EPD ni aina mojawapo ya magonjwa ya ngozi ya kurithi yanayoipa ngozi mabaka yenye sura kama yai au kutokuwa na mipaka ya kueleweka na yenye rangi ya kijivu au blue iliyokolea kuelekea nyeusi. EPD huweza kutokea shingoni, usoni, na katika kiwiliwili.
EPD ni aina mojawapo ya magonjwa ya ngozi ya kurithi yanayoipa ngozi mabaka yenye sura kama yai au kutokuwa na mipaka ya kueleweka na yenye rangi ya kijivu au blue iliyokolea kuelekea nyeusi. EPD huweza kutokea shingoni, usoni, na katika kiwiliwili.
Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC
Erythema Dyschromicum Perstans
Ugonjwa huu unamaana gani?
Katika makala hii na tovuti hii ugonjwa huu umeitwa kwa jina la erithima diskromikamu pastansi au EDP. EPD ni aina mojawapo ya magonjwa ya ngozi ya kurithi yanayoipa ngozi mabaka yenye sura kama yai au kutokuwa na mipaka ya kueleweka na yenye rangi ya kijivu au blue iliyokolea kuelekea nyeusi. EPD huweza kutokea shingoni, usoni, na katika kiwiliwili.
​
Ugonjwa wa EDP hufahamika kwa jina jingine la dematosisi ya Ramirezi kwa sabababu ya mwnekano wa rangi yake. Ugonjwa huu hutokea sehemu yoyote ya mwili ikiwa pamoja na maeneo yanayopigwa mwanga wa jua au yale ambayo hayapigwi na jua. Asilimia kubwa hutokea kwenye kiwiliwili(asilimia 69), mikono, miguu uso na shingo
Sifa za EDP;
​
-
Mabaka yanaweza kuwa yamesambaa kwa usawa mwili mzima au kuwa upande mmoja wa mwili tu
-
Mabaka ya awali yanaweza kuwa na rangi kama nyekundu, yenye mipaka inaoonekana vema na kama vile kuwa na mwinuko. Hata hivyo hatua hii huwa haionekani kwa watu wengi
-
Mgonjwa huwa mzima kabisa bila kuwa na shida yoyote kimwili na vipimo vya damu huwa vipo kawaida.
​
Historia ya tatizo
Tatizo la EDP huanza taratibu na kutokea, huanza na madoa madogo kisha kukua, na yenye rangi ya kijivu, tatizo huweza kupotea ndani ya miaka 2 au 3
​
Vihatarishi vya kupata tatizo hili
-
Kuwa na ngozi nyeusikama waafrika na wahindi- ugonjwa huu huwa hauonekani kwa watu wenye rangi nyeupe
-
Huweza kutokea kwenye umri wowote ule, lakini huonekana sana kwa watu wazima kuliko watoto, wanawake huathiriwa zaidi kuliko wanaume
Visababishi ni nini
Madaktari bado hawajaweza kutambua haswa ni nini kinachosababisha EDP. EDP huchukuliwa kama toleo la aina tofauti la ugonjwa wa licheni planasi pigimentosasi kutokana na mwonekano wake kwenye kipimo cha histopatholoji. Mambo yafuatayo yanahusianishwa au kusababisha EDP;
​
-
Kurithi vinasaba kutoka kwa wazazi
-
Mzio wa mguso wa vipodozi au dai za kubadilisha rangi nywele
-
Madhara ya kula vyakula vyenye au sumu ya kemikali kama amonium nitrate na barium sulphate na Chlorothalonil
-
Maambukizi ya virusi
-
Maambukizi ya minyoo jmii ya nematode kama whipworm
-
Maudhi makali ya dawa
​
Matatizo mengine yanayofanana na tatizo hili la EDP ni;
​
-
Akwayadi demo macula haipapigimentensheni- ADMH
-
Licheni planasi- LP
-
Matipo lesheni kutokana na matumizi ya dawa
-
Posti inflamatori haipapigmentesheni
-
Yutikaria pigmentosa
-
Inkontineshia pigmenti
-
Pinta
-
Ukoma wa ngozi
​
Ugonjwa wa EPD hutambuliwaje?
Kwa baadhi ya wagonjwa, mwonekano wa mabaka tu na historia ya mgonjwa inaweza kutosha kabisa kutambua tatizo la EDP. Kipimo cha bayopsi ya ngozi kinaweza kuonyesha kuharibik kwa ukuta wa chini wa ngozi kwenye hatua za awali.
Matibabu ni yapi?
​
Matibabu ya EDP huhusisha matibabu ya kulenga mwonekano wa mtu uwe vema. Ugonjwa unaweza kudumu kwa miaka kadhaa, hata hivyo unaweza kupotea wenyewe bila matibabu. Hata hivyo kwa mtu anayetumia matibabu dawa wakati mwingine yanaweza yasifanikiwe kuondoa tatizo.
Matibabu huhusisha;
-
Dawa za kupata jamii ya steroidi
-
Kujianika kwenye mwanga wa UV
-
Tiba mwangawa laser
-
Kukwangua ngozi kwa kutumia kemikali maalumu
Matibabu dhabiti yamekuwa yakitumia ni dawa ya clofazimine, dapson, griseofulvin, hydroxycholoquine, isoniazide na corticosteroids
Matokeo ya ugonjwa
EDP huweza kukaa kwa mtu kwa miaka kadhaa na baadae kupotea, hata hivyo huwa hauna madhara yoyote kwa binadamu isipokuwa wagonjwa huhofu kuhusu mwonekano wao tu wa nje na kushindwa kuvaa nguo wanazozipenda ili kuweza kuficha madoa haya.
ULY CLINIC inakushauri siku zote ufuate ushauri wa daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya
​
​
Rejea za mada,
-
Dermnetnz. Erythema Dyschromicum Perstans. https://www.dermnetnz.org/topics/erythema-dyschromicum-perstans/. Imechukuliwa 06.07.2020
-
-
Mediscape. Erythema Dyschromicum Perstans. https://emedicine.medscape.com/article/1122807-clinical. Imechukuliwa 06.07.2020
-
NCBI. Erythema dyschromicum perstans: A case report and systematic review of histologic presentation and treatment.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6322153/. Imechukuliwa 06.07.2020
-
NCBI. Erythema Dyschromicum Perstans: Response to Topical Tacrolimus. .https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC4601471/. Imechukuliwa 06.07.2020
-
JAMA dermatology. Erythema Dyschromicum Perstans Response to Isotretinoin.https://jamanetwork.com/journals/jamadermatology/fullarticle/2496385. Imechukuliwa 06.07.2020
-
MDedge dermatology. Erythema Dyschromicum Perstans: Successful Treatment With Clofazimine Under a Single-Patient Investigational New Drug Study.https://www.mdedge.com/dermatology/article/68720/nonmelanoma-skin-cancer/erythema-dyschromicum-perstans-successful. Imechukuliwa 06.07.2020