Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
20 Septemba 2023 17:35:47
Tenoxicam
Dawa Tenoxicam
Ni dawa kwa ajili ya kutuliza maumivu madogo hadi ya wastani ya mwili na maungio kwa kupunguza kiwango cha homoni inayoleta madhara hayo mwilini. Dawa hipo kwenye kundi la dawa jamii NSAIDS.
Tenoxcam hufanya kazi kwa kuzuia uzalishwaji wa homoni ya prostaglandini kwenye tishu mwilini, prostanglandini ni kemikali inayozalishwa na mwili kuitikia uharibifu uliotokea kwenye seli. Kemikali hii inapotolewa huambatana na homa Pamoja na uvimbe sehemu yenye shida.
Rangi na fomu ya tenoxicam
Hupatikana mfumo wa vidonge, tembe na maji
Dawa inapoingia mwilini huvunjwa na Ini na sumu yake hutolewa Utoaji taka mwili kupitia Figo kwa njia ya mkojo na kinyesi
Tenoxcam inafanyaje kazi?
Tenoxcam hufanya kazi kwa kuzuia kimeng'enya cycooxygenase na hivyo kuzuia uzalishaji wa homoni prostaglandin katika tishu za pembeni. Prostaglandin huongeza hisia za vitambua maumivu hivyo kuzuia uzalishaji wake husaidia kupunguza maumivu ya mwili ya tishu za pembeni. Uzuiaji wake wa maumivu unaweza kutokea pia kupitia ufanyaji kazi wake kwenye tezi ya hypothalamus, na kupelekea kutanuka kwa mishipa ya damu ya pembeni, kuongezeka kwa kiwango cha damu na kupoteza kwa joto.
Umetaboli wa tenoxcam
Tenoxicam hufanyiwa umetaboli kwenye ini na kuzalisha kampaundi mbalimbali zilizolala.
Nusu maisha ya tenoxcam
Nusu maisha ya dawa ni masaa 72.
Matumizi ya tenoxicam
Tenoxicam kwenye matibabu ya dalili na hali zifuatazo:
Kutuliza maumivu ya mwili
Kutuliza homa
Kupunguza uvimbe
Kutibu maumivu ya athraitis na osteoarthraitizi
Maudhi madogo ya tenoxicam
Maumivu ya kichwa yasiyoisha
Kuzimia
Makelele sikioni
Hisia za mapigo ya moyo kwenda mbio
Mabadiliko ya kiasiki na roho
Maumivu ya tumbo
Mabadiliko ya machoni
Kupumua kwa shida
Dalili za kufeli kwa moyo kama vile kuvimba miguu, kuongezeka uzito gafla na uchovu usio wa kawaida
Wakati gani wa kuacha kutumia tenoxcam kutokana na maudhi?
Kutokwa damu kirahisi
Dalili za maambukizi kama vile koo kuwa kavu bila kuisha, homa
Kukaza kwa shingo kusikoelezeka
Dalili za tatizo kwenye figo kama mabadiliko ya kiasi cha mkojo
Maudhi makali ya tenoxcam
Dawa hii inaweza kusababisha maudhi makali, na kuleta ugonjwa wa kufisha wa ini. Kama ukihisi mabadiliko yoyote yafuatayo, acha kutumia tenoxcam na onana na daktari wako haraka.
Kichefuchefu kisichoisha
Udhaifu wa mwili
Maumivu makali ya tumbo
Mkojo kuwa mweusi
Manjano kwenye ngozi/Macho
Maudhi ya kufisha
Maudhi makali kabisa ya tenoxcam hutokea kwa nadra sana. Hata hivyo yakitokea unapaswa kupata msaada wa haraka. Miongoni mwayo ni:
Homa
Kuvimba mitoki
Harara kwenye ngozi
Kuwashwa, kuvimba( haswa usoni, ulimi au koo)
Kizunguzungu kikali
Kushindwa pumua vema
Tahadhari ya tenoxicam
Dawa hii inaweza isifae kwa baadhi ya hali na wagonjwa. Ongea na daktari wako kabla ya kutumia kama una:
Mzio kwenye aspirini
Kufanyiwa upasuaji wa mishipa ya damu ya moyo
Kutokwa na damu/Vidonda/Kutokwa na damu kwenye mfumo wa tumbo
Kabla ya kutumia dawa hii, mwambie daktari endapo una historia ya
Pumu ya kifua
Matatizo ya kutokwa damu
Matatizo ya damu
Shinikizo la juu la damu
Kisukari
Magonjwa ya moyo
Ugonjwa wa ini
Uvimbe wa polipsi puani
Uzito mkubwa kupita kiasi
Kutumia sigara
Historia ya matatizo kwenye tumbo kama kiungulia, vidonda vya tumbo
Kuvimba miguu/mikono
Dawa usizopaswa kutumia pamoja na tenoxicam
Dawa hii hairuhusiwi kutumika pamoja na:
Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa jamii ya NSAIDS mfano aspirin, ibuprofen, naproxen hii hupelekea
Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa zinazozuia damu kuganda mfano warfarin
Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa jamii ya steroids mfano Prednisone
Usitumie Dawa hii pamoja na Dawa methotrexate
Usitumie dawa hii pamoja na Dawa Lithium
Usitumie dawa hii pamoja na Dawa fluoxetine, fluvoxamine
Matumizi ya tenoxicam kwa Wajawazito na Wanaonyonyesha
Kwa Wajawazito
Tahadhari wakati wa ujauzito isitumike kwa mama mjamzito haswa miezi ya mwanzoni na miezi ya mitatu mwishoni ya ujauzito.
Kwa Wanaonyonyesha
Dawa hii isitumike kwa mama anaenyonyesha kwa sababu dawa hii hupita katika maziwa ya mama na hivyo kuleta athari kwa mtoto anaenyonyesha.
Je endapo umesahau dozi ya tenoxicam ufanyeje?
Kama umesaau kunywa dose yako unaweza kunywa Mara tu unapokumbuka, isipokua endapo muda wa dozi nyingine umefika, acha dozi uliyoruka na kunywa dozi ingine kwa muda uliopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
20 Septemba 2023 18:35:49
Rejea za mada hii:-