top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Peter R, CO

Dkt. Benjamin L, MD

Alhamisi, 18 Novemba 2021

Binzari
Binzari

Binzari ni mmea unaoota aridhini na kutengeneza mizizi ambayo hutumika kama kiungo cha chakula na dawa. Mmea huu wenye asili ya India huwa na viuaji sumu kwa wingi na kemikali ya curcumin muhimu kwenye afya ya ubongo na mwili.


Virutubisho muhimu vinavyofanya kazi kama dawa ndani ya binzari hufyonzwa vema kama itatumika pamoja na pilipili manga.


Kuna aina nyingi za binzari lakini maarufu zaidi ni binzari ya manjano na binzari nyekundu.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye binzari


 • Mafuta

 • Protini

 • Nyuzilishe

 • Sukari

 • Madini

 • Vitamini

 • Kabohaidreti


Viinilishe vinavyopatikana kwenye binzari yenye ujazo wa gramu 100


 • Nishati = 312 Kilo kalori

 • Kabohaidreti = 67.14g

 • Mafuta = 3.25g

 • Protini = 9.68g

 • Nyuzilishe = 23g

 • Sukari = 3.2g

 • Maji = 12.85g


Madini yanayopatikana kwenye binzari yenye ujazo wa gramu 100


 • Kalishiamu = 168mg

 • Kopa = 1.3mg

 • Madini chuma = 55mg

 • Magineziamu = 208mg

 • Manganaizi = 19.8mg

 • Potashiamu = 2080mg

 • Fosifolasi = 299mg

 • Seleniamu = 6.2mg

 • Sodiamu = 27mg

 • Zinki = 4.5mg


Vitamini zinazopatikana kwenye binzari yenye ujazo wa gramu 100


 • Vitamini B1 = 0.058mg

 • Vitamini B2 = 0.150mg

 • Vitamini B3 ­= 1.350mg

 • Vitamini B5 = 0.542mg

 • Vitamini B6 = 0.107mg

 • Vitamini B9 = 20mg

 • Vitamini C = 0.7mg

 • Vitamini E = 4.43mg

 • Vitamini K = 13.4mg


Faida ya binzari kwenye mwili wa bianadamu


 • Huboresha afya ya ngozi

 • Hurekebisha kiwango cha suakri mwilini

 • Huondoa uchovu na kuupa mwili nguvu

 • Huondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume

 • Huimarisha afya ya moyo, ngozi pamoja na ini

 • Huzuia kasi ya kupata ugonjwa wa kusahau pamoja na saratani

 • Huchangamsha mwili na kuondoa mawazo

 • Husaidia kupunguza uzito

 • Huimarisha mmeng`enyo wa chakula

 • Inapunguza athari ya ugonjwa wa baridi yabisi


Imeboreshwa,
18 Novemba 2021 16:03:57
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. Vaughn, et al (2016). "effects of turmeric (curcuma longa) on skin health: a systematic review of the clinical evidence". Phytotherapy research. 30 (8): 1243–64.

 2. Daily, et al (2016). "efficacy of turmeric extracts and curcumin for alleviating the symptoms of joint arthritis: a systematic review and meta-analysis of randomized clinical trials". Journal of medicinal food. 19 (8): 717–29.

 3. Niir. board of consultants & engineers (2006). The complete book on spices & condiments (with cultivation, processing & uses). Delhi: asia pacific business press. Pp. 188–191. Isbn 9788178330389.

 4. Imtiaz, et al(11 may 2016). "turmeric latte: the 'golden milk' with a cult following". The guardian. Imechukuliwa 18.11.2021

 5. Health line. https://www.healthline.com/nutrition/top-10-evidence-based-health-benefits-of-turmeric#TOC_TITLE_HDR_3. Imechukuliwa 18.11.2021

bottom of page