Mwandishi:
Dkt. Peter A, MD
Mhariri:
Dkt. Sospeter M, MD
22 Novemba 2021, 19:20:19

Wiki ya 6 ya ujauzito
Kuwa na hisia za juu au chini hutokea sana kipindi hiki. Mabadiliko ya hisia hutokea kutokana na mabadiliko ya homon yanayoendelea mwilini mwako wakati mtoto anaendelea kukua.
Ukiweka kando mabadiliko ya homon kando, unaweza kuwa na mabadiliko ya hisia kutokana na mawazo ya hali yako ya ujauzito tu.
Unapaswa kuhudhuria kliniki mara ya kwanza ili kuonana na daktari au mhudumu wa afya kwa ushauri. Mara utakapofika utafanyiwa kipimo cha ultrasound ili kutoa mwangaza wa kijusi tumboni. Kufanya kipimo hiki pia husaidia kuwa na majibu mazuri ya kuliganisha ukuaji wa mtoto na tarehe ya kujifungua.

Mabadiliko kwa kijusi
Mapigo ya moyo ya mtoto huwa kati ya mapigo 100 hadi 160 kwa dakika.
Nini unatakiwa kufanya?
Hupaswi kuwa na hofu endapo utaona unatokwa na matone kidogo ya damu wakati huu haswa kama hayaambatani na maumivu ya tumbo au kubana kwa tumbo la chini
Kutokwa na matone kiasi ya damu ukeni ni hali ya kawaida kama damu inayotoka ni kidogo na inaataka kufanana na damu ya hedhi lakini, huwa na rangi nyekundu au kahawia.
Hata hivyo ukitokwa na damu unapaswa kuwasiliana na daktari kwa ushauri kwa kuwa hali hii inaweza kuashiria pia dalili ya mimba inayotishia kutoka au ujauzito uliotungwa nje ya kizazi. Kutungwa kwa ujauzito nje ya kizazi hutishia uhai wa mama hivyo hutakiwa kudhibitiwa mapema.
Viungo vya mtoto
Wakati huu viungo vya nje ya mwili huanza kuonekana kama vile;
Pua
Midomo
Masikio
Mengine unayopaswa kufahamu
Mtoto huanza kucheza tumboni, kwa vile huwa mdogo sana, hutaweza kupata hisia za mtoto kucheza.
Majina mengine
Majina mengine yanayoendana na mada hii ni:
Ujauzito wa wiki 6
Mimba ya wiki 6
Wiki 6 ya mimba
Kijusi cha wiki 6
Mwonekano wa ujauzito wa wiki 6
ULY Clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kufanya maamuzi yanayohusisha afya yako
Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kutumia namba za simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
12 Julai 2022, 10:24:25
Rejea za dawa
American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]
Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]
Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]
McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]
Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]
Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]
Kagan KO, et al. Principles of first trimester screening in the age of non-invasive prenatal diagnosis: screening for chromosomal abnormalities. Arch Gynecol Obstet. 2017 Oct;296(4):645-651. [PubMed]
Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]
ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]
Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]