Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Benjamin L,MD
7 Novemba 2021 20:22:47
Damu nyingi kwa mjamzito
Damu nyingi humaanisha kuwa na chembe nyekundu za damu katika kiwango cha juu kuliko kawaida.
Kuwa na damu nyingi kutokana na sababu za kurithi wakati wa ujauzito ni tatizo linalotokea kwa nadra sana na huambatana na matokeo mabaya ya ujauzito, ambapo ni asilimia 40 tu ya wajawazito hupata watoto hai. Matokeo mazuri ya ujauzito hupatikana kama mama atakuwa kwenye makali kwa kutumia dawa za kuyeyusha damu kama aspirini, heparini yenye uzito kidogo na interferon alpha
Dalili
Dalili za damu nyingi ni;
Kutokwa na damu bila sababu mfano kwenye fizi na puani
Kuwashwa haswa unapooga maji ya uvuguvugu
Maumivu ya kichwa
Hisia za mgandamizo chini ya mbavu ya kushoto au hisia za tumbo kujaa muda mfupi baada ya kula upande wa kushoto juu ya kitovu kutokana kukua kwa bandama
Mwili kuwa dhaifu
Kizunguzungu
Kupoteza uzito bila sababu
Kuona vitu vyeusi vinavyokuja na kuondoka
Kuona kitu kimoja kama viwili
Kushindwa kupumua vema
Kuvimba kwa maungio ya mwili haswa kidole gumba
Uso kuwa na rangi nyekundu au mweusi kama mtu aliyeungua na jua
Hisia za ganzi, kuchomachoma na kuungua kwenye, migu, kanyagioa, mikono na viganja
Hisia za ganzi miguuni, kwenye mikono, kanyagio na viganjani
Visababishi
Visababishi vya damu nyingi huweza kuwa;
Sababu za awali
Tatizo hili huweza kutokea kwa sababu mbalimbali zinazoweza kuwa madhaifu ya awali kwenye chembe za erythroid kwenye ma mifupa zinazohusika kutengeneza damu kama ugonjwa wa kuonekana ukubwani wa polycythaemia vera (PV) au wa kurithi kutokana na mabadiliko ya jeni kama erythropoietin.
Sababu za pili
Damu nyingi kutokana na sababu ya pili hutokana na mabadiliko katika jeni zinazohisi oksijeni na sababu mbalimbali zinazotokana na kiwango kidogo cha oksijeni katika tishu.
Magonjwa yanayofanya upungufu wa oksijeni katika tishu kama magonjwa ya mapafu na moyo.
Sababu zisizofahamika
Baadhi ya nyakati, sababu halisiinayosababisha uzalishaji wa damu nyingi inaweza isifahamike, kisababishi hiki huoitwa ‘damu nyingi isiyo na kisababishi’
Madhara ya damu nyingi
Kuwa na damu nyingi husababisha ongezeko la uzito wa damu linalopelekea kuganda kirahisi na kuleta madhaifu yanayotokana na damu kuganda kama kiharusi.
Wagonjwa wengi wenye tatizo la kuzaliwa na damu nyingi huonyesha dalili mapema katika umri mdogo hivyo kuweza gunduliwa pia katika ujauzito.
Matokeo ya ujauzito, matibabu na madhara yanayoweza kutokea kwa wagonjwa wenye damu nyingi hayafahamiki vema kutokana na kutokuwa na taarifa nyingi.
Utambuzi
Utambuzi wa tatizo hili huanza kwa kupima kiwango cha homon inayohusika katika uzalishaji wa chembe nyekundu za damu yenye jina la erythropoietin ( EPO) kama hatua ya awali.
Magonjwa yanayofanana
Magonjwa yanayofahana na damu nyingi ni;
Saratani ya EPO
Magonjwa ya figo
Kuwa kwenye dozi ya EPO
Matibabu
Matibabu ya damu nyingi wakati wa ujauzito yanapaswa kufanyika katika vituo maalumu. Matibabu huhusha matumizi ya dawa na yasiyo dawa.
Matibabu ya dawa
Dawa hulenga kuzuia dalili na madhara yanayoweza kujitokeza na kudhibiti tatizo linalosababisha kama limefahamika.
Dawa za kudhibiti madhara
Madhara yanayotokana na kuganda kirahisi kwa damu kutokana na kuwa nzito hutibiwa na dawa za kuyeyusha damu kama vile;
Aspirin
Heparin yeney uzito kidogo
Dawa za kudhibiti ongezeko la damu
Dawa za kudhibiti kiwango cha chembe nyekundu za damu ni;
Hydroxyruea (Droxia, Hydrea)
Interferon alfa-2b (Intron A)
Ruxolitinib (Jakafi)
Busulfan (Busulfex, Myleran)
Dawa za kudhibiti muwasho
Kudhibiti muwasho miongoni mwa dawa zifuatazo zinaweza kutumika;
Paroxetine
Fluoxetine
Matibabu ya kisababishi
Kuacha kuvuta sigara au kutumia mazao yenye nicotini hupunguza hali ya upungufu wa oksijeni kwenye tishu inayopelekea ongezeko la uzalishaji damu.
