Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULY CLINIC
17 Juni 2025, 06:34:24
Homa baada ya chanjo
Kwanini homa hutokea baada ya chanjo?
Chanjo hutayarisha mfumo wa kinga ya mwili kuulinda dhidi ya virusi au bakteria wanaoweza kuleta ugonjwa. Homa hutokea kwa sababu chanjo huwa na viunda vya vijidudu vinavyoamsha mwitikio wa kinga ya mwili. Hata hivyo, chanjo hazisababishi ugonjwa halisi kama vile vimelea asili vinavyofanya mtu kuugua. Kwa baadhi ya watu, mwitikio wa kinga huwa na nguvu ya kutosha kusababisha dalili kama homa kali.
Nini unapaswa kufanya unapopata homa?
Mara nyingi si lazima kutumia dawa za kushusha homa kama paracetamol baada ya chanjo. Inashauriwa kunywa maji ya kutosha. Kama homa ni kali au inakupelekea kukulaza, tafadhali wasiliana na daktari kwa ushauri zaidi.
Rejea za mada hii
Ahn SH, Zhiang J, Kim H, Chang S, Shin J, Kim M, Lee Y, Lee JH, Park YR. Postvaccination Fever Response Rates in Children Derived Using the Fever Coach Mobile App: A Retrospective Observational Study. JMIR Mhealth Uhealth. 2019 Apr 22;7(4):e12223. doi:10.2196/12223. Erratum in: JMIR Mhealth Uhealth. 2020 May 7;8(5):e18921. PMID: 31008712; PMCID: PMC6658305.
Children's Hospital of Philadelphia. Fever and Vaccines [Internet]. Available from: https://www.chop.edu/centers-programs/vaccine-education-center/vaccine-safety/fever-and-vaccines. Accessed 16 Jul 2022.
Kaiser Permanente. Immunization that causes fever [Internet]. Available from: https://healthy.kaiserpermanente.org/health-wellness/health-encyclopedia/he.immunizations-that-may-cause-fever.not35603/. Accessed 16 Jul 2022.
Seattle Children’s. Immunization Reactions [Internet]. Available from: https://www.seattlechildrens.org/conditions/a-z/immunization-reactions/#:. Accessed 16 Jul 2022.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
