Disopyramide
Ni dawa moja wapo kwenye dawa za kutibu arithmia kundi 1a
Matumizi na dozi
Hutumika kutibu na kuzuia Arithmia ya ventriko na supaventriko, ikijumlisha arithmia inayopatikana baada ya kupata infakshen ya mayokadia na kurejesha rizimu ya sainaz baada ya kufanyiwa kadioveshen
Inatumika kwa kunywa kidonge,
-
Kwa watu wazima kidonge mg 300 -800 kila siku inanywewa kama dozi iliyogawanyika
-
Au kidonge cha mg 250- 375 kila baada ya masaa 12
Marufuku
Kutumika kwa wagonjwa wenye kizuizi kwenye bando ya Atrioventrikula(AV) haswa digree ya kwanza ya pili na tatu ya AV au kizuizi cha bifasaikula, dalili kali za moyo kuferi (isipokuwa endapo zimesababishwa na arizima) na kutofanya kazi vema kwa nodi ya sinaz
Chukua Tahadhari
Kwa wagonjwa wenye Flata ya Atria, au Takikadia na kizuizi kiasi
Zuia kutumika kwa wagonjwa wenye pofria ya ghafla, wazee wenye dalili kali za moyo ulioferi mayasthinia graviz, na wenye tezi dume iliyovimba, magonjwa ya moyo kutokana na maumbile,wenye hatari ya kupata glaukoma ya kufunga pembe
Mwingiliano
Dawa hii inaweza kuingiliana na dawa mbalimbali, endapo mwingiliano ni wa hatari dawa hii haipaswi kutumika kabisa.
Bonyeza kusoma hapa kusoma mwingiliano wa dawa hii na nyingine
Maudhi madogo
-
Kupungua kwa hamu ya kula(apetaiti)
-
Arithmia
-
Madhaifu ya kadiaki konduksheni
-
Shoku ya kadiojeniki
-
Madhaifu ya koginitivu
-
Kuharisha
-
Kukauka kinywa
-
Matatizo ya kutosimamisha uume
-
Haipahidrosisi
-
Haipoglaisemia
-
Haipotenshen
-
Manjano ya kolestatiki (jaundiz)
-
Nutropenia
-
Matatizo ya kisaikotiki
-
Kuongezeka kwa muda wa QT
-
Harara
-
Madhaifu ya mfumo wa mkojo
-
Madhaifu ya kuona
-
Kutapika
Bonyeza hapa kusoma zaidi kuhusu dawa hii na Ujauzito, Kunyonyesha, Ini lisilofanya kazi vema, Figo kuwa na shida, Unahitaji maalumu, Majina mengine ya dawa, Rangi ya dawa. Kumbuka Itakuhitaji kuwa na email tu
ULY clinic inakukumbusha uwasiliane na daktari wako kwa maelezo zaidi ya namna ya kutumia dawa hii