top of page

Rangi ya ute ukeni na maana yake kiafya

Updated: Nov 6, 2021

Majimaji (ute) ya kawaida yanayotoka ukeni huzalishwa na tezi ndogo zinapatikana kwenye tundu la uke na shingo ya kizazi. Majimaji au ute huu hutoka kila siku ili kuondoa chembe zilizokufa na uchafu na kufanya uke uwe kwenye hali safi ya kiafya. Kiasi na rangi ya majimaji yatokayo ukeni hutofautiana kila siku na kwa kila mtu mmoja na mwingine. Kiasi na rangi ya majimaji yatokayo ukeni hutofautiana kila siku na kwa kila mtu mmoja na mwingine.


Makala hii imeelezea aina za ute na maana yake kiafya. Ute umetumika kumaanisha majimaji ya kawaida au uchafu unaoweza kutoka ukeni.


Je rangi ya ute ukeni zinazohamika ni zipi?Rangi zinazoonekana hapa ni zile ambazo zimeelezewa hapa chini
Rangi ya majimaji ukeni na maana yake kiafya

Kuna rangi mbalimbali za ute unaoweza kutoka ukeni, rangi hizo ni;

 • Ute mweupe kama maziwa

 • Ute wa rangi nyeupe ya maji

 • Ute wa rangi nyekundu

 • Ute wa rangi ya kijivu

 • Ute wa rangi ya kijani

 • Ute wa rangi ya njano

 • Ute wa rangi ya bluu

Kila rangi imeelezewa hapa chini ni nini kinawez akuwa kisababishi


Ute mweupe rangi ya maji ukeni


Ute wa kawaida ukeni huwa na rangi kama ya maji kwa watu wengine huita uta mweupe lakini weupe si kama wa maziwa bali weupe wa maji. Licha ya kuwa mweupe kama maji, pia huwa na utelezi mithiri ya utelezi wa maji ya bamia au yai .


Ute ute huzidi kuteleza zaidi na kuwa mweupe zaidi kipindi cha hatari (kipindi yai linatolewa), wakati wa kusisimuliwa kingono na wakati wa ujauzito.


Ute wa rangi ya maziwa ukeni


Kutokwa na ute wa rangi nyeupe kama maziwa ukeni ni nini kisababishi?


Kutokwa ute wa rangi ya maziwa inamaanisha kutokwa na uchafu ulio mzito na mweupe kama maziwa au kuwa laini kama mafuta mgando(krimu).


Endapo ute huo hauambatani na dalili zingine ukeni, hii humaanisha ute wa kawaida kwa ajili ya kulainisha uke.


Endapo ute huu una harufu kali huweza kuashiria maabukizi ukeni na mara nyingi humaanisha maambukizi ya ‘fangasi ukeni’ ambapo huweza kupelekea dalili zingine za muwasho ukeni.


Ute wa rangi ya njano mpauko ukeni


Kutokwa na ute wenye rangi ya njano mpauko bila kuwa na dalili zingine humaanisha ute wa kawaida kwa ajili ya kulainisha uke na huweza kusababishwa pia mabadiliko ya chakula au matumizi ya virutubisho nyongeza.


Endapo ute una rangi ya njano iliyokolea au njano inayoelekea kijani, mara nyingi humaanisha maambukizi ya 'magonjwa ya zinaa'. Dalili zingine zinazoweza kuambatana ni, harufu mbaya, kama ya kuoza samaki, majimaji kuwa mazito zaidi au mabonge.


Endelea kusoma rangi zingine zaidi kwa kubofya hapa


Kusoma kuhusu ugonjwa wa vajinosis ya bakteria bofya hapa


Rejea za makala hii;

 1. 5 Types of vaginal discharge & what they mean. https://www.unitypoint.org/livewell/article.aspx?id=06f8f035-9f6e-4a79-bb58-9045b9d7d0d8. Imechukuliwa 16.06.2021

 2. Merck manual. Vaginal discharge. https://www.merckmanuals.com/home/women-s-health-issues/symptoms-of-gynecologic-disorders/vaginal-discharge. Imechukuliwa 16.06.2021

 3. Vaginal discharge. http://www.pamf.org/teen/health/femalehealth/discharge.html. Imechukuliwa 16.06.2021

 4. Vaginal discharge. https://familydoctor.org/condition/vaginal-discharge/. Imechukuliwa 16.06.2021.

 5. Vaginal discharge. https://www.hhs.gov/opa/reproductive-health/fact-sheets/vaginal-discharge/index.html. Imechukuliwa 16.06.2021

 6. Vaginal discharge. https://www.sutterhealth.org/health/teens/female/vaginal-discharge. Imechukuliwa 16.06.2021

 7. Vaginal discharge.https://www.drugs.com/health-guide/vaginal-discharge.html. Imechukuliwa 16.06.2021

 8. What's the cervical mucus method of FAMs?. https://www.plannedparenthood.org/learn/birth-control/fertility-awareness/whats-cervical-mucus-method-fams. Imechukuliwa 16.06.2021

1,196 views1 comment

Recent Posts

See All

댓글 1개


Dr.Sospeter Mangwella, MD
Dr.Sospeter Mangwella, MD
2022년 2월 14일


좋아요
bottom of page