top of page
Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:

Dr.Sospeter Mangwella, MD

ULY CLINIC

4 Agosti 2025, 12:37:04

Damu au kinyama mimba ya mwezi mmoja ikiharibika (1).jpg

Kumwaga shahawa zenye damu| ULY CLINIC

Nina tatizo la kukojoa damu badala ya shahawa kwenye tendo la ndoa na sina maumivu yoyote wala ugonjwa wa zina wowote je shida ni nini?

HIli ni swali ambalo limeulizwa mara kwa mara na watumiaji wa tovuti ya ULY CLINIC. Majibu yake ningependa kuyaelezea hapa chini


Mwanaume anapo mwaga mbengu wakati wa kujamiana, mbengu hizo huwa na mchanganyiko wa majimaji yaliyotolewa katika tezi mbalimbali kwenye mfumo wa uzalishaji mbegu  ikiwapo tezi dume. Shahawa  na majimaji hupita katika mirija mbalimbali hadi kufikia kwenye mrija unatoa mkojo nje ya mwili yaani urethra, njia hizi huwa na mishipa ya damu na hivyo endapo kuna tatizo katika mirija hiyo kama maambukizi au matatizo mengine mbalimbali, hupelekea kuvilia damu ndani ya mirija  na kuonekana kama  mchanganyiko  wa damu kwenye shahawa au mkojo.


Soma zaidi kuhusu visababishi kwa kubonyeza hapa

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

bottom of page