Dalili za magonjwa ya zinaa kwa wanawake ni zipi?
top of page
To see this working, head to your live site.
Edited: Jul 02, 2021
Dalili za gono kwa mwanamke ni zipi?
Dalili za gono kwa mwanamke ni zipi?
3 answers0 replies
Like
Maoni (3)
bottom of page
Utajua kwamba umepona gono kwa dalili zilizokuwepo kupotea.
Utajuwaje kama umepona gono
Dalili za gono kwa wanawake
Dalili za gono au gonorrhea (hufahamika pia kama gonorea au kisonono) kwa wanawake na wanaume huwa hazina utofauti mkubwa isipokuwa kuchelewa kuonekana kwa wanawake.
Tafiti zinaonyesha ni asilimia 20 hadi 50 tu ya wanawake walioambukizwa gono huwa wanaonyesha dalili. Hata hivyo dalili za gono kwa wanaume huonekana haraka. Soma zaidi kuhusu dalili za gono kwa wanaume sehemu nyingine ya tovuti hii.
Dalili hizo hizo ni zipi?
Endapo dalili za gono kwa wanawake zitatokea, zifuatazo huwa miongoni mwa dalili;
Kutoka ute, usaha au maji machafu ukeni
Kutokwa na ute wenye harufu kali ukeni
Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
Kutokwa na ute wenye rangi ya njano, kijani au nyingine tofauti na kawaida ukeni
Matibabu ya gono kwa wanawake
Licha ya kuchelewa kutokea na kuwa na utofauti mdogo, matibabu ya gono hususisha matumizi ya dawa za antibiotiki zinazolenga kuua vimelea vya magonjwa yote ya zinaa endapo yataonekana kwenye vipimo ambayo ni kisonono, pangusa, trikomoniasisi, kaswende, chunjua na herpes. Orodha ya dawa za gono zinapatikana katika makala ya 'dawa za gono' au kwa kubofya hapa.
Majina mengine ya dalili za gono
Dalili za gono hufahamika na wagonjwa kwa majina ya 'dalili za kisonono', 'kutokwa usaha kwenye uume', kutokwa uchafu unaonuka ukeni,'kutokwa uchafu rangi ya njano au kijani au kahawia sehemu za siri' na 'ugonjwa wa zinaa'
Wapi utapata maelezo zaidi kuhusi gono kwa wanawake?
Kwa maelezo zaidi kuhusu gono na dalili za gono au 'dalili za kisonono' ingia kwa kubofya hapa
Mambo muhimu kufahamu kukumbuka kuhusu dalili za gono kwa wanawake
Dalili za gono zinaweza kufanana na magonjwa mengine ya zinaa, hakikisha siku zote unawasiliana na daktari wako kabla ya kujipa ugonjwa na kufanya matibabu pasipo ushauri wa daktari wako.
Wapi unaweza kupata msaada zaidi?
Endapo una maswali zaidi, wasiliana na daktari wako kwa ushauri na tiba.
Waweza wasiliana pia na daktari wa ULY CLINIC moja kwa moja kupitia kitufe cha 'mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii.
Rejea za mada hii
ULYCLINIC. Dalili za gono. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/Dalili-za-Gono%28kisonono%29. Imechukuliwa 02.07.2021
ULY CLINIC. Dawa za gono. https://www.ulyclinic.com/dawa-gono. Imechukuliwa 02.07.2021
NHS. STIs. https://www.nhs.uk/conditions/sexually-transmitted-infections-stis/. Imechukuliwa 02.07.2021
ULY CLINIC. rangi ya ute ukeni na maana yake kiafya. https://www.ulyclinic.com/post/rangi-ya-majimaji-ukeni-na-maana-zake-kiafya-uly-clinic. Imechukuliwa 02.07.2021