top of page

Elimu ya magonjwa kwa mjamzito

Sehemu hii utajifunza maelezo ya ziada kuhusu matatizo mbalimbali ya kiafya wakati wa ujauzito. Unashauriwa siku zote kuwasilaina na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile iliyoandikwa humu ili kupata ushauri unaoendana na hali yako ya kiafya.

Wiki ya 1 ya ujauzito

Wiki ya 1 ya ujauzito

Wakati unapoingia hedhi, mayai mapya hukua kwenye ovari na mimba hutokea takribani wiki mbili baada ya kuanza kwa hedhi.

Upungufu wa damu kwa mjamzito

Upungufu wa damu kwa mjamzito

Upungufu wa damu wakati wa ujauzito licha ya kupelekea athari mbalimbali kwa mama na mtoto kama vile kujifungua njiti, kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo, kupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua n.k. huweza kuzuilika.

Kumkinga kichanga na baridi

Kumkinga kichanga na baridi

Mtoto anapaswa kuwa na joto la kawaida ili mwili wake uweze kuendesha shughuli mbalimbali za kiumetaboli. Baadhi ya njia za kumkinga na baridi huhusisha kumvalisha nguo, kumyonyesha na matunzo ya kangaruu.

Matunzo ya kangaruu

Matunzo ya kangaruu

Matunzo ya kangaruu hutolewa kwa mtoto mchanga kwa kugusanisha ngozi yake na ngozi ya kifua cha mama. Matunzo haya ni thabiti na rahisi kufanyika kuimarisha afya na ustawi wa kichanga.

Mambo muhimu kufahamu kuhusu kichanga

Mambo muhimu kufahamu kuhusu kichanga

Kukingwa dhidi ya baridi, kunyonyeshwa maziwa ya mama tu, kufanyiwa usafi, kupewa chanjo na matunzo maalumu ni miongoni mwa mambo 8 anayopaswa kufanyiwa kichanga chini ya miezi sita ili akue vema na kutougua.

bottom of page