 yadawa) kisha huingia kwenye mzunguko wa damu, kiwango cha juu kabisa kwenye damu hufikiwa ndani ya saa 1 baada ya kunywa dozi ya kidonge. Nusu ya Maisha ya dawa kwenye mwili ni masaa 3-4 kwa watu wasio na magonjwa ya figo na Ini. Na masaa 7- 15 kwa wagonjwa watu wazima wenye shinikizo la juu la damu.


Pindolol na chakula


Tumia Pindolol pamoja na vyakula vyenye protini ili kuongeza ufyonzaji wake.


Umetaboli wa Pindolol


Asilimia 35-40 tu ya kiini cha pindolol hupita kwenye ini bila kufanyiw aumetaboli kasha kuingia kwenye mzunguko wa damu ili kufanya kazi yake.


Utoaji Pindolol mwilini


Mwili hutoa dawa hii kwenye mzunguko wa damu kwa njia kuu ya mkojo kwa asilimia 35-40, kiasi kinachobaki huvunjwa na ini.


Pindolol hutibu nini?Pindolol hutumika kwenye matibabu ya kushusha shinikizo la juu la damu, inaweza kutumika kama yenyewe au pamoja na dawa jamii ya thiazide diuretics.


Namna Pindolol inavyofanya kazi


Dawa ya pindolol pamoja na kuwa kundi la dawa la Beta bloka, ufanyaji kazi wake wa kushusha shinikizo la juu la damu bado haufahamiki. Hata hivyo vitu vinavyochangia dawa hii kushusha shinikizo la damu la juu ni;


 • Kupunguza mzigo wa moyo kufanya kazi

 • Kuzuia figo kuzalisha homoni renini

 • Kupunguza mfumo toniki wa simpathetiki kwenye kituo cha vasomota kilicho ndani ya ubongo .


Dawa zenye muingiliano na Pindolol


Pindolol haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;


 • Verapamil

 • Timolol

 • Sotalol

 • Saquinavir

 • Rivastigmine

 • Propranolol

 • Penbutolol

 • Nebivolol

 • Nadolol

 • Metoprolol

 • Lofexidine

 • Labetalol

 • Esmolol

 • Diltiazem

 • Digoxin

 • Clonidine

 • Celiprolol

 • Carvedilol

 • Bisoprolol

 • Betaxolol

 • Acebutolol


Wagonjwa wasiopaswa kutumia Pindolol


Pindolol haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;


 • Wagonjwa wenye mzio na dawa hii au dawa zingine jamii ya Beta bloka

 • Wagonjwa wenye asthma

 • Wagonjwa wa moyo ulioferi wakiwa na daliliza kuishiwa pumzi na kuvimba mwili

 • Wagonjwa wenye kizuizi kwenye mfumo wa umeme wa moyo

 • Wagonjwa wenye shoku ya kikadiojeniki


Angalizo


Pindolol inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa wagonjwa wafuatao;


 • Wagonjwa wenye haipathairodizim

 • Wagonjwa wenye shida ya figo

 • Wagonjwa wenye matatizo ya ini kufanya kazi

 • Wagonjwa wenye moyo ulioferi


Pindolol kwa mjamzito


Pindolol inaweza kutumika kwa tahadhari kwa mama mjawazito.


Pindolol kwa mama anayenyonyesha


Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii inaweza kuathiri mtoto anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa hii, hata hivyo itumike kwa uangalifu.


Baadhi ya maudhi madogo ya Pindolol ni;


 • Kukosa usingizi

 • Maumivu ya misuli

 • Kizunguzungu

 • Uchovu

 • Edema

 • Maumivu ya tumbo

 • Kichefuchefu

 • Haipotensheni

 • Kuhara


Je, kama umesahau dozi ya Pindolol ufanyaje?


Kama umesahau kutumia dozi yako ya Pindolol, tumia mara pale utakapokumbuka isipokuwa kama muda umekaribia sana, subiria mpaka ufike na kasha endelea na dozi inayofuata kama ulivyoshauriwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

3 Novemba 2021 11:26:32

Rejea za mada hii:-

1.FDA. Pindolol. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2007/018285s034lbl.pdf. Imechukuliwa 24/4/2020

2.Drugs.Pindolol.https://www.drugs.com/mtm/pindolol.html. Imechukuliwa 24/4/2020

3.Medscape.Pindolol.https://reference.medscape.com/drug/visken-pindolol-342362#4. Imechukuliwa 24/4/2020

4.WebMd.Pindolol.https://www.webmd.com/drugs/2/drug-14386/pindolol-oral/details. Imechukuliwa 24/4/2020
5.MedicinePlus.Pindolol.https://medlineplus.gov/druginfo/meds/a684032.html. Imechukuliwa 24/4/2020

5.Modern pharmacology with Clinical applications written by Charles R. Craig and Robert E. Stitizel ISBN 978-0316159340 ukurasa wa 213-2014
bottom of page