Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULY CLINIC
17 Juni 2025, 08:30:48
Lenge la usaha
Lenge usaha hufahamika pia kama pustule aina ya jeraha la ngozi ambalo huonekana kama mwinuko mdogo juu ya ngozi wenye kioevu cha usaha ndani yake. Usaha huu unaweza kuwa ishara ya maambukizi ya bakteria, fangasi, au hata kuwa bila maambukizi kama inavyoonekana kwa baadhi ya wagonjwa wa soriasis ya kipistula
Muonekano lenge usaha
Lenge dogo lilioinuka juu ya ngozi
Rangi nyeupe, ya manjano au kijani hafifu
Hujazwa na usaha unaoonekana wazi
Huweza kuuma, kuwasha au kuwa laini kwa mguso
Visababishi vya lenge usaha
Maambukizi ya bakteria – kama vile impetigo au folliculitis.
Maambukizi ya fangasi – kama tinea sugu inayoweza kuambatana na pustule.
Soriasis ya pustul – hali ya kinga ya mwili inayosababisha upele wenye usaha bila maambukizi.
Acne vulgaris – chunusi zinazojitokeza na usaha.
Hali zingine za kinga – kama vile Michomokinga ya vena na lupas.
Utambuzi
Hutegemea muonekano wa kliniki
Uchunguzi wa usaha (Kuotesha vimelea)
Biopsy ya ngozi (kwa magonjwa yasiyo ya maambukizi)
Kipimo cha ngozi (skin scraping kwa fangasi)
Tiba
Maambukizi ya bakteria – hutibiwa kwa antibioticki ya kupaka au ya kumeza.
Pustule zisizoambukiza – hupatiwa dawa za kupunguza uvimbe (kama kortikosteroid ya akupaka au immunomodulator).
Kujitibu nyumbani – usafi wa ngozi, epuka kukwangua au kubinya pustul, tumia antiseptiki nyepesi.
Hitimisho
Pustule ni jeraha la kawaida linaloweza kuwa na chanzo tofauti. Ni muhimu kutambua iwapo kuna maambukizi au hali nyingine ya ngozi ili kutoa matibabu sahihi na kuzuia madhara ya muda mrefu.
Rejea za mada hii
James WD, Berger TG, Elston DM. Andrews’ Diseases of the Skin: Clinical Dermatology. 13th ed. Philadelphia: Elsevier; 2019.
Habif TP. Clinical Dermatology: A Color Guide to Diagnosis and Therapy. 6th ed. Elsevier; 2015.
Bolognia JL, Schaffer JV, Cerroni L. Dermatology. 4th ed. Elsevier; 2017.
Korman NJ. Management of psoriasis as a systemic disease: what is the evidence? Br J Dermatol. 2020;182(4):840-848. doi:10.1111/bjd.18123
World Health Organization. Skin conditions. [Internet]. 2023 [cited 2025 Jun 17]. Available from: https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/skin-diseases
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
