Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
29 Aprili 2020 09:53:00
Prednisolone
Prednisolone ni dawa aina ya glucorticoid inayofanana na cortisol na wakati mwingine huitwa dawa jamii ya steroid. Hutumika kuzuia uvimbe unaotokana na mwitikio wa kinga ya mwili, kudhorofisha kinga ya mwili, kuzuia saratani na kupunguza kipenyo cha mishipa ya damu.
Fomu na uzito wa dawa
Dawa hii hutolewa katika mfumo wa kidonge chenye uzito wa milligramu 5 Hadi milligramu 60.
Vidonge hupatikana vyenye uzito wa miligramu 10, 15 na 30.
Dawa ya Prednisolone hutibu nini
Prednisolone hutibu:
Aina zote za uvimbe
Aleji balimbali za kwenye ngozi macho, damu, mfumo wa chakula, mfumo wa fahamu, upumuaji, figo na magonjwa halisi ya aleji
Kudhibiti shambulio la kiungo dhidi ya kinga za mwili kwa mgonjwa aliyepandikiziwa kiungo kutoka kwa mtu mwingine
Magonjwa ya udhaifu wa vichochezi (homoni)
Kutumika kama dawa ya paliesheni kwa wagonjwa wenye maumivu kutokana na saratani
Dalili za Pumu (asthma)
Maumivu ya viungo ( baridi yabisi)
Magonjwa aina fulani ya ngozi
Maelezo ya ziada kuhusu magonjwa yanayotibiwa na prednisolone
Hutibu magonjwa ya mzio/aleji
Pumu ya ngozi (atopiki demataitizi)
Mzio wa dawa
Aleji ya msimu
Homa ya seramu
Kutibu magonjwa ya ngozi
Mfano wake ni;
Bullous demataitiz hepatiformizi
Demataitizi ya mguso
Exfolietivu erithrodima
Maikosisi fungoidezi
Pemfigazi
Mzio mkali wa sindromu ya stevens Johnson
Magonjwa ya vichocheo vya mwili
mfano;
Haipakalsemia inayosababishwa na saratani
Thairoidaitizi isiyo na usaha
Ugonjwa wa kuzaliwa wa adreno haipaplesia
Kutojitosheleza kwa homoni za adrenokotiko
Kupunguza dalili za saratani
Mfano;
Kuwa na kiwango kikubwa cha madini potasiamu (Haipakalsemia) inayosababishwa na saratani
Magonjwa ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula
Ugonjwa wa crohn’s
Ugonjwa wa asaletivu kolaitizi
Magonjwa ya damu
Upungufu wa damu wa kihemolitiki wa kuzaliwa nayo
Upungufu wa dawa wa kidayamond blakfani
Upungufu wa chembe sahani za damu bila sababu kwa watu wazima
Aplasia ya chembe nyekundu za damu
Thrombosaitopenia ya upili kwa watu wazima
Saratani
Leukemia ya muda mfupi
Limfoma kali
Na magonjwa mengine....
Namna Prednisolone inavyofanya kazi
Dawa hii huwa na madhara tiba ya muda mfupi ya kupunguza kipenyo cha mishipa ya damu na kuzuia chembe za ulizi(leukosaiti) kuitikia uvamizi mwilini(unaotokana na maamukizi)
Dozi ndogo ya dawa hii huweza kuleta madhara tiba ya kuzuia inflamesheni, dozi kubwa husababishwa kuzoroteka kwa mfumo wa kinga mwilini.
Dozi kubwa huambatana na kuzidi kwa kiwango cha sodiamu na kupungua kwa kiwango cha potasimau kwenye damu.
Maudhi madogo Prednisolone
Kichefuchefu na kutapika
Kiungulia
Maumivu ya kichwa
Kukosa usingizi
Kutokwa jasho jingi
Maumivu ya mgongo
Kuvimba Uso
Mabadiliko ya kihisia
Wasiwasi na Kukosa utulivu
Masikio kupiga kelele
Kuongezeka uzito wa mwili
Kizunguzungu
Madhara ya kuacha Prednisolone ghafla
Uchovu ama kukosa nguvu
Kichefuchefu
Uzito kupungua
Maumivu ya misuli
Kizunguzungu
Maumivu ya kichwa
Angalizo la Prednisolone
Tumia dawa hii kwa umakini kwa wafuatao
Wenye mzio na dawa hii
Wenye magonjwa ya moyo
Wenye matatizo ya Figo
Wenye kisukari
Wenye shida ya Ini
Udhaifu wa mfumo wa kinga ya mwili
Mwingiliano wa Prednisolone na dawa zingine
Usitumie Prednisolone pamoja na dawa zifuatazo kwa kuwa huwa na mwingilino mkali;
Usitumie dawa hii pamoja na dawa za fangasi mfano itraconazole
Usitumie dawa hii pamoja na dawa baadhi ya antibiotiki mfano rifampicin, refabuton
Usitumie dawa hii pamoja na dawa za kutibu kifafa mfano phenytoin
Usitumie pamoja na dawa za homoni mfano estrogens
Prednisolone na ujauzito
Tahadhari wakati wa ujauzito, isitumike kwa mama mjamzito haswa katika wiki za mwanzoni mwa ujauzito. Huleta madhara katika ukuaji wa kiumbe tumboni.
Prednisolone kwa mama anayenyonyesha
Dawa hii isitumike kwa mama anaenyonyesha. Sababu dawa hii hupita katika maziwa ya mama na hivyo kuleta athari kwa mtoto anaenyonyesha.
Je, kama umesahau dozi ya Prednisolone ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi yako ya Prednisolone, tumia mara tu utapokumbuka isipokua endapo muda wa dozi nyingine umefika Unatakiwa kuruka hiyo dozi uliyosahau na kuendelea na dozi yako kwa muda uliopangiwa. Usitumie dozi mbili kwa wakati mmoja.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
5 Juni 2022 15:12:18
Rejea za mada hii:-