top of page
Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

ULY CLINIC

8 Juni 2025, 07:31:04

Damu au kinyama mimba ya mwezi mmoja ikiharibika (1).jpg

Dalili za utoaji mimba usio kamili baada ya kutumia Misoprostol

Baada ya kutumia Misoprostol, mimba inapaswa kutoka kabisa. Hata hivyo, kuna hatari ya utoaji mimba usiokamilika, ambapo baadhi ya tishu za mimba hubaki ndani ya mji wa mimba (mfuko wa kizazi). Hii inaweza kusababisha maambukizi na matatizo mengine ya kiafya.


Dalili za Utoaji mimba Usio kamili kwa kutumia misoprostol

Zifuatazo ni baadhi ya dalili za utoaji mimba usiokamili:

  • Kutokwa na damu kwa muda mrefu (zaidi ya wiki 2-3).

  • Kutokwa na damu nyingi kupita kiasi (zaidi ya kipindi cha hedhi cha kawaida, au kubadilisha pedi nyingi kwa saa chache).

  • Maumivu makali ya tumbo yanayoendelea kwa siku kadhaa baada ya kutumia Misoprostol.

  • Maumivu makali yasiyovumilika hata baada ya kutumia dawa za kupunguza maumivu.

  • Homa (joto la mwili kuongezeka), ambayo inaweza kuwa ishara ya maambukizi.

  • Kutokwa na damu bila kukoma kwa zaidi ya wiki 3.

  • Maumivu makali wakati unapobonyeza tumbo lako.


Nini Cha Kufanya Ikiwa Una Dalili Hizi?

Ikiwa una dalili zilizoorodheshwa hapo juu, wasiliana na daktari wako haraka kwani unahali inaohitaji matibabu ya zaidi kama vile:

  • Kusafisha kizazi kwa kutumia dawa.

  • Kufanyiwa upasuaji mdogo wa kusafisha kizazi ikiwa tishu za ujauzito hazijatoka kikamilifu.

  • Dawa za kutibu au kuzuia maambukizi kwenye kizazi kama kuna hatari ya maambukizi.


Rejea za mada hii:
  1. World Health Organization. Medical management of abortion. Geneva: WHO; 2018.

  2. Kapp N, Blanchard K, Coast E, Ganatra B, Harries J, Footman K, et al. Developing a forward-looking agenda and methodologies for research of self-use of medical abortion. Contraception. 2018;97(2):184–8.

  3. Grossman D, Grindlay K. Safety of medical abortion provided through telemedicine compared with in person. Obstet Gynecol. 2017;130(4):778–82.

  4. Raymond EG, Grimes DA. The comparative safety of legal induced abortion and childbirth in the United States. Obstet Gynecol. 2012;119(2 Pt 1):215–9.

  5. National Abortion Federation. Clinical Policy Guidelines. Washington DC: NAF; 2020.

  6. Gynuity Health Projects. Providing medical abortion with mifepristone and misoprostol. New York: Gynuity Health Projects; 2021.

  7. American College of Obstetricians and Gynecologists. ACOG Practice Bulletin No. 225: Medication abortion up to 70 days of gestation. Obstet Gynecol. 2023;141(2):e1-e17.

Imeandikwa:

8 Juni 2025, 07:17:02

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

bottom of page