Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
15 Aprili 2020, 07:30:35
![Sodium](https://static.wixstatic.com/media/26af9c_61fef365ecc848128f56bc338c829cf7~mv2.jpg/v1/fill/w_81,h_50,al_c,q_80,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/Image-empty-state.jpg)
Sodium
Sodium ni moja madini muhimu sana mwilini. Upungufu wa sodium huweza kusimamisha shughuli nyingi ndani ya mwili, mfano shughuli za usafirishaji wa taarifa kati ya mishipa ya fahamu, ubongo na moyo.
Madini haya huweza kuthibiti kiasi cha maji kwenye mwili na kusafirisha taarifa za mfumo wa neva, kazi hizo hufanya madini haya kuwa moja ya elementi muhimu sana kuyapata kwenye mlo wako.
Sodium hupatikana wapi?
Chumvi ya mezani ni chanzo kizuri cha madini ya sodia, chumvi ina asilimia 40 tu ya madini haya.
Kijiko kimoja cha chumvi ya chai huwa na uzito wa Mg 2300 za madini ya sodiamu ambacho ni kiasi kinachotosha kwa matumizi ya mwili kwa siku.
Kwa watu wenye shinikizo la juu la damu wanapaswa kuthibiti matumizi yao ya chumvi kwa kutumia Milligram 1500 kwa siku na kwa watoto wadogo wanapaswa kutumia kuanzia mg 1000 hadi 1500 kwa siku.
Vyanzo vingine vyenye madini ya sodium
Supu
Mboga za majani
Nyama za kusindikwa
Nyama ya kuku, ng’ombe, samaki n.k zilizochomwa kwa moshi na kuhifadhiwa kwa chumvi
Vitunguu maji
Soseji
Karanga zenye chumvi
Na vitu vingine ambavyo vimewekewa chumvu
Unaponunua bidhaa yoyote ile dukani angalia kiwango cha madini ya sodiamu kwenye sehemu iliyoandikwa ingredients. Ni vema kufanya hivi ili kudhibiti kiwango cha madini hayo unayokula kwa siku
Zipo aina zingine za madini ya sodium ambayo ni;
Monosodium glutamate
Sodium nitrate
Sodium saccharin
Sodium benzoate
Sodium bicarbonate.
Kazi za Sodium mwilini
Hutumika kudhibitiki kiasi cha maji kwenye seli za mwili
Hutumika kuweka muwiano sawa wa ions kwenye mwili kati ya ions hasi na chanya
Huzuia mwili kupoteza maji pale unapokaa kwenye jua kwa muda mrefu
Huzuia misuli kukbana- wa kutumia vyakula vyenye chumvi na juisi zenye sodiamu husaidia kurudisha elekrolaiti za sodiamu zilizopotea na kufanya misuli ifanye kazi vema.
Huondoa hewa chafu ya karbon diyoksaidi mwilini- huondoa karbon diyoksaidi inayozidi mwilini kwa njia ya uchujwaji kwenye mfumo wa mkojo
Husaidia kufanya kazi kwa ubongo- Kiasi kidogo cha sodiam hupelekea kizunguzungu,na kuchoka
Husaidia afya nzuri ya moyo kusafirisha taarifa za mfumo wa fahamu.
Huimarisha meno
Huimarisha ngozi
Kupoza kiungulia kinachotokana na asidi kutoka katika tumbo
Majina ya kitiba ya udhaifu wa sodium
Upungufu wa madini ya sodiamu kwenye damu huitwa haiponatremia na kiwango cha madini kikizidi kwenye damu huitwa haipanatremia
Maudhi ya sodiamu
Maudhi ya madini ya sodiamu yanaweza kutokana na upungufu au wingi wa madini hayo kwenye damu
Dalili za upunfugu wa Sodium kwenye damu
Kichefuchefu na kutapika
Maumivu ya kichwa
Kupoteza kumbukumbu za muda mfupi
Kuchanganyikiwa
Kupoteza hamu ya kula
Kutotulia au kuw amsumbufu
Kulegea kwa misuli
Kukaza kwa misuri
Degedege
Kupoteza fahamu
Dalili za kuzidi kwa Sodium kwenye damu
Kiu kupita kiasi
Kubadilika kwa uzito wa mkojo na rangi
Kuferi kwa moyo kutokana na kujawa na maji (konjestive), Ugonjwa wa figo na sirosisi ya Ini
Kuchanganyikiwa
Uchovu mkali wa mwili
Huweza kupelekea shinikizo la juu la damu endapo itatumika kwa wingi
Maumivu ya kichwa
Kichefuchefu na kutapika
Degedege
Kupoteza fahamu
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:24:17
Rejea za mada hii:-