top of page
Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:

Dkt. Glory, MD

ULY CLINIC

28 Januari 2026, 13:11:58

Damu au kinyama mimba ya mwezi mmoja ikiharibika (1).jpg

Magonjwa yanayotibiwa na mlonge

Mlonge (Moringa oleifera) ni mmea wenye thamani kubwa kiafya na unatumiwa kutibu na kusaidia katika kudhibiti magonjwa mbalimbali kutokana na wingi wa virutubisho na viambata vyenye uwezo wa kitiba. Makala hii imeorodhesha baadhi ya magonjwa yanayodhibitiwa au yanayotibiwa na mlonge;


Ugonjwa wa kisukari

Majani ya mlonge yana uwezo wa kupunguza viwango vya sukari kwenye damu, hivyo kusaidia wagonjwa wa kisukari kudhibiti ugonjwa huu, Tafiti zinaonyesha pia kuwa mlonge huongeza uzalishaji wa kichohceo insulini na kuboresha utendaji kazi wa kongosho, kwa kufanya hivi huweza kudhibiti kisukari.


Shinikizo la juu la damu

Mlonge una kiasi kikubwa cha potasiamu, ambacho husaidia kupunguza shinikizo la damu, potasiumu hufanya kazi ya kupanua mishipa ya damu hivyo kupelekea kushuka kwa shinikizo. Viuajisumu vilivyoshamiri katika mlonge husaidia kuimarisha afya ya moyo na mishipa ya damu.


Magonjwa ya Ini

Mlonge una viambata vinavyosaidia kulinda ini dhidi ya sumu na kuimarisha uwezo wake wa kutoa sumu mwilini. Husaidia pia kurekebisha uharibifu wa ini unaosababishwa na matumizi mabaya ya pombe au dawa.


Upungufu wa damu

Mlonge una madini ya chuma na vitamini C ambayo husaidia kuongeza uzalishaji wa chembe nyekundu za damu na hivyo husaidia wagonjwa kurejesha kiwango cha damu katika hali ya kawaida.


Magonjwa ya mfumo wa kinga

Majani ya mlonge yana vitamini C na E nyingi ambazo husaidia kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya maambukizi. Pia yana viambata vyenye uwezo wa kupambana na bakteria na virusi.


Magonjwa ya udhaifu wa mifupa na maungio ya mwili

Mlonge una kalsiamu na fosforasi nyingi ambazo ni muhimu kwa uimara wa mifupa. Pia una sifa za kupunguza maumivu na uvimbe katika viungo.


Magonjwa ya tumbo na matatizo ya mmeng’enyo wa chakula

Mlonge husaidia kupunguza vidonda vya tumbo na gesi, na kuvimbiwa kwa kuongeza usagaji mzuri wa chakula.


Magonjwa ya ngozi

Mafuta ya mbegu za mlonge yanaweza kutumika kutibu chunusi, upele, na mikunjo ya ngozi kwa sababu yana sifa za kuwa na viuajibakteria na vizuia michomo kinga.


Saratani

Baadhi ya tafiti zinaonyesha kuwa mlonge una viambata vinavyoweza kusaidia kupunguza kasi ya ukuaji wa seli za saratani na pia husaidia mwili kuondoa sumu ambazo zinaweza kusababisha saratani.


Magonjwa ya macho

Mlonge una vitamini A kwa wingi inayosaidia kulinda macho dhidi ya matatizo kama upofu wa usiku na matatizo mengine ya kuona


Jinsi ya kutumia mlonge kwa tiba

  • Majani – Hutumiwa kama chai, juisi, au unga kwenye chakula.

  • Mbegu – Huliwa moja kwa moja au kusagwa kuwa unga kwa detox.

  • Mafuta ya Mlonge – Hutumika kwa ngozi na nywele.

  • Gome na Mizizi – Hutumiwa kwa tiba za kienyeji, lakini zinahitaji tahadhari.


Jinsi ya Kutumia Mlonge kwa Tiba – Kina na Faida

Sehemu ya Mlonge

Namna ya Kutumia (Kiasi, Muda, Mara)

Faida Zinazopatikana

Majani

Chai: Majani 2–3 ya kijiko cha chai kwa kikombe 1 cha maji moto, acha ichemshe 5–10 min, kunywa 1–2 vikombe kwa siku (asubuhi/mchana), angalau wiki 2–4.


 Juisi: Majani 3–5 kwenye juisi ya matunda/mboga, kunywa mara 1–2 kwa siku.


Unga kwenye chakula: Ongeza 1–2 vijiko vya unga wa majani kwenye chakula cha kila siku.

  • Hupunguza sukari kwenye damu (msaada kwa wagonjwa wa kisukari)

  • Huongeza kinga ya mwili

  • Husaidia mmeng’enyo wa chakula

  • Huimarisha afya ya moyo na mishipa ya damu

Mbegu

Huliwa moja kwa moja: Mbegu 5–10 kila siku, asubuhi.


 Unga wa detox: Mbegu 1–2 zilizosagwangwa, mchanganyiko kwenye maji/juisi, kunywa mara 1 kwa siku, angalau wiki 2–4.

  • Husaidia kuondoa sumu mwilini

  • Huimarisha afya ya moyo na kupunguza cholesterol

  • Huongeza nishati na kuimarisha kinga

Mafuta ya Mlonge

Ngozi: Tumia 2–3 vijiko vidogo kwa eneo la ngozi, mara 1–2 kwa siku, angalau wiki 3–4.


 Nywele: Tumia 1–2 vijiko kwenye nywele/mizizi, acha 30–60 min, suuza, fanya mara 2–3 kwa wiki.

  • Hutoa unyevu na kuondoa mikunjo kwenye ngozi

  • Huondoa chunusi na upele

  • Huimarisha nywele, kuondoa kavu na kupasuka kwa nywele

Gome na Mizizi

Mchemsho wa mizizi na gome: Vijiko 1–2 kwa kikombe 1 cha maji, chemsha 10–15 min, kunywa 1–2 vikombe kwa siku, angalau wiki 1–2.

  • Husaidia matatizo ya tumbo na mmeng’enyo

  • Huondoa maumivu ya misuli na viungo

  • Husaidia kupunguza uvimbe na kuimarisha kinga


Kumbuka: Kuelewa kuhusu dozi halisi na matumizi ya kitiba wasiliana na daktari wako wa tiba asili kwa ushauri.



Tahadhari na Watu Wasiopaswa Kutumia Mlonge

  1. Wanawake wajawazito na wanaonyonyesha – hasa gome na mizizi, kwani vinaweza kusababisha contractions au kuathiri mtoto.

  2. Wagonjwa wenye shinikizo la damu chini sana – majani na gome vinaweza kupunguza shinikizo zaidi.

  3. Wagonjwa wenye matatizo ya figo au ini – mbegu, gome, au majani makubwa bila ushauri wa daktari inaweza kuwa hatari.

  4. Wale wanaotumia dawa za kudhibiti sukari – majani yanaweza kuongeza hatari ya sukari kushuka sana.

  5. Watu wenye ngozi nyeti – jaribu mafuta ya mlonge kidogo kwanza ili kuangalia kama hakuna upele au muwasho.


Maswali yaliyoulizwa mara kwa mra na majibu yake

Mlonge ni nini na unasaidia nini?

Mlonge ni mmea wenye virutubisho vingi unaosaidia kudhibiti sukari, shinikizo la damu, upungufu wa damu, afya ya ini, kinga ya mwili, ngozi, nywele, na mmeng’enyo wa chakula.

Ninaweza kutumia majani ya mlonge mara ngapi kwa siku?

Unaweza kunywa chai au juisi ya majani 1–2 vikombe kwa siku, au kuongeza unga kwenye chakula cha kila siku.

Mbegu za mlonge zinatumiwa vipi?

Mbegu huliwa moja kwa moja 5–10 kila siku au kusagwa kuwa unga kwenye maji au juisi mara 1 kwa siku.

Mafuta ya mlonge yanatumika kwa nini?

Hutumika kwenye ngozi kuondoa mikunjo, chunusi, upele, na kwenye nywele kuondoa kavu na kuimarisha nywele.

Gome na mizizi ya mlonge yanatumika vipi?

Huchemshwa kwenye maji (kupata mchemsho) na kunywa 1–2 vikombe kwa siku, angalau wiki 1–2, kusaidia matatizo ya tumbo, maumivu ya misuli, na uvimbe.

Je, mlonge unaweza kusaidia wagonjwa wa kisukari?

Ndiyo, majani ya mlonge hupunguza sukari kwenye damu na huongeza uzalishaji wa insulin.

Ni faida gani nyingine za mlonge?

Huongeza kinga ya mwili, hupunguza uvimbe, husaidia mmeng’enyo wa chakula, huimarisha afya ya moyo, mishipa, nywele, na ngozi.

Watu gani hawapaswi kutumia mlonge bila ushauri?

Wanawake wajawazito/wanaonyonyesha, wagonjwa wenye shinikizo la chini, wagonjwa wenye matatizo ya figo au ini, na wale wanaotumia dawa za kudhibiti sukari.

Ni muda gani wa kuona faida za mlonge?

Matumizi ya mara kwa mara kwa angalau wiki 2–4 huanza kuonyesha faida katika sukari, mmeng’enyo, na nishati; ngozi na nywele huchukua wiki 3–4.

Je, mlonge una madhara yoyote?

Kwenye kipimo kilichopendekezwa, mlonge ni salama. Hata hivyo, kutumia gome/mizizi au kipimo kikubwa bila ushauri wa daktari kunaweza kusababisha kizunguzungu, kuhara, au kushuka kwa shinikizo la damu.


Rejea za mada hii
  1. Pareek A, et al. Moringa oleifera: An Updated Comprehensive Review of Its Pharmacological Activities, Ethnomedicinal, Phytopharmaceutical Formulation, Clinical, Phytochemical, and Toxicological Aspects. Int J Mol Sci. 2023 Jan 20;24(3):2098. doi: 10.3390/ijms24032098. PMID: 36768420; PMCID: PMC9916933.

  2. Fuglie L.J. Producing Food without Pesticides: Local Solutions to Crop Pest Control in West Africa. 1st ed. Church World Service; Dakar, Senegal: 1998. pp. 1–158.

  3. Gandji K.,et al. Status and utilisation of Moringa oleifera Lam: A review. Afr. Crop Sci. J. 2018;26:137–156. doi: 10.4314/acsj.v26i1.10.

  4. Chaudhary K., Chourasia S. Nutraceutical properties of Moringa oleifera: A review. EJPMR. 2017;4:646–655.

  5. Gopinath L.R., Jeevitha S., Gokiladevi T., Archaya S. Isolation and Identification of therapeutic compounds from Moringa oleifera and its antimicrobial activity. IOSR-JPBS. 2017;12:1–10.

  6. Kasolo J.N.,et al. Phytochemicals and uses of Moringa oleifera leaves in Ugandan rural communities. J. Med. Plant Res. 2010;20104:753–757.


Imeandikwa:

8 Juni 2025, 06:50:13

ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.

Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba

bottom of page