Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
9 Agosti 2020 17:06:08
Terbinafine
Terbinafine ni dawa mojawapo ya kutibu magonjwa ya fangasi iliyopo katika kundi la dawa linaloitwa antifangasi aina ya allylamine. Dawa hii huwa maarufu kwa jina la lamisil
Rangi ya dawa
Rangi yake huwa ni nyeupe lakini hutegemea aina ya kiwanda kinachotengeneza
Fomu na uzito wa terbinafine
Terbinafine hupatikana katika mfumo wa kidonge kwa 250 Milligram
Namna dawa inavyofanya kazi ili kutibu fangasi
Dawa ya terbinafine ni aina ya dawa ambayo hufanya kazi kwa kufungamana na steroli (ergosteroli) kwenye seli ya fangasi. Kwa kufanya hivi hutengeneza matundu kwenye ukuta wa seli ya fangasi na kuifanya kuruhusu kuingia kwa vitu vigeni ndani ya seli na hivyo hufa.
Dawa hii ipo katika kundi sawa na dawa zifuatazo:
Amorolfin
Butenafine
Naftifine
Kazi za hii dawa ni kama ifuatavyo:
Hutumika kwenye matibabu ya maradhi ya fangasi kwenye kucha
Hutumika katika maradhi ya fangasi kwenye ngozi yanayojulikana kama tinea pedis na Corporis
Dawa mwiko kutumika kwa pamoja na terbinafine
Dawa hii haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo :
Pitolisant
Tazemetostat
Ubrogepant
Metoclopramide
Wagonjwa wasiopaswa kutumia terbinafine
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au jamii ya dawa za Antifangasi
Haipaswi kutumika kwa wagonjwa wa ini
Upekee wa terbinafine na dawa zingine zilizo kundi moja
Utofauti wa pekee wa dawa hii na dawa zingine za kwenye kundi hili la (Antifangasi):
Dawa hii hutolewa mwilini kwa njia ya mkojo kwa asilimia kubwa zaidi kuliko njia zingine.
Dawa hii nusu ya maisha ya dawa hii ni masaa 36 tangu itumike mwilini
Matumizi ya terbinafine kwa mjamzito
Dawa hii inaweza kutumika kwa mama mjamzito , Tafiti za wanyama na binadamu hazijaweza kukuta madhara kwenye dawa hii
Matumizi ya terbinafine kwa mama anayenyonyesha
Hakuna takwimu zinazoonyesha kuwa dawa hii hutolewa kwenye maziwa ,Inaweza kutolewa kwa tahadhari
Maudhi ya terbinafine
Baadhi ya maudhi madogo ya dawa hii ni pamoja na
Kutokwa Vipele
Kuwashwa
Kichefuchefu
Kuharisha
Maumivu ya tumbo
Kupata shida ya ladha
Macho kutokuona Vizuri
Madhara ya terbinafine
Madhara ya dawa hufahamika pia kama maudhi makubwa ya dawa. Dawa hii inaweza kusababisha maudhi makubwa kwa takribani mtu mmoja kati ya watu 1000 waliotumia dawa hii.
Tahadhari
Kama unatumia dawa hii na unapata maudhi makali, acha kutumia na wasiliana na daktari wako mara moja.
Madhara ya terbinafine kama yafuatayo
Kupata manjano machoni na kwenye ngozi
Kukojoa mkojo uliopauka na kinyesi kilichopauka
Kupata michubuko kirahisi
Homa kali
Kuwashwa ngozi
Kuchoka kuliko kawaida
Kuota madoa rangi ya zambarau chini ya ngozi
Maumivu kwenye chemba ya moyo yanayoelekea mgongoni
Udhaifu au maumivu ya misuli
Kupungua uzito kutokana na kukosa hamu ya kula
Kukosa usingizi, kushindwa kulala na kuwa na huzuni
Kubadilika kwa ladha ya chakula
Kusahau kunywa dozi ya terbinafine
Je endapo utasahau dozi yako ufanyaje ?
Endapo ukisahau kutumia dozi yako, tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda umekaribia wa dozi nyingine acha dozi uliyosahau na endelea na dozi yako kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
23 Julai 2023 16:55:27
Rejea za mada hii:-