Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULY CLINIC
17 Julai 2025, 18:26:13
Azuma inatibu nini?
AZUMA inatibu maradhi yanayosababishwa na vimelea wanaouliwa na dawa hii. Magonjwa yanayotibiwa na azuma yameorodheshwa hapa chini.
Magonjwa yanayotibika kwa kutumia AZUMA
Magonjwa yafuatayo huweza kutibika kwa kutumia AZUMA na wakati mwingine huhitaji kuchanganywa na dawa zingine kwa ufanisi;
Ugonjwa wa PID iliyosababishwa na Chlamydia trachomatis, Neisseria gonorrhoeae, au Mycoplasma hominis.
Magonjwa ya zinaa yaliyosabaishwa na Chlamydia trachomatis au Neisseria gonorrhoeae.
Vidonda sehemu za siri kwa mwanaume viliyosababishwa na Haemophilus ducreyi (chancroid).
Tonses au maambukizi/michomokinga kwenye koo yaliyosababishwa na Streptococcus pyogenes.
Nimonia iliyosababishwa na Chlamydophila pneumoniae, Haemophilus influenzae, Mycoplasma pneumoniae au Streptococcus pneumoniae.
Magonjwa ya masikio kwa watoto yaliyosababishwa na Haemophilus influenzae, Moraxella catarrhalis au Streptococcus pneumoniae.
Magonjwa ya ngozi iliyosababishwa na Staphylococcus aureus, Streptococcus pyogenes au Streptococcus agalactiae
Ugonjwa mkali wa kuziba kwa sainazi au ugonjwa wa michomokinga kwenye sainaz iliyosababishwa na Haemophilus influenzae, Moraxella catarrhalis au Streptococcus pneumoniae.
COPD kali kutokana na Haemophilus influenzae, Moraxella catarrhalis au Streptococcus pneumoniae.
Tahadhali ya matumizi ya AZUMA
Kama ulishawahi pata manjano au tatizo la ini baada ya kutumia dawa azithromycin, usitumie dawa hii. Matumizi holela ya dawa pasipo kuandikiwa na daktari au vipimo husababisha vimelea kuwa sugu kwenye dawa Kabla ya kunywa azithromycin
Fahamu kwanza kama una mzio na dawa hii na dawa zingine kwenye kundi moja ambazo ni
Clarithromycin
Erythromycin na
Telithromycin
Mambo ya kumshirikisha daktari kabla ya kutumia azuma
Vitu vya kumshirikisha daktari Ili kuhakikisha kuwa azithromycin itakuwa salama kwako, hakikisha unamwambia daktari kama umewahi kutibiwa magonjwa yafuatayo;
Magonjwa ya ini
Magonjwa ya figo
Myasthenia gravis
Magonjwa ya moyo
Upungufu wa potassium kwenye damu
Wapi utapa maelezo zaidi kuhusu azuma?
Pata maelezo zaidi katika makala zifuatazo
Maswali yaliyoulizwa sana kuhusu azuma
1. Azuma hutumiwa kutibu nini?
Azithromycin hutumiwa kutibu maambukizi ya bakteria kama vile magonjwa ya njia ya hewa (pumu inayoambatana na maambukizi, bronkaitis), maambukizi ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya ngozi, na magonjwa ya zinaa kama Klamidia.
2. Kazi kuu ya azithromycin ni nini?
Kazi kuu ya azithromycin ni kuua au kuzuia ukuaji wa bakteria wanaosababisha maambukizi mwilini.
3. Ni nini wigo wa shughuli za azithromycin?
Azithromycin ina wigo mpana wa kuzuia bakteria aina mbalimbali, hasa bakteria wa aina ya Gram-chanya na Gram-hasi, na husaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa tofauti.
4. Kwa nini dozi ya azithromycin ni fupi sana?
Dozi ya azithromycin ni fupi kwa sababu dawa hii ina nusu- maisha mrefu mwilini, hivyo inabaki mwilini kwa muda mrefu na kuendelea kufanya kazi hata baada ya kuchukuliwa kwa siku chache tu.
5. Je, ni sawa kuchukua antibiotics kwa siku 3 tu?
Ndiyo, kwa azithromycin, mara nyingi kozi fupi ya siku 3 inatosha kutibu maambukizi fulani, lakini ni muhimu kufuata maelekezo ya daktari na kuhakikisha unamaliza kozi yote.
6. Azithromycin inatumiwa kwa siku ngapi?
Azithromycin kawaida hutumiwa kwa kozi fupi za siku 3 hadi 5, lakini muda na dozi hutegemea aina ya maambukizi na ushauri wa daktari.
Rejea za mada hii:
Azithromycin. ncbi.https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK557766/. Imechukuliwa 15.10.2024
Dunne MW, Singh N, et al. A multicenter study of azithromycin, alone and in combination with chloroquine, for treating acute uncomplicated Plasmodium falciparum malaria in India. J Infect Dis. 2005 May 15;191(10):1582-8.
Girard AE, Girard D, et al.Pharmacokinetic and in vivo studies with azithromycin (CP-62,993), a new macrolide with an extended half-life and excellent tissue distribution. Antimicrob Agents Chemother. 1987 Dec;31(12):1948-54.
Romano A, Valluzzi RL,et al. Cross-Reactivity and Tolerability of Cephalosporins in Patients with IgE-Mediated Hypersensitivity to Penicillins. J Allergy Clin Immunol Pract. 2018 Sep-Oct;6(5):1662-1672.
Sidhu AB, Sun Q, et al. In vitro efficacy, resistance selection, and structural modeling studies implicate the malarial parasite apicoplast as the target of azithromycin. J Biol Chem. 2007 Jan 26;282(4):2494-504.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
