top of page

Elimu ya magonjwa kwa mjamzito

Sehemu hii utajifunza maelezo ya ziada kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa ujauzito. Unashauriwa siku zote kuwasilaina na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile iliyoandikwa humu ili kupata ushauri unaoendana na hali yako ya kiafya.

Wiki ya 6 ya ujauzito

Wiki ya 6 ya ujauzito

Viungo vya nje ya mwili wa mtoto kama vile pua, midomo na masikio huanza kuonekana na mtoto huanza kucheza tumbon, hata hivyo hutaweza kuhisi uchezaji wake.

Wiki ya 5 ya ujauzito

Wiki ya 5 ya ujauzito

Wiki ya 5 mtoto huwa na ukubwa wa sentimita 0.25 na hufanana na kiluwiluwi, hata hivyo ogani kuu kama moyo, ini, figo, mapafu ubongo huwa vimeanza kutengenezwa.

Wiki ya 4 ya ujauzito

Wiki ya 4 ya ujauzito

Mwili wako unapitia kwenye mabadiliko makubwa huku mpira mdogo wa chembe ambao utakuwa mtoto wako hunabadilika na kuwa kiinitete chenye tabaka nyingi. Wakati huu kipimo cha mimba kwenye mkojo hutambua kuwa unaujauzito.

Wiki ya 3 ya ujauzito

Wiki ya 3 ya ujauzito

Wiki ya tatu ya ujauzito ni wiki ambayo uchavushaji wa yai na utungishaji mimba hufanyika. Kipimo cha mimba kinaweza kisioneshe majibu yoyote wakati huu.

Wiki ya 2 ya ujauzito

Wiki ya 2 ya ujauzito

Katika ovari, mayai hukomaa na uovuleshaji hufanyika mwishoni mwa wiki ya pili. Hii ina maana kwamba, moja ya ovari itaruhusu yai moja kutolewa kisha kuingia kwenye mrija wa falopio tayari kwa kurutubishwa.

bottom of page