Kasi ya kusafisha pombe kwenye damu inayofanywa na Ini pamoja na figo inategemea jinsia ya mtu, uzito, umri, hali ya kiafya, kiwango cha shughuli za metaboliki, kiwango na aina ya pombe iliyotumiwa, dawa ulizotumia pamoja na pombe, na aina au kiasi cha chakula ulichotumia pamoja na pombe.
Kwa wastani inachukua saa moja(1) kwa mwili kuondoa uniti moja ya pombe kwenye damu
Uniti moja ya pombe hupatikana kwa kuzidisha kiasi cha kilevi kwenye pombe mara ujazo wa pombe( kwa mililita) kisha gawanya kwa elfu moja(1000). Mfano bia ya kawaida ina asilimia 6% ya kilevi na ujazo wake kwenye chupa ni mililita 300. Pombe hii itakuwa na uniti za kilevi ambazo ni 1.8 yaani (6*300)/1000
Hivyo mtu akinywa bia moja kama iliyotolewa mfano hapo juu itachukua takribani masaa mawili kutolewa mwilini.
Mfano mwingine Mtu anayetumiwa wine jamii ya dompo endapo atakunywa chumba nzima, yenye mililita 750 na kiasi cha kilevi 18% uniti atakazokuwa ametumia ni (18*750)1000 ambapo jibu litakuwa ni unit 13.5. hivyo pombe itaisha kwenye damu baada ya masaa 13 hadi 14 mara baada ya kunywa pombe.
Mfano wa tatu, endapo mtu ametumia bia yenye mililita za ujazo wa 300 na kiwango cha pombe ni asilimia 6 na ametumia bia tatu. Uniti alizotumia itakuwa sawa na (6*300*3)/1000 ambapo jibu ni uniti 5.4 hivyo itachukua takribani masaa matatu hadii manne kwa mwili kusafisha kiwango cha bia tatu katika damu.
Jibu