top of page

Mwandishi:

Dkt. Sospeter M, MD

Mhariri:

Dkt. Lugonda B, MD

13 Agosti 2021 16:27:32

Secnidazole

Secnidazole

Secnidazole ni dawa ya antibayotoki kudi la nitroimidazole inayotumika kutibu maambukizi yanayosababishwa na bakteria.


Majina ya kibiashara


Secnidazole hufahamika kw ajina la kibiashara la Solosec


Fomu na dozi ya secnidazole


Dawa hii hupatikana katika fomu ya chenga au kidonge kwa ajili ya kunywa. Kila pakiti huwa na gramu 2 za chenga ya dawa au miligramu 500 za kidonge


Ufyonzwaji wa dawa


Ufyonzwaji na Utoaji wa mabaki ya secnidazole. Nusu maisha ya dawa ni masaa 17, dawa hutolewa kwa njia ya mkojo.


Mara baada ya kunywa dawa hufyonzwa na kuingia kwenye mzunguko wa damu bila kuathiriwa na chakula.


Dawa zilizo kundi moja na secnidazole


Secnidazole ni dawa jamii ya nitroimidazole, dawa zingine kwenye kundi hili ni;


 • Benznidazole

 • Metronidazole (Flagyl)

 • Tinidazole (Tindamax)


Mwingiliano wa secnidazole na dawa zingine


Secnidazole huwa na mwingiliano mdogo endapo itatumika kwa pamoja na dawa zifuatazo;


 • Ethinyl estradiol (EE)

 • Norethindrone

 • Vidonge vya uzazi wa mpango

 • Pombe


Dawa zisizopaswa kutumika pamoja na secnidazole


Hakuna dawa ambazo zimeripotiwa kuleta madhara endapo zitatumika pamoja na secnidazole, hata hivyo kama ilivyo metronidazole, dawa hii haipaswi kutumika pamoja na pombe


Namna secnidazole inavyofanya kazi


Secnidazole ni dawa ya antibayotiki kundi la 5-nitroimidazole yenye uwezo wa kuingia ndani ya bakteria na kubadilika kuwa sumu. Inapokuwa sumu huaminika kuzuia utengenezaji wa DNA ya bakteri wannaodhuliwa na dawa hii.


Bakteria wanashambuliwa na secnidazole


Dawa hii hutumika kwenye matibabu yaliyoosababishwa na bakteria wafuatao;


 • Gardnerella vaginalis

 • Bacteroides spp.

 • Prevotella spp.

 • Mobiluncus spp.

 • Megasphaera- aina ya I/II


Magonjwa yanayotibiwa na secnidazole


Secnidazole hutibu


Vaginosisi ya bakteria

Trikomoniaisi


Wakati gani usitumie dawa ya secnidazole?


Kama una mzio na dawa hii au dawa zingine jamii ya nitroimidazole


Tahadhari


Matumizi ya secnidazole huweza pelekea mtumiaji kupata fangasi kwenye mashavu ya uke kutokana na dawa hii kuua bakteria walinzi wa uke.


Matumizi ya dawa hii pasipo kuwa na ugojwa huongeza hatari ya usugu wa vimelea wa maradhi kwenye dawa


Taarifa muhimu kwa mgonjwa kuhusu secnidazole


 • Matumizi sugu ya dawa jamii ya nitroimidazole ikiwa pamoja na secnidazole yanaambatana na kusababisha saratani katika tafiti zilizofanyika kwa panya. Unashauriwa kutotumia dawa hii mara kwa mara.

 • Dawa hii haijaruhusiwa kutumika kwa watu walio na umri chini ya miaka 18


Matumizi ya secnidazole kwa mjamzito


Usalama wa dawa hii katika ujauzito bado hajawa na taarifa za kutosha, hivyo hayafahamiki. Soma maelezo zaidi kuhusu secnidazole na ujauzito kwenye mada zingine au dawa jamii ya nitroimidazole kama metronidazole kupata maelezo zaidi.


Matumizi ya secnidazole wakati kunyonyesha


Hakuna tafiti za kutosha kuhusu madhara wakati wa kunyonyesha. Itumike kwa tahadhali na endapo hakuna dawa nyingine ya mbadala.


Hutakiwi kunywa dawa hii wakati unanyonyesha, subiria angalau siku nne zipite toka umeacha kutumia dawa hii ndipo unyonyeshe.


Madhara ya secnidazole


 • Maambukizi ya fangasi kwenye uke na mashavu ya uke

 • Maumivu ya kichwa

 • Kichefuchefu

 • Kutapita

 • Kuharisha

 • Maumivu ya tumbo

 • Muwasho kwenye uke na mashavu ya uke


Maudhi ya dawa


Maudhi madogo ya secnidazole ni; • Maambukizi ya fangasi kwenye uke na mashavu ya uke

 • Maumivu ya kichwa

 • Kichefuchefu

 • Kutapita

 • Kuharisha

 • Maumivu ya tumbo

 • Muwasho kwenye uke na mashavu ya uke

 • Ladha mbaya, ya umetabli au chungu

 • Na mengine


Ufanye nini endapo umesahau dozi yako ya secnidazole?


Secnidazole hutumika mara nyingi kama dozi moja hivyo ni vigumu kusahau kutumia dozi hii. Hata hivyo kama umesahau dozi yako, kunywa mara pale utakapokumbuka na endapo muda umekaribia sana, ruka dozi uliyosahau kisha endelea na dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

23 Julai 2023 16:54:56

Rejea za mada hii:-

1. Jean-Marc Bohbot, et al. Treatment of Bacterial Vaginosis: A Multicenter, Double-Blind, Double-Dummy, Randomised Phase III Study Comparing Secnidazole and Metronidazole. https://www.hindawi.com/journals/idog/2010/705692/. Imechukuliwa 13.08.2021

2. Secnidazole. https://www.drugs.com/mtm/secnidazole.html. Imechukuliwa 13.08.2021

3. Secnidazole. https://reference.medscape.com/drug/solosec-secnidazole-1000168. Imechukuliwa 13.08.2021

4. Tagera Forte 500mg Tablet. https://www.1mg.com/drugs/tagera-forte-500mg-tablet-187476. Imechukuliwa 13.08.2021

5. Secnidazole. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/label/2017/209363s000lbl.pdf. Imechukuliwa 13.08.2021

6. Secnidazole. https://www.accessdata.fda.gov/drugsatfda_docs/nda/2017/209363Orig1s000TOC.cfm. Imechukuliwa 13.08.2021

7. Secnidazole. https://www.fda.gov/drugs/drug-approvals-and-databases/drug-trials-snapshot-solosec. Imechukuliwa 13.08.2021
bottom of page