Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
10 Aprili 2020 14:41:20
Rilpivirine
Rilpivirine ni dawa ya kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI iliyo kundi la NNRTIs.
Namna Rilpivirine inavyofanya kazi
Dawa jamii ya NNRTIs hufanya kazi kwa kuzuia kimengenya cha kirusi kinachoitwa Reverse Transkriptezi. Kimen’enya hiki kikizuiwa kufanya kazi, huzuia kirusi cha UKIMWI kujizalia Zaidi, na hivyo kupunguza idadi ya virusi vya UKIMWI mwilini. Idadi ya virusi vya UKIMWI vinapopungua mwilini husababisha kinga ya mwili kutoharibika na kuwa imara Zaidi.
Fomu ya Rilpivirine
Dawa huuzwa katika jina la Edurant na hutumika pamoja na dawa zingine ili kuwa na nguvu Zaidi.
Dawa inapatikana katika mfumo wa kidonge
Rilpivirine na chakula
Huweza kutumika pamoja na chakula au pasipo na chakula
Dawa zilizo kundi moja na Rilpivirine
Dawa zingine ambazo zipo kwenye kundi moja na Rilpivirine ni zifuatazo :
Nevirapine(NVP)
Etravirine(ETR)
Efavirenz
Doravirine
Baadhi ya dozi zilizounganika na Rilpivirine
Dolutegravir+ Rilpivirine
Rilpivirine + Emtricitabine + Tenofovir
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na Rilpivirine
Rilpivirine haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo:
Nevirapine
Omeprazole
Lansoprazole
Pantoprazole
Dexamethasone
Efavirenz
Carbamazepine
Etravirine
Rabeprazole
Esomeprazole
Rifampin
Phenobarbital
Phenytoin
Elvitegravir+cobicistat+emtricitabine+tenofovir
Eslicarbazepine acetate
Dexlansoprazole
Fosphenytoin
Oxcarbazepine
Rifapentine
Hydroxychloroquine sulfate
Macimorelin
Ombitasvir/paritaprevir/ritonavir na dasabuvir
Rifabutin
Umeclidinium bromide/vilanterol inhaled
Vilanterol/fluticasone furoate
Tahadhari ya Rilpivirine
Rilpivirine inapaswa kutumika kwa uangalifu kwa wagonjwa wa:
Magonjwa mengine yanayoharibu kinga ya mwili kama ugonjwa wa Graves
Mzio mkali
Kwa wagonjwa wa Ini
Haipaswi kutumika kwa mtu mwenye mzio na dawa hii
Matumizi ya Rilpivirine Kwa mama mjamzito na anayenyonyesha
Tafiti zinaonyesha bado hakuna madhara yaliyojitokeza kwa mama mjamzito na mtoto
Mama mwenye Maambukizi ya HIV hapaswi kunyonyesha wakati wa miezi 6 yote
Maudhi ya Rilpivirine
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hi ni pamoja na :
Kizunguzungu
Kuwa na hali za huzuni
Vipele
Kichefuchefu
Kutapika
Mawazo ya kujiua
Ndoto zisizo za kutisha
Maumivu ya tumbo
Kuchoka
Maumivu ya kichwa
Je endapo umesahau dozi ya Rilpivirine ufanyeje?
Rilpivirine hutumika kwa mchanganyiko pamoja na dawa zingine za kuthibiti HIV endapo utasahau dozi yako kunywa unapaswa kunywa na Kuendelea na muda huo siku inayofuata
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021 11:23:36
Rejea za mada hii:-