Swali 1: Je ni kawaida kwa mtoto mchanga kupata choo mara kwa mara kidogo kidogo?
Jibu:
Kujisaidia ni afya kwa kichanga na husaidia kuondoa maumivu ya tumbo(chango) hivyo hakuna shida na pia itapungua siku zinavyoenda.
Swali 2: Kinachonifanya nipate hofu ni kuna muda nakuta amejisaidia majimaji tu kaloana sehemu ya haja kubwa, hii ni kawaida?
Jibu:
Majimaji kuzunguka njia ya haja kubwa yanaweza kutokana na mkojo wa mtoto haswa akiwa amevalishwa nepi qu pampasi isiyofyonza maji vema. Kwa kuwa mara nyingi mtoto hulala chali, anapokojoa ni rahisi nkojo wake kwenda katikati ya makalio na mapaja na hivyo ukaona dalili kama hiyo.