Nini matokeo ya vipimo vya HIV (Bioline) kwa mtu anaye tumia dawa za ARV, na je kama kipimo kitaonesha negative ni salama kwa mpenzi wake kushiriki tendo bila kumuambukiza?
top of page
To see this working, head to your live site.
Nini matokeo ya vipimo vya HIV (Bioline)
Nini matokeo ya vipimo vya HIV (Bioline)
4 answers1 reply
Like
Maoni (5)
bottom of page
Dilisha la matazamio
Window period ya HIV au dilisha la matazamio la vipimo vya VVU ni muda utakaopita tangu kupata maabukizi na kabla ya kutambulika kuwa na maambukizi ya VVU kwa kutumia aina fulani ya kipimo. Muda huu hutofautiana kati ya kipimo na kipimo, kati ya mtu mmoja na mwingine na hutegemea aina ya sampuli pia iliyotumika yaani damu ya mishipa au ya kidole au sampuli ya mate.
Dilisha la matazamio ni muda gani?
Vipimo vingi vya haraka vya VVU vinavyotambua maambukizi kwa kutambua uwepo wa immunoglobin G, M na antijeni p24 ya kirusi huwa na dilisha la matazamio kati ya siku 45 hadi 90( sawa na miezi mitatu) hii ina maansha asilimia 99 ya watu walio na maambukizi ya VVU watatambulika ndani ya kipindi cha siku 45 hadi 90.
Vipimo vya VVU
Kuna madaraja manne ya vipimo vya kutambua VVU, vipimo dalaja la nne ni vipimo vinavyoweza kutambua kwa muda mfupi zaidi ukilindaganisha dalaja la la pili na kwanza ambayo huchukua takribani siku 90 kutambua asilimia 99 ya watu waliopata maambukizi. Kipimo cha HIV SD bioline kipo kwenye daraja la tatu la vipimo vya VVU. Maelezo kwa undani ya muda wa matazamio ya vipimo mbalimbali vya VVU unayapata kwenye linki hii.
Rejea za mada hii;
British HIV Association, British Association for Sexual Health and HIV and British Infection Association. Adult HIV Testing Guidelines 2020.
Kevin P. et al. Time Until Emergence of HIV Test Reactivity Following Infection With HIV-1: Implications for Interpreting Test Results and Retesting After Exposure, Clinical Infectious Diseases, Volume 64, Issue 1, 1 January 2017, Pages 53–59, https://doi.org/10.1093/cid/ciw666
Delaney KP et al. Time from HIV infection to earliest detection for 4 FDA-approved point-of-care tests. https://www.croiconference.org/abstract/time-hiv-infection-earliest-detection-4-fda-approved-point-care-tests/. Imechukuliwa 31.10.2021
Avert. How do hiv tests work and what's involved?. https://www.avert.org/hiv-testing/whats-involved. Imechukuliwa 31.10.2021
Window period ya sd bioline ni muda gani?
Window period ya sd bioline ni muda gani?
Ni salama endapo Hana maambukizi ya VVU yaani Negative. kipimo Cha HIV SD bioline husoma mtu Ana maambukizi ya VVU hata Kama anatumia Dawa, hii Ni kwa sababu vipimo hivi hupima antibody zinazotolewa na mwili kupambana na kirusi na huwa hazipotei kwenye damu hata Kama virusi vipo kwa kiwango kiasi gani kwenye damu. Karibu Sana kwa maswali zaidi Kupitia Namba zetu.