Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dkt. Benjamin L, MD
ULY CLINIC
8 Machi 2026, 23:26:04
.jpg)
UKIMWI unaonekana baada ya muda gani kwenye kipimo?
Swali la msingi
Ni baada ya muda gani tangu kupata maambukizi ya VVU unaweza kugundulika kwa kipimo kuwa una virusi vya UKIMWI (VVU)?
Majibu

Katika hatua za awali za maambukizi ya VVU, mwili huanza kutoa ishara mbalimbali kupambana na virusi, lakini si mara moja kipimo kinaweza kugundua maambukizi haya. Uwezo wa kipimo kugundua maambukizi hutegemea aina ya kipimo kinachotumika na teknolojia yake.
Kipindi cha dirisha la matazamio
Kipindi cha dirisha ni muda kati ya kupata maambukizi na wakati ambapo kipimo kinaweza kutambua maambukizi hayo. Kipindi hiki ni muhimu kwa sababu mtu anaweza kuwa ameambukizwa lakini vipimo vya awali visionyeshe maambukizi — hali inayojulikana kama matokeo hasi ya uongo.
Aina za vipimo na muda wake wa kugundua VVU
Aina ya Kipimo | Kinaweza Tambua Maambukizi Kuanzia | Maelezo Mafupi |
DNA PCR | Kuanzia siku ya 9–14 | Hutambua vinasaba vya virusi. Hupatikana zaidi kwenye maabara maalum au benki ya damu. Gharama ni kubwa kwenye nchi zinazoendelea. |
Kipimo cha Antijeni/Antibodi (Kizazi cha 4) | Siku 18–45 | Kipimo cha kisasa kinachotambua antijeni ya p24 pamoja na antibodi. Hupatikana katika VCT na hospitali nyingi. |
Kipimo cha Antibodi pekee (Kizazi cha 3) | Siku 30–90 | Hutegemea kinga ya mwili (antibodi). Kipimo hiki sasa kimeboreshwa na kinaweza kugundua mapema zaidi kuliko zamani. |
RNA PCR (Kipimo cha nakala za virusi kwenye damu) | Siku 10–14 | Hutambua RNA ya virusi. Hupatikana zaidi kwa wagonjwa waliothibitishwa kwa ajili ya kufuatilia kiwango cha virusi. |
Je, kuna kipimo kinachogundua VVU ndani ya masaa 24?
Hapana. Mpaka sasa hakuna kipimo kilichothibitishwa kuwa na uwezo wa kugundua VVU ndani ya masaa 24 baada ya maambukizi. Hata vipimo vya kisasa kama DNA PCR au RNA PCR
