top of page
Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

ULY CLINIC

15 Juni 2025, 09:47:11

Damu au kinyama mimba ya mwezi mmoja ikiharibika (1).jpg

Ishara ya mimba kutoka

Swali 1.

Je, inawezekana kutokwa na damu nyingi na ya mabonge bila maumivu yoyote na mimba kuendelea kuwepo?


Jibu:


Ndio


Njia ya kufahamu mimba imetoka kwa dalili

Kutokwa damu ya mabonge baada ya kutumia dawa ya kutoa mimba inaweza maanisha mimba imetoka au la. Mara nyingi mimba ikitoka damu yake huwa nyingi na kuambatana na maumivu ya tumbo yanayoweza kuwa ya kawaida au makali. Damu inayotoka huambatana na tishu za ujauzito au viungo vya mwili wa mtoto na hivi hutegemea mimba ilikuwa na umri gani.


Kwa mimba ya chini ya mwezi mmoja, kiasi cha damu kinachotoka huzidi kidogo damu ya hedhi na wakati mwigine huwa kama ya hedhi.


Je, unafahamu vipi mimba imetoka?

Njia pekee ya kufahamu mimba imetoka ni kwa kufanya kipimo cha ujauzito ambacho majibu yake huwa sahihi ukipima angalau wiki la pili toka umetoa mimba. Hii ni kwa sababu katika kipindi hiki, kiwango cha homoni ya jauzito(HCG) kwenye mkojo huwa kidogo kuweza kutambuliwa na kipimo na hivyo ukipima wakati huu mimba haitaonekana endapo imetoka. Inashauriwa kutumia mkono wa asubuhi unapoamka kwa kuwa huwa na kiwango kikunwa cha homoni hii endapo mimba ipo.


Njia zingine mbali na kipimo cha mkojo ya kufahamu kuwa mimba imetoka

Njia nyingine ya haraka inayoweza kutumika ni kwa kutumia kipimo cha picha mionzi sauti(ultrasound) ya kizazi. Kipimo hiki hutambua kama tishu za mimba zimeshatoka kwenye kuta za mji wa mimba au la. Licha ya kuwa kipimo kizuri kutambua mapema kuwa mimba imetoka au la, majibu ya kipimo hutegemea uwezo na uzoefu wa mpigaji picha kupiga na kutafsiri.


Wapi unaweza kupata maelezo zaidi?

Soma zaidi kwenye makala nyingine kuhusu kutoa mimba kwa dawa katika tovuti hii.


Rejea za mada hii
  1. World Health Organization (WHO). Safe abortion: technical and policy guidance for health systems. 2nd ed. Geneva: WHO; 2012.

  2. Raymond EG, Harrison MS, Weaver MA. Efficacy of misoprostol alone for first-trimester medical abortion: a systematic review. Obstet Gynecol. 2019;133(1):137–47.

  3. Chen MJ, Creinin MD. Mifepristone with buccal misoprostol for medical abortion: a systematic review. Obstet Gynecol. 2015;126(1):12–21.

  4. American College of Obstetricians and Gynecologists (ACOG). ACOG Practice Bulletin No. 225: Medical management of first-trimester abortion. Obstet Gynecol. 2020;136(4):e31–e47.

  5. Grossman D, Blanchard K, Blumenthal P. Complications after medical abortion: a review. Am J Obstet Gynecol. 2004;190(2):S54–S59.

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

bottom of page