top of page
Faida za kiafya za Mbegu ya chia
Faida za kiafya za Mbegu ya chia

Faida za kiafya za Mbegu ya chia

Chia ni mbegu zinazotoka katika mmea unaoitwa Salvia hispanica, mmea huu hupatikana sehemu nyingi duniani. Mbegu hizi vimepata umaarufu sana maeneo mengi duniani kuwa ni mbegu zenye faida nyingi kiafya. Mbegu hizi ambazo huwa na uwezo wa kuyeyuka zinapowekwa kwenye majimaji huhitaji kutumiwa kwa muda mrefu kidogo ili kupata faida zake. Makala hii imezungumzia kuhusu faida za kiafya za mbegu hizi.

Virutubisho vinavyopatikana kwenye mbegu za chia ni vipi?

Mbegu ya chia ina virutubisho muhimu oamoja na nishati, baadhi ya virutubisho ilivyonavyo kwa wingi ni;

• Nyuzinyuzi
• Nishati
• Protini
• Mafuta ya omega 3
• Madini Kalisiamu
• Madini manganese
• Madini fosforusi
• Madini zinki
• Madini potasiamu
• Vitamin B1,B2na B3

Ifahamike kuwa vijiko viwili vya chakula vya mbegu hii vina nishati ya kalori 101, chia pia huwa haina protini ya gluten hivyo huwa nzuri kwa wagonjwa wenye aleji nap rotini hii inayopatikana kwenye ngano n.k

Faida za kiafya za chia

Faida za kiafya za mbegu ya chia zinaletwa na nyuzinyuzi na virutubisho vilivyomo kwenye mbegu hizi, makala hii imezungumzia faida katika mifumo mbalimbali.

Hutengeneza mazingira mazuri ya umeng’enyaji wa chakula

Kwa kuwa huwa na nyuzinyuzi nyingi, mbegu hizi husfanya shughuli ya umengenyaji wa chakula ifanyike vema mwilini. Hata hivyo chia huwa na uwezo wa kufyonza maji kwa wingi hivyo kukitumia kwenye chakula itakufanya ushibe mapema zaidi. Kwa wale wanaopunguza uzito mbegu hizi ni nzuri kuzitumia kutokana na kufanya ushibe haraka na pa kupata haja laini.

Mbegu hizi pia huwa chakula kizuri cha bakteria marafiki katika utumbo wako, bakteria hawa hutumia chakula hiki na huwa na afya njema. Bakteria hawa wakiwa na afya njema hufanya mfumo wako wa umeng’enyaji uchakula usiwe na matatizo .

Hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo

Tafiti chache zimeonyesha kuwa mbegu za chia zina uwezo wa kupunguza shinikizo la juu la damu hivyo kupelekea kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo. Hata hvyo tafiti nyingi zaidi zinahitajika kufanyika ili kutambua umuhimu wa mbegu hizi katika kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo.

Huimarisha mifupa

Protini na madini ya kalisiamu, fosforasi, magnesium husaidia sana kwenye afya ya mifupa. Vijiko viwili vya mbegu za chia huwa na kiwango cha asilimia 18 ya madini ya kalisiamu ambao ni muhimu kwa kuimarisha mifupa yako, mtu mwenye upungufu wa madini haya anaweza kuyapata kiasi cha kutosha kwa kula mbegu hizi.

Tafiti zinaonyesha kuwa mbegu hizi huwa na kemikali ya phytic acid ambayo huweza kuzuia ufyonzaji wa madini ya kalisiamu kwa kiasi kidogo.

Kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu

Tafiti kwa zilizofanyika kwa wanyama zinaonyesha kuwa matumizi ya mbegu za chia yanaongeza uwezo wa mwili kutumia sukari kwa kupunguza upinzani wa mwili dhidi ya homoni insulin inayohusika kuondoa sukari kwenye damu. Matumizi ya mbegu hizi huzuia sukari kupanda kwa kiasi kikubwa kwenye damu.

Tafiti zilizofanyika kwa binadamu zinaonyesha kuwa, kiwango cha sukari huwa cha chini endapo mtu akitumia mkate pamoja na mbegu za chia ukilinganisha na mtu ambaye amekula mkate tu bila mbegu hizi.

Hupunguza kiwango cha kiashiria cha uvimbe kwenye damu kwa jina la C-reactive protein (CRP)

Kutokana na tafiti zilizofanyika kwa wagonjwa wa kisukari waliotumia gramu 37 za mbegu hizi za chia kwa siku kwa muda wa miezi mitatu tu, kiwango cha CRP kilionekana kupungua kwenye damu mara dufu zaidi kuliko kwa wale ambao hawakutumia. Kiwango cha CRP huwa kikubwa kwa watu wanaovuta sigara, wasiofanya mazoezi na kutokula vema. CRP hufahamika kuhusiana na saratani na magonjwa mbalimbali ya moyo na mfumo wa tumbo. Hata hivyo faida za kupunguza CRP bado hazifahamiki vizuri, tafiti zinahitajika kufanyika zaidi kutambua faida hizo mwilini.

Matumizi ya kiwango cha juu ya mbegu hizi hupunguza kuamka kwa dalili za ugonjwa wa diverticulosis, sababu ikifahamika kuwa hufyonzaji maji kwenye utumbo na kufanya haja kubwa iwe laini na itoke kirahisi.

Huwa na mafuta ya ya omega-3

Huwa na kiwango kikubwa cha mafuta ya omega 3 aina ya linoleic na alpha-linolenic (ALA) acid ambayo ni vigumu sana kutumiwa na mwili wa binadamu, utahitaji kula lita tano ili utapte kiwango sawa ambacho unaweza kukipata kutoka kwenye vyakula vingine kwa siku.

Mafuta ya omega 3 kutoka kwenye vyanzo vingine (mimea na viumbe wa baharini mfano samaki n.k) huwa na umuhimu mwilini. Tafiti zinaonyesha mafuta ya omega 3 huweza kupunguza kiwango cha kolestro kwenye damu na hivyo kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo. Inashauriwa kutegemea mafuta ya omega -3 kutoka kwenye vyanzo vingine zaidi kuliko kwenye mbegu za chia kwa sababu licha ya kuwa na mafuta haya kwa wingi mwili wako hauna uwezo wa kuyatumia.

Huupa mwili nguvu

Vijiko viwili vya mbegu za chia huwa na kiwango cha nishati za kalori 101. Nishati hii ni muhimu mwilini. Kwa wale wanaotaka kupunguza uzito, kutumia mbegu hizi kwenye maji ya moto wakati wa asuhuhi kabla ya kunywa chai na wakati wa mchana kabla ya kula chakula kutakufanya ujihisi umeshiba na kula kidogo hivyo kuwa kama nyenzo nzuri ya kukufanya ufikie malengo ya kupunguza uzito

Namna ya kutumia mbegu za chia kupata faida za kiafya

Unaweza kutumia mbegu hizi kwa kuweka kwenye vyakula mbalimbali, inashauriwa utumie vijiko viwili mara mbili kwa siku ili kupata faida zake. Tumia mbegu hizi kwa;

• Kuwekwa kwenye uji
• Kuwekwa kwenye juisi isiyochujwa
• Kutumia kwenye mikate iliyokwisha okwa
• Unaweza kuzinyunyizia kwenye chakula kingine kama maziwa mtindi, mboga za majani zilizopikwa au wali uliopikwa
• Unaweza kutumia kuongeza uzito mchuzi wa chakula chako
• Unaweza kutumia kama mbadala wa mayai

ULY CLNIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa elimu na ushauri kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu zilizo chini ya tovuti hii au bonyeza pata tiba.

Imeboreshwa,

29 Novemba 2020 10:49:59

Rejea za mada hii,

1. Healthline. 22 High Fiber Foods You Should Eat. https://www.healthline.com/nutrition/22-high-fiber-foods. Imechuukuliwa 26.11.2020
2. Francisco Guarner etal. Gut flora in health and disease. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/12583961. Imechuukuliwa 26.11.2020
3. Vladimir Vuksan etal. Supplementation of conventional therapy with the novel grain Salba (Salvia hispanica L.) improves major and emerging cardiovascular risk factors in type 2 diabetes: results of a randomized controlled trial. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/17686832. Imechuukuliwa 26.11.2020
4. Janet K Snell-Bergeon etal. Hypoglycemia, diabetes, and cardiovascular disease. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/22650225. Imechuukuliwa 26.11.2020
5. Antonio Ceriello, MD. Postprandial Glucose Levels Are a Clinically Important Treatment Target. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC2909084/. Imechuukuliwa 26.11.2020
6. V Vuksan etal. Reduction in postprandial glucose excursion and prolongation of satiety: possible explanation of the long-term effects of whole grain Salba (Salvia Hispanica L.). https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/20087375. Imechuukuliwa 26.11.2020
7. H Ho etal. Effect of whole and ground Salba seeds (Salvia Hispanica L.) on postprandial glycemia in healthy volunteers: a randomized controlled, dose-response trial. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/23778782. Imechuukuliwa 26.11.2020
8. chia seed. The nutrition source. https://www.hsph.harvard.edu/nutritionsource/food-features/chia-seeds/. Imechuukuliwa 26.11.2020
9. What are the benefits of chia seeds? https://www.medicalnewstoday.com/articles/291334#. Imechuukuliwa 26.11.2020
10. Is Eating Chia and Flax Enough to Meet Your Daily Omega-3 Needs?. https://www.nordicnaturals.com/healthy-science/is-eating-chia-and-flax-enough-to-meet-your-daily-omega-3-needs/. Imechuukuliwa 26.11.2020

bottom of page