top of page
Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

ULY CLINIC

7 Juni 2025, 18:50:47

Damu au kinyama mimba ya mwezi mmoja ikiharibika (1).jpg

Dawa ya kurudisha hedhi

Swali la msingi


Habari za leo dkt. dawa za kurudisha hedhi ni zipi?


Majibu

ree

Dawa ya kurudisha hedhi inategemea chanzo cha tatizo. Hedhi kuchelewa au kukoma kunaweza kutokana na mambo mbalimbali kama;

  • Mabadiliko ya homoni (hasa estrojeni na projesteroni)

  • Msongo wa mawazo

  • Uzito kupita kiasi au kupungua sana

  • Matatizo ya tezi (thairoid)

  • Sindromu ya ovari yenye vifukomaji vingi

  • Mimba

  • Matumizi ya dawa fulani


Dawa zinazoweza kutumika kwa ushauri wa daktari


Provera (medroxyprogesterone acetate)

Hii ni dawa ya homoni (projesteroni) inayotolewa kwa siku kadhaa, kisha hedhi huanza baada ya kuacha.


Primolut-N (norethisterone)

Hutumika pia kudhibiti au kurudisha mzunguko wa hedhi.


Clomid (clomiphene citrate)

Hutumika zaidi kwa wanawake wanaotaka kupata mimba, hasa wanaoishi na sindromu ya ovari yenye vifukomaji vingi na hawapati uovuleshaji.


Vidonge vya uzazi wa mpango

Zinaweza kusaidia kurudisha mzunguko wa kawaida wa hedhi.


Tiba mbadala au ya asili

  • Tangawizi, mdalasini, au manjano: Hivi vinaaminika kusaidia kuchochea damu ya hedhi, ingawa ushahidi wa kisayansi ni mdogo.

  • Mazoezi ya mwili: Yanaweza kusaidia kurudisha mzunguko wa kawaida hasa kama uzito ni sababu.


Tahadhari

Usianze kutumia dawa yoyote kabla ya kwenda hospitali kupima (hasa ujauzito na vipimo vya homoni). Daktari au mtaalamu wa afya atakupa dawa sahihi kulingana na sababu ya kuchelewa kwa hedhi.


Rejea za mada hii:

  1. Medroxyprogesterone (Provera): Uses, Side Effects, Dosage & Reviews [Internet]. GoodRx; 2023. Imechukuliwa 10.04.2025 kutoka: https://www.goodrx.com/medroxyprogesterone/what-is

  2. Norethisterone: Adult Medication Guideline [Internet]. Department of Health, Western Australia; 2021. Imechukuliwa 10.04.2025 kutoka: https://www.kemh.health.wa.gov.au/~/media/HSPs/NMHS/Hospitals/WNHS/Documents/Clinical-guidelines/Obs-Gyn-MPs/Norethisterone.pdf

  3. Clomid (Clomiphene Citrate) Information for Patients [Internet]. Manchester University NHS Foundation Trust; 2013. Imechukuliwa 10.04.2025 kutoka: https://mft.nhs.uk/app/uploads/sites/4/2018/04/13-05-Clomid-October-2013.pdf

  4. Medroxyprogesterone Uses, Dosage & Side Effects [Internet]. Drugs.com; 2024. Imechukuliwa 10.04.2025 kutoka: https://www.drugs.com/medroxyprogesterone.html

  5. Ovulation Induction with Clomiphene Citrate [Internet]. UpToDate; 2024. Imechukuliwa 10.04.2025 kutoka: https://www.uptodate.com/contents/ovulation-induction-with-clomiphene-citrate

  6. Primolut N (Norethisterone): How Does it Work? [Internet]. Care Gynaecology; 2021. Imechukuliwa 10.04.2025 kutoka: https://www.caregynaecology.com.au/wp-content/uploads/2021/07/Primolut-N-Norethisterone-1.pdf 

  7. Chrousos GP. Stress and disorders of the stress system. Nat Rev Endocrinol. 2009 Jul;5(7):374-81. doi: 10.1038/nrendo.2009.106. Epub 2009 Jun 2. PMID: 19488073.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

bottom of page