Mwandishi:
Dkt. Sospeter M, MD
Mhariri:
Dkt. Lugonda B, MD
3 Mei 2020, 13:38:55

Trandolapril
Trandolapril ni dawa mojawapo ya kushusha shinikizo la juu la damuiliyo kundi la angiotensini conventing enzyme inhibitor (ACEIs).
Majina ya kibiashara
Trandolapril ni maarufu kwa jina la kibiashara la Mavik
Matumizi na chakula
Trandolapril inaweza kutumika pamoja na au bila chakula kama utakavyoelekezwa na kushauriwa na daktari wako.
Hakikisha unakunywa dawa hii kama ulivyoshauriwa na daktari wako kila siku na kwa kiwango cha dozi uliyopewa. Kupunguza madhara ya maudhi ya dawa daktari atakuanzishiwa dozi ndogo na kuiongeza kadri ambavyo mwili wako utakavyoitikia. Baada ya wiki mbili au zaidi tangu ulipoanza kutumia dawa hii shinikizo la damu litashuka na kuwa kawaida.
Trandolapril hupatikana katika fomu ya kidonge chenye uzito wa;
1mg
2mg
4mg
Ufanyaji kazi wa Trandolapril
Dawa jamii ya ACEIs ikiwa pamoja na Trandolapril hufanya kazi zifuatazo ilikupunguza shinikizo la damu;
Huongeza kipenyo cha mishipa ya damu ya vena na ateri kwa kupinga utengenezaji wa homoni ya angiotensini II na uvunjwaji wa Bradykinin.
Kuogezeka kwa kipenyo cha mishipa husababisha kushuka kwa shinikizo ndani ya mishipa na hivyo kupunguza mzigo wa damu unaoingia na kutoka kwenye moyo na kupunguza moyo kufanya kazi kupita kiasi
Hupinga kazi za homoni ya angiotensini II kwenye mishipa ya fahamu ya simpathetiki
Huongeza uwezo wa figo kupoteza madini ya sodiamu na maji kwa njia ya mkojo kwa kuzuia uzalishwaji wa homoni ya aldosterone inayochochewa kuzalishwa zaidi na homoni ya angiotensin II. Homoni ya aldosterone kazi yake ni kutunza maji na madini hayo mwilini
Huzuia kuharibika kwa kuta za moyo na mishipa ya damu kutokana na shinikizo la damu ,kuferi kwa moyo na infaksheni ya mayokadia
Dawa kundi moja na Trandolapril
Dawa zingine zilizo kwenye kundi moja na dawa hii ni;
Benazepril
Enalapril
Fosinopril
Lisinopril
Lisinopril
Captopril
Moexipril
Perindopril
Quinapril
Ramipril
Trandolapril hutibu nini?
Hutumika kwenye matibabu ya wagonjwa wenye shinikizo la damu la juu
Hutumika kwenye matibabu ya moyo ulioferi
Upekee wa Trandolapril na dawa kundi hili la ACEIs
Huweza kupinga kazi ya homoni ya angiotensin II Hata baada ya masaa 72 baada ya dozi kuisha
Hupunguza hatari ya shida kwenye figo kwa wagonjwa wenye shiniko la juu la damu
Muingiliano wa Trandolapril na dawa zingine
Trandolapril haipaswi kutumika pamoja na dawa zifuatazo;
Aspirin
Azilsartan
Candesartan
Celecoxib
Choline magnesium trisalicylate
Dalteparin
Diclofenac
Diflunisal
Eprosartan
Etodolac
Fenoprofen
Flurbiprofen
Ibuprofen
Idomethacin
Irbesartan
Ketorolac
Lofexidine
Losartan
Meclofenamate
Mefenamic acid
Meloxicam
Nabumetone
Naproxen
Olmesartan
Oxaprozin
Piroxicam
Wagonjwa wasiopasw akutumia Trandolapril
Dawa hii haipaswi kutumika kwa wagonjwa wafuatao;
Wagonjwa wenye aleji na dawa hii au dawa jamii ya ACEIs
Wagonjwa wenye historia yakupata angioedema
Angalizo kwa watumiaji wa Trandolapril
Tahadhari ya Trandolapril inaaswa kuchukuliwa kwa kuwa;
Huweza kupelekea Haipotension endapo itachanganywa na Diuretic
Ikitolewa pamoja na temsirolimus huweza kupelekea angioedema
Ipo na hatari ya kupelekea haipakalemia kwa wagonjwa wenye shida ya figo
Dalili ya kikohozi huweza kutokea kwa miezi ya mwanzo ya matumizi ya dawa hii
Haipaswi kutolewa pamoja na Aliskiren kwa wagonjwa wa kisukari au kwa wagonjwa wenye Shida ya figo ambaye uwezo wa figo kuchuja mkojo ni GFR <60 mL/min/1.73 m²
Matumizi ya Trandolapril kwa anayenyonyesha
Inapaswa kutumika kwa tahadhari kwa mama anayenyonyesha kwa sababu huingia kwenye maziwa ya mama.
Maudhi madogo
Baadhi ya maudhi madogo ya Trandolapril ni;
Kukohoa
Kiasi cha uric asidi kupanda
Haipotension
Haipakalemia
Haipocalcaemia
Kiharusi
Mapigo ya moyo kushuka
Je kama umesahau dozi yako ufanyaje?
Kama umesahau kutumia dozi yako ya Trandolapril tumia mara pale utakapokumbuka, na endapo muda wa dozi nyingine umekaribia acha dozi uliyoisahau kasha endelea na dozi inayofuata kama ulivyopangiwa na daktari wako.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
3 Novemba 2021, 11:22:29
Rejea za mada hii:-