Kupata matibabu ya magonjwa ya moyo na mapafu yanayopelekea upungufu wa oksijeni kwenye tishu hudhibiti tatizo la damu nyingi kutokana na sababu hizi.
Matibabu yasiyo dawa
Matibabu yasiyo dawa huhusisha tiba ya kupunguza kiwango cha damu kwa kutoa damu mwilini mara kwa mara.
Kinga
Inaweza kuwa ngumu kujikinga na tatizo hili kama ni la kuzaliwa au linahusisha mabadiliko ya jeni. Hata hivyo unaweza kufanya baadhi ya mambo ili kudhibi baadhi ya visababishi vinavyofahamika kwa;
Kuacha kuvuta sigara na kukaa mbali na moshi wa sigara
Kuacha matumizi ya mazao yenye nicotine kama sigara na mengine
Kuishi maeneo karibu na usawa wa bahari na kuepuka maeneo yaliyo mbali na usawa wa bahari. Maeneo yaliyo mbali na usawa wa bahari huwa na kiwango kidogo cha oksijeni kinachoamsha uzalishaji wa damu.
Matumizi ya dawa za kuyeyusha damu ili kujikinga na madhara.
Vyakula vya kuepuka
Vyakula vya kuepuka kwa wagonjwa wenye damu nyingi ni;
Kutumia mafuta yaliyoshamiri
Matumizi ya nyama nyekundu au zile zilizosindikwa
Matumizi ya magarine
Matumizi ya vyakula vilivyokaangwa
Tiba ya chakula
Vyakula ambavyo vimeonekana kwenye tafiti kudhibiti dalili za damu nyingi kutokana na kufanya kazi kwa namna mbalimbali ni;
Binzari
Kemikali ya resveratrol inayopatikana kwenye wine nyekundu, zabibu nyekundu na zambarau na mulberries
Vyakula vyenye mboga za majani, mbegu, karanga, na chanzo cha protini kutoka kwenye nyama nyeupe na mimea jamii ya kunde hushauriwa kutumika zaidi.
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
7 Novemba 2021 20:22:47
Rejea za dawa
Beillat T, et al. [Polycythemia vera and pregnancy]. J Gynecol Obstet Biol Reprod (Paris). 2004 Oct;33(6 Pt 1):525-7. French. doi: 10.1016/s0368-2315(04)96566-0. PMID: 15567969.
Robinson S, et al. The management and outcome of 18 pregnancies in women with polycythemia vera. Haematologica. 2005 Nov;90(11):1477-83. PMID: 16266894.
Wille K, et al. Differenzialdiagnose der Erythrozytose – Ursachen und klinische Bedeutung [Differential Diagnosis of Erythrocytosis - Background and Clinical Relevance]. Dtsch Med Wochenschr. 2019 Jan;144(2):128-135. German. doi: 10.1055/a-0739-8340. Epub 2019 Jan 23. PMID: 30674061.
Polycythemia vera. National Heart, Lung, and Blood Institute. https://www.nhlbi.nih.gov/health-topics/polycythemia-vera. Imechukuliwa 11.07.2021
Goldman L, et al., eds. Polycythemia vera, essential thrombocythemia, and primary myelofibrosis. In: Goldman-Cecil Medicine. 26th ed. Elsevier; 2020. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 11.07.2021
Cuthbert D, et al. Polycythemia vera-associated complications: Pathogenesis, clinical manifestations, and effects on outcomes. Journal of Blood Medicine. 2019; doi:10.2147/JBM.S189922.
Tefferi A, et al. Polycythemia vera treatment algorithm 2018. Blood Cancer Journal. 2018; doi:10.1038/s41408-017-0042-7.
Tefferi A. Prognosis and treatment of polycythemia vera. https://www.uptodate.com/contents/search. Accessed Dec. 7, 2019.
Griesshammer M, et al. Thromboembolic events in polycythemia vera. Annals of Hematology. 2019; doi:10.1007/s00277-019-03625-x.
Spivak JL. Polycythemia vera. Current Treatment Options in Oncology. 2018; doi:10.1007/s11864-018-0529-x.
Van de Ree-Pellikaan C, et al. Treatment strategies for polycythemia vera: Observations in a Dutch "real-world" cohort study. European Journal of Haematology. 2019; doi:10.1111/ejh.13291.
Ferrari A, et al. Clinical outcomes under hydroxyurea treatment in polycythemia vera: A systematic review and meta-analysis. Haematologica. 2019; doi:10.3324/haematol.2019.221234